Kihistoria, Nazareti ulikuwa ni mji mdogo sana wa wakulima na mafundi uliokuwa chini ya ukoloni wa Kirumi. Huyu mwanamke alikuwa mke wa fundi seremala na alikuwa anaongea lugha ya Kiaramu kwa lafudhi ya kishamba ya kule Galilaya. Hiyo ndio primary identity yake kisayansi.
Mkuu ukienda kwenye ukweli wa maandiko ya kale, utagundua kitu kimoja cha kushangaza. Vitabu vya kwanza kabisa vya Biblia havitaji neno Zizi la Ng'ombe, na Quran haisemi kuwa alikuwa peke yake jangwani bila sababu.
Biblia Inasema tu kuwa baada ya kumzaa, alimfunga nepi na akamlaza kwenye hori la kulia ng'ombe kwa sababu hawakupata nafasi kwenye nyumba ya wageni. Kwenye utamaduni wa Kiyahudi wa karne ya kwanza, watu walikuwa wanahifadhi wanyama wao kwenye pango la chini ya nyumba zao au nje kidogo ya nyumba.
Quran yenyewe huwa inasema uchungu ulimshika akajisogeza karibu na shina la mti wa mtende ili kupata hifadhi, kivuli, na chakula.
Kwahiyo Kihistoria, mazingira yote mawili yanaelezea kitu kile kile kimoja, moja inazingatia pale mtoto alipolazwa na nyingine inazingatia mazingira ya asili yaliyomzunguka mama wakati wa uchungu.
Maria anabaki kuwa ni mmoja yule yule aliyepitia hayo mazingira magumu.