Watu 10 maarufu zaidi kuwahi kutokea duniani

Watu 10 maarufu zaidi kuwahi kutokea duniani

1. Jesus
2. Muhammad
3. Wako Jako
4.....
5.....

Tupaki mtoe katika hiyo list, hana umaarufu wa kumuweka kwenye hiyo list.
Mkuu unajua ushawishi na umaarufu ni vitu viwili tofauti. Wanaotaka Mohamad akae juu naona kama wame-base sana kwenye kigezo cha ushawishi wakati orodha inaongelea umaarufu.

Umaarufu ni kujulikana tu. Ushawishi ni namna mtu ana-influence maamuzi ya wengine. Mohamad ana ushawishi mkubwa. Lile nyomi linaendaga macca sio mchezo lakini ukija kwenye umaarufu sina uhakika sana kama kawazidi wakina Michael Jackson.

Leo hii tukikusanya makundi ya watoto, watu wazima na wazee. Tuwaulize wanamjua nani kati ya ronaldo na Mohamad, una uhakika Mohamad atapata kura nyingi zaidi?
 
Huyu dogo atakuwa Gen Z hafikiri sawa sawa. Baba wa babu yangu aliyefariki 1986 anamjua Ronaldo?
Kama kawaida ya wabongo. Very easily to be provoked. Introduction imetoa mwanya wa orodha kurekebishika. Lilikua ni suala la kuonyesha tu makosa na kusema usahihi wake.
 
Kama kawaida ya wabongo. Very easily to be provoked. Introduction imetoa mwanya wa orodha kurekebishika. Lilikua ni suala la kuonyesha tu makosa na kusema usahihi wake.
Sasa mbona wewe ndiye umekuwa provoked. You are too shallow in world affairs.
List gani hiyo haina Isaac Newton?
Unamuweka Tupac😀😃😀
Au hiyo ni list yako ya karne ya 21?
 
Ni uchizi watu wa zamani huko kwenye karne kuwaweka na hawa wa milenia

Na kama ni hivyo basi maarufu wangekuwa akina Ibrahim, Mussa, Adamu, Firauni, Yesu, Muhammad na ukiongeza na wa sasa ni kina trump, netanyahu, rais wa iran, mimi nk
 
Mkuu unajua ushawishi na umaarufu ni vitu viwili tofauti. Wanaotaka Mohamad akae juu naona kama wame-base sana kwenye kigezo cha ushawishi wakati orodha inaongelea umaarufu.

Umaarufu ni kujulikana tu. Ushawishi ni namna mtu ana-influence maamuzi ya wengine. Mohamad ana ushawishi mkubwa. Lile nyomi linaendaga macca sio mchezo lakini ukija kwenye umaarufu sina uhakika sana kama kawazidi wakina Michael Jackson.

Leo hii tukikusanya makundi ya watoto, watu wazima na wazee. Tuwaulize wanamjua nani kati ya ronaldo na Mohamad, una uhakika Mohamad atapata kura nyingi zaidi?
Umaruufu bado Mohamed ni maarufu kaka kuliko wengi hapo.
Ulipo uislam hata kwa uchache basi wanamjua huyo mtu hata kama sio waislam.

Japo hata mimi nakiri kumjua baadae kidogo ila kusema Tupac na Pele ni maarufu kumliko ni urongo.

Pele na Maradona ni mpaka uwe unafatilia mpira, tupac ndo kabisaaa.
 
Ni uchizi watu wa zamani huko kwenye karne kuwaweka na hawa wa milenia

Na kama ni hivyo basi maarufu wangekuwa akina Ibrahim, Mussa, Adamu, Firauni, Yesu, Muhammad na ukiongeza na wa sasa ni kina trump, netanyahu, rais wa iran, mimi nk
Jesus na Mohamad ni maarufu kipindi chote, MJ anawekwa kwenye list nadhani kwasababu kwa miaka ya karibuni hakuna aliemfikia kwa umaarufu.
 
HAkuna kafir asiemjua Muhammad hata uko utotoe ndani ndani wanamjua

Punguza ujinga, makafir wote mnafundishwa kanisan kama Muhammad aling'atwa tako na nguruwe na mbakaj uko makanisan kwenu toka mkiwa watoto

Hakuna kafir asiemjua Muhammad na hakuna kobaz asiemjua Yesu


Punguza ujinga
Kwaiyo dunia nzima ndio wanaishi hao kafiri na kobazi? Halafu nilikua hata sijui hiyo story ya Mohamad kung'atwa tako
 
Ni uchizi watu wa zamani huko kwenye karne kuwaweka na hawa wa milenia

Na kama ni hivyo basi maarufu wangekuwa akina Ibrahim, Mussa, Adamu, Firauni, Yesu, Muhammad na ukiongeza na wa sasa ni kina trump, netanyahu, rais wa iran, mimi nk
Unajua madingi wa zamani na sisi vijana wa milenia sometimes tunazingua sana. Kila kitu gen z hivi gen z vile kama vile sisi tulifanya chochote cha maana kufikia tulipo leo

Ukiangalia wapiga dili maofisini ni sisi, tulioruhusu katiba mbovu ni sisi, tulioruhusu nchi kuwa shamba la bibi tangu enzi za kikwete ni sisi lakini tukianza kuwaponda gen z sasa...
 
Orodha hii sio rasmi, ni utafiti wangu binafsi. Unapingika, unajadilika na unarekebishika.

10.Mohamad.
Huyu ni muasisi wa dini ya kiislamu. Alikua mwanamapinduzi, askari na mwanasiasa. Kulingana na imani ya waislamu ndie mjumbe wa mwisho wa Mungu. Jina lake ni maarufu sana duniani. Changamoto umaarufu wake unaishia kwenye nchi za kiislamu au ambazo angalao dini ya kiislamu imeenea. Katika nchi ambazo hakuna kabisa uislamu sio ajabu kumkuta mtu mzima kabisa hajui chochote kuhusu Mohamad.

9.Bob Marley.
Mwanamziki wa muziki aina ya reggae. Huyu jamaa ndio taswira ya huu mziki. Nyimbo zake aliamasisha zaidi masuala ya ukombozi na kujenga umoja, upendo na mshikamano.
View attachment 3636620

8.Pele na Maradona.
Nimeshindwa kuwatenganisha hawa jamaa wawili maana umaarufu wao ni kama upo kwenye mzani sawa. Ni wachezaji mahiri ambao waliu-define mchezo wa mpira wa miguu. Pele ni mzaliwa wa Brazil na Maradona ni mzaliwa wa Argentina. Pele alianza kucheza mpira miaka mingi kidogo kumzidi Maradona. Pamoja na kuwepo kwa wachezaji wengine mahiri hapa duniani lakini Pele na Maradona ni kama wameshajijengea daraja lao ambalo hakuna mchezaji mwingine anaweza kuvuka.
View attachment 3636621

7.Bruce Lee.
Alitambulika kwa umahiri wake wa upiganaji wa mtindo wa karate na kong fu. Kumekua na mjadala watu wakihoji kama Bruce Lee ndie mpiganaji mahiri zaidi kutokea. Wanaipinga hilo suala hoja wanayoitumia ni kwamba jamaa hakuwahi kushiriki na kushinda mashindano rasmi. Ngumi zake ni za kwenye movie na sanaa za maonyesho tu. Lakini pamoja na hayo bado haiondoi ukweli Bruce ni moja ya watu maarufu zaidi kuwahi kutokea dunian na amekua kioo na role model kwa watu wote wanaopenda kong fu.
View attachment 3636623

6.Tupac.
Alitambulika kwa umahiri wake katika mziki wa rap au hip hop. Nini kilimpa umaarufu Tupac kuzidi wasanii wengine?

Je ni umahiri wa kurap? Sina uhakika kama anawazidi Nas, lil wayne n.k

Je ni ile style yake ya kurap fasta ambayo inahitaji pumzi nyingi? Sina uhakika kama anamzidi Eminem.

Je ni ile ngoma yake ya dear mama? Binafsi nafikiri ile ndio hit song kali ya muda wote ya kumsifia mama( Lucas Mwashambwa, choice variable na machawa wengine nieleweni vizuri hapa. Simaanishi huyo mama yenu mnaomfikiria nyie)

Au ilitokea tu zali mziki wa hip hop ukatengenezewa taswira ya huyu jamaa?
View attachment 3636624

5.Adolf Hitler.
Mwamba huyu hapa. Harakati zake za kutaka kuitawala dunia zilisababisha awe center ya vita ya pili ya dunia. Wayahudi ndio hawataki hata kumsikia huyu muhuni
View attachment 3636626

4. Lionel Messi.
Sina mengi ya kumuongelea huyu jamaa. Kwa kifupi tu inasemekana ndie mchezaji mpira wa miguu mahiri zaidi kuwahi kutokkea duniani. Mashabiki wa soka wa kizazi chake tuna bahati sana ya kumwona huyu jamaa akicheza maana habari zake zitakuwepo juu kabisa kwenye kumbukumbu za kidunia mpaka mwisho wa dohari
View attachment 3636627

3.Cristiano Ronaldo.
Mchezaji wa mpira wa miguu ambaye kwa miaka mingi amekua mshindani wa Messi huku wakiwagawa mashabiki. Umaarufu wake ulianza kupanda kwa kasi baada ya kusajiriwa na manchester united kwa mara ya kwanza akitokea timu ya sporting lisbon ya nyumbani kwake Ureno.

Namba hazidanganyi. Ndie binadamu mwenye wafuasi wengi zaidi katika mitandao yote ambayo yupo active. Style yake ya ushangiliaji inayotambulika kwa jina la siuuu ndio style maarufu zaidi ya ushangiliaji. Ndie mchezaji ambae ni role model wa wachezaji wengi sana mahiri wanaotamba sasa mfano mbappe, vinicious, kravatkhelia, dembele n.k. Ndie mchezaji ambae ni kipenzi zaidi cha watoto.

Tofauti yake na Messi ni kwamba Messi anaonekana kupendwa na wanaopenda mpira pamoja na mashabiki wa timu alizocheza tofauti na Ronaldo anapendwa na hata wasiokua na mapenzi na mpira wa miguu pamoja na mashabiki wa timu ambazo hajacheza.
View attachment 3636628

2.Michael Jackson.
Madogo wa GenZ wanaweza kushangaa kidogo hapa maana hawakuwepo nyakati ambazo huyu jamaa alikua ameiweka dunia chini ya nyayo za miguu yake.

Ndie msanii wa kwanza mweusi wimbo wake kupigwa mtv. Aliibuka katika nyakati ambazo ubaguzi wa rangi umeshamiri kiasi cha kuwepo na sheria ya kuzuia nyimbo za watu weusi kupigwa kwenye baadhi ya station. Wimbo wake wa billie jean ulifanya mtv waondoe huo utaratibu.

Katika prime yake alishawahi kupanda jukwaani na kusimama tu kwa takribani dakika 2. Ukumbi ukalipuka kwa shangwe mpaka watu wakazimia kwa sababu ya furaha isiyo kifani. Just imagine hali hiyo inatokea wakati mtu kasimama tu bila kuimba chochote.

Nyakati zake ilifika hatua super market zikawa zinamtengea muda wa kufanya shopping, yaani akitaka kufanya manunuzi anawasiliana na uongozi wa super market watu wote watoke kwanza ili yeye aingie kufanya manunuzi akiwa peke yake. Maana kila anapoingia shughuli zilikua zinasimama.

Kumbuka hayo yote yalitokea kwenye nyakati ambazo hakuna mitandao ya kijamii
View attachment 3636629

1.Yesu.
Anatambulika katika dini ya ukristo kama masiha. Sidhani kama kuna pembe ya dunia unaweza kwenda leo hii ukakutana na jamii ya watu wanaoishi katika mtindo huu wa modern civilization na hawamjui kabisa Yesu. Najua hapa utaibuka mjadala wa kuhoji. Je, huyu Yesu alishawahi kuwepo duniani au ni fictional character tu?

Wanahistoria nguli wanakubaliana kwamba Yesu ni binadamu halisi alikuwepo. Aliishi uko Bethlehemu, Nazareti na Misri. Alikua fundi selemala na mtabibu wa tiba za jadi(kibongo bongo ni kama hawa wakina dr.mwaka). Pia alikua mwanaharakati anaepingana na mienendo ya watawala(mfano Tundu Lissu kwa sasa). Mafundisho yake yalimsababishia kuwa na mikwaruzano na watawala kiasi cha kufikia kukamatwa na kuhukumiwa kifo.

Madai ya kwamba ni mtoto wa Mungu, alifanya miujiza, alifufuka hayo ni ya kiimani zaidi. Hayana uthibitisho wa kihistoria wala sayansi.

NB: Adam na Hawa hawapo kwenye list kwa sababu hakuna uthibitisho kwamba walikuwepo hapa duniani. Wanahistoria nguli wanasema habari yao ni myth tu za wayahudi.

Hii haiko sawa. Sijaona jina la Professor wetu ndani. mtu mwenye degree mpaka hazielezeki.Degree za aina mbali mbali.Degree za kufika chuo , kusoma, kuandika thesis, kuitetea, na hatimaye kupewe siku hiyo hiyo moja
 
Back
Top Bottom