Watu 19 wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kufundisha vijana mbinu za utajiri

Watu 19 wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kufundisha vijana mbinu za utajiri

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linawashikilia watu 19 wanaodaiwa kuwa matapeli kutoka katika makampuni yanayowarubuni vijana kwa kuwafundisha mbinu za utajiri kupitia njia za mtandaoni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama, amesema kuwa makampuni hayo yamekuwa yakiwaingiza vijana katika mipango isiyo halali ya kupata utajiri, na kwa sasa jeshi hilo linafanya uchunguzi kubaini uhalali wa shughuli zao.

Aidha, Mkama amebainisha kuwa katika kipindi cha Januari hadi Machi mwaka huu, jumla ya vijana 399 wameokolewa kutoka mikononi mwa watu hao waliokamatwa.

Jeshi la Polisi limewataka vijana kuwa makini na matangazo yanayoahidi utajiri wa haraka, huku likiendelea na uchunguzi zaidi juu ya suala hili.

 
QNET.. Hao jamaa walinisumbua sana mwaka jana, kuna rafiki yangu mmoja hivi hadi leo amenichukia kisa nilikataa kujiunga.

Walitaka kuniuzia saa kwa 7.5M kutoka Malaysia.

Wanavyuo wengi wanatapeliwa sanaaa.
 
Back
Top Bottom