Watu 20 wahofiwa kufariki baada ya basi walilokuwa wakisafiria kugongana na lori mjini Nzega, leo Oktoba 21, 2023

Wapumzike kwa amani. Truly sad
 
Uwezo wa kiakili wa madereva na barabara haziruhusu gari kwenda zaidi ya speed 80kph. Hii magari yanayokuja Tz yasiwe na uwezo zaidi ya huo.
 
Dereva wa Lori alikua amesinzia ngoma ikahama njia
 
Mkuu wa Wilaya ya Nzega anamwakilishaje Mkuu wa Mkoa wa Tabora huko Sikonge ambako siyo wilaya ya Nzega?
 
Hivi kwa wastani hii nchi watu wangapi wanakufa kwa ajali kila siku?
 
Nzega na sikonge zote zipo mkoa wa Tabora
Hizo ni wilaya tofauti. Mkuu wa wilaya ya Nzega hahusiki na Sikonge ambayo ina mkuu wa wilaya mwingine. Ni sawa na kusema Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni akamwakilishe Mkuu wa Mkoa wa Dar katika shughuli inayofanyika Temeke Yombo, eti kwa kuwa tu maeneo yote yako mkoa wa Dar.
 
Mungu atulinde sote, tuwa makini watumiaji wote wa barabara.
 
Hyo ajali aisee imeniogopesha sanaa.....uzembe wa dereva wa lorry imewacost abiria na dereva wa basi..

Afu dereva wa lorry katoka mzimaa...

Innalillah wainnailayh rajiuun..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…