Watu kusalia majumbani (total lockdown) hakuepukiki, ndiyo njia pekee ya uhakika itakayo tunusuru na kusambaa kwa Corona nchini

Watu kusalia majumbani (total lockdown) hakuepukiki, ndiyo njia pekee ya uhakika itakayo tunusuru na kusambaa kwa Corona nchini

Wakuu kabisa, makamanda na makomredi wote wa nchi hii kuu iliyotukuka, moja kwa moja kwenye mada.

"Siyo siri tena ugonjwa wa Corona umeingia nchini na sasa unasambaa kwa sababu hatua tulizokuwa tumechukua hakikuwa sahihi."

Ilikuwa ni wazi kuwa ugonjwa huu ulikuwa utakuja kutokea nje ya nchi. Hatukuchukua tahadhari za kutosha kuhakikisha kuwa hakika hautaingia bila hofu.

Hii ni kwa kuwa hatukuwa tumehakiki tumeyafanya haya effectively:

1. mipaka inafungwa
2. wageni wote wanaoingia wanawekwa quarantine siku 14 kabla ya kuruhusiwa kuingia nchini.

Fursa hiyo ya kuudhibiti kabla ya kuingia imeshatutoka kwa maana hatukufanya hivyo na ugonjwa umeshaingia.

Kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi.

Sasa tupo katika hatua ya pili ambapo bahati mbaya zaidi, tukifanya tena makosa ya kutokuwa na umakini kamili kama pale mwanzo sasa itakuwa ndiyo basi tena. Ni vyema kuiona hii kama nafasi ya mwisho kabisa ambayo uzuri ni kuwa kungali mikononi kwetu.

Changamoto kubwa iliyopo katika hatua hii, zaidi iko kwenye kufuatilia watu walio husiana kwa namna yoyote na mgonjwa au mtu mwenye maambuk. Hii ni either directly ama indirectly. Hili ndilo linalowakabili vilivyo kwa sasa:

1. Italy ambako vifo ni zaidi ya 800 kwa siku kwa jana tu.
2. Spain ambako wanaokufa ni zaidi ya 300 kwa siku kwa jana tu.
3. Iran ambako anakufa mtu kila baada ya dakika 10 kufikia jana.
4. Nk nk

Kumuweka mtu kwenye isolation kwa siku 14 tu zinatosha kabisa kumfanya afuzu kuwa hana maambukizi au anayo. Kwa kuwaweka watu kwenye isolation kwa siku 14 tu wagonjwa wote na wazima wote watafahamika.

Kwa kuwaweka watu kwenye isolation kwa siku 28, wagonjwa na waliohusiana nao wote watafahamika na tutakuwa tunaelekea kuumaliza ugonjwa huu.

Hakuna madaladala "total lockdown" ni njia ya kwenda.

Katika lockdown kuna uwezekano wa vifo vya njaa na vifo vya Corona. Ni muhimu kuweka utaratibu wa kuhakikisha kuwa hakuna mtu atakufa kwa njaa. Ni heri ikibidi tushindie uji ili tuwe hai lakini ugonjwa huu uondoke kuliko kula biriani wakati Corona iko mtaani bila kudhibitiwa.

Tunaweza kujizatiti kutumia raslimali zote kuhakikisha watu wetu wote wanajikimu vizuri kwa chakula kwa kadri ya uwezo wetu. Hii ikiwa ni sisi kama sisi, na sisi kama taifa, serikali pia ikiwa ni sehemu ya sisi.

Miradi yote isiyo na udharura iwe ya maendeleo au vinginevyo ni wakati wake saaa wa kusimama. Raslimali zote ziende kwenye kuwawezesha wananchi wote kujikimu. Huwezi kuwa na shughuli za ujenzi wakati unauguliwa. Hii ni common sense.

Bajeti za uchaguzi na shughuli zozote zisizo na lazima kwa sasa zielekezwe kwenye wananchi kujikimu kuhusiana na dharura hii.

Tutakaa lockdown muda mfupi zaidi kama hatutaendelea kupoteza muda zaidi kabla ya kuanza. Wenzetu Rwanda wameanza na wanasonga mbele.

Tunavyochelewa itatugharimu zaidi, kwanza maisha ya watu, siku za lockdown na hata raslimali pesa.

Lockdown haiepukiki ni suala la muda tu. Ni au tunakwenda sasa hali ikiwa si mbaya sana, au tunakwenda tukiwa tumechelewa mno "at our own peril."

Corona ni uzembe wetu isingetufikia, na itatumaliza tusipoamka sasa - ukweli mchungu - JamiiForums

Vita dhidi ya Corona: Rwanda ni mfano wa kuigwa Afrika na wanaweza kusalimika iwapo gonjwa hili litakuwa tiishio na hapa Afrika - JamiiForums

Corona virus: Tunajifunza nini toka kwa wengine? - JamiiForums
Rais amesema tufanye kazi, korona isitutishe. Ww haya mamlaka unayatoa wapi!?
 
Tukisali nyumbani ni sawa.je sadaka itapelekwa wapi na Nani ataipokea

Mkuu kusalia = kubakia hicho ni kiswahili kumbe wewe ulidhani kusali ki Mwamposa Mwamposa?

Hapana mkuu "kusalia majumbani" haikuhusiana na mafuta ya upako hata kidogo bali I kubakia nyumbani.
 
Ni suala la kuchagua tu... kufa kwa njaa au kufa kwa virusi...
sio kila kitu ni cha kuiga,

Eti kwakua umesikia mataifa makubwa yanafanya total lock down, kumbuka uchumi wa mtu mmoja mmoja tulionao watanzania,

ikifanyika lockdown tutaishi siku ngapi tufe wote na njaa kabla virus havijatukuta?
 
Watoyo wote wapo likizo lakini wazazi wao walikua wamejazana kwenye nightclubs na bar usiku baadae wanaenda kuchanganyika na watoto wao
Ninaumia sana kuona uzembe wa namna hii bora hao watoto wangebakia huko shuleni na waalimu wao


Sent from my iPhone using JamiiForums
Vipi wazazi wanaofanya kazi maeneo yenye msongamno mkubwa wa watu?
 
Watoyo wote wapo likizo lakini wazazi wao walikua wamejazana kwenye nightclubs na bar usiku baadae wanaenda kuchanganyika na watoto wao
Ninaumia sana kuona uzembe wa namna hii bora hao watoto wangebakia huko shuleni na waalimu wao


Sent from my iPhone using JamiiForums
Rais kasema.
 
Ni suala la kuchagua tu... kufa kwa njaa au kufa kwa virusi...

Ninadhani kwa njaa ni vigumu dana.

Yesu kama mwanadami alikaa bila kula 40 days. Sembuse ka uji na maji ya kunywa yapo achilia mbali jitihada shirikishi za kuhakikisha kila mtu anaishi?
 
Tanzania bado hatuna uwezo wa

Najia nini nazungumza kijana usipanik

We never argue with fools. Kwa maana nyingi umepuuzwa kama ulivyokuja kipuuzi upuuzi.

Kwenu ni fb mnatafuta nini huku na milegezo yenu?
 
South Africa kwenda total lockdown kwa wiki 3 kuanzia alhamisi. Hii ni wakati wana wagonjwa zaidi ya 110. Yaani tayari ni roho juu ya rojo.

Eeh mola wetu hebu wafungue macho hawa viongozi wetu waweze kuyaona maisha ya watu ni muhimu kuliko faida uchwara za kiuchumi ambazo aghalabu wala hazitapatikana.
 
Spain vifo ndani ya saa 24 zilizopita 426.

Kama hadithi vile.
 
Congo hadi sasa maambukizi 33, vifo 2. Hali inazidi kuwa mbaya.
 
Kabla ya kufanya total lockdown,tupime athari za kiuchumi vs kibaiolojia za corona kwa Africa.
Tusikurupuke,tufanye maamuzi kulingana na kile kinachojiri ndani ya mipaka yetu.
Total lockdown means kuua uchumi wa mtu mmoja mmoja na wa taifa kabisa kwa nchi kama zetu hizi,hivyo linapaswa kuwa suala la mwisho kabisa baada ya kujiridhisha kwamba hakuna jinsi.
pia tupate mfano wa mataifa ambayo lockdown imesaidia kuwaondolea tatizo la corona hadi hivi sasa,na uchumi wake kuathirika kidogo kiasi cha kuweza kuurudisha kirahisi.Maana kama unaweka lockdown halafu tatizo haliondoki,au linaondoka taratibu sana kiasi usichoweza kuvumilia,nadhani unaona nini kitatokea hapo.
 
Kwani Mungu kashindwa kuzuia Corona isiingie makanisani?

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
Uganda case zilizothibitishwa zimepanda tokea 1 hadi 8.

Baadhi ya hawa ni wale waliokuwa waliokuwa quarantine.

Pana wachina walitoroka kwenye quarantine wakielekea DRC. Hii ilikuwa baada ya kukaa quarantine kwa siku 10 baada ya kufika Uganda.

Wamekamatwa kwa agizo la m7. Watafikishwa mahakamani baada ya quarantine mpya kwisha.
 
Kenya wamekuwa 19. Pana padri toka Roma alifika Kenya akafikia kuendesha misa ya wafu naye kathibitishwa na Corona.

Pana naibu gavana alikaidi kukaa quarantine alipowasili tokea ulaya. Akaendelea hadi ofisini kwake, naye kathibitishwa kuwa na hivi virusi. Anatibiwa akipona mahakamani.
 
South Africa confirmed cases zimefika 462 mara sita tokea wiki iliyopita. Ramaphosa anasema total lockdown ni muhimu kuudhibiti huu ugonjwa. Lockdown ya wiki 3 tokea alhamisi itakuwa sasa imeamriwa.

Anasema Ramaphosa lockdown ni lazima katika kuukabili ugonjwa huu. Anasema ni sasa au baadaye, makini baadaye kwa gharama ya maisha ya watu zaidi.

Si Magufuli, Majaliwa wala Kabudi wanaoona hivyo. Tuko sawa sawa kweli katika mafikra? Nini tofauti ya u Doctor au Profesa kwa mwendo huu. No wonder tulijazana kwa babu Loliondo msomi ikiwa mbele zaidi.

Sisi tumerogwa na nani kutoweza kuona logic ndogo ndogo kama hizi?

Sisi siasa siasa tu?
 
Rwanda Lockdown day 3. Wanabakiza na siku 9. Hajafa mtu kwa njaa. Kwa vyovyote wanavuna kwenye kuudhibiti ugonjwa huu.

Duniani kote pamoja jitihada zote ugonjwa unaongezeka isipokuwa Tanzania tu ambako tuna nawa nawa mikono tu? Kweli?
 
Vifo 2 tu...unasema hali mbaya?wenzenu wanakatika 800 per day

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu nasema hali ni mbaya kwa sababu hao wenzetu waliofikia 800 leo nao walianza hivi hivi vifo kidogo kidogo tu.

Kinachotokea kwetu hivi sasa si kigeni na kitapofikia haitakuwa kigeni pia. Kwa mwendo huu muelekea ni huo huo wa 800 na hata zaidi muda si mrefu unaokuja.
 
Back
Top Bottom