Watu kusalia majumbani (total lockdown) hakuepukiki, ndiyo njia pekee ya uhakika itakayo tunusuru na kusambaa kwa Corona nchini

Watu kusalia majumbani (total lockdown) hakuepukiki, ndiyo njia pekee ya uhakika itakayo tunusuru na kusambaa kwa Corona nchini

[emoji16][emoji16][emoji16].
Unaleta vichekesho vya TASAF.
Ebu tuanzie kwako mwenzetu unafanya KAZI GANI?

Sent using Jamii Forums mobile app

Nilichukua muda kidogo kukuelimisha nikidhani unaweza kutambua hatari ilivyo na fursa zilipo kwenye gonjwa hili.

Sinao muda mwingi wa kupoteza na mtu asiyeelewa wala kuwa na nafasi ya kujifunza akaelewa.

Si unajua akili zote kubwa na ndogo zimeumbwa na maulana?

Ukipenda rejea mabandiko yangu yote.

Ningependa mno binafsi na familia yangu, wewe na yule tukanusurika na janga la ugonjwa huu. Hilo halitatokea kwa kukaa tu au kwa hatua zozote zilizopo sasa.

Utanikumbuka kitakapo nuka sawa sawa.

Kwa heri ya kuonana.
 

Uzuri kwa Rwanda wagonjwa hao kwa sasa hawaambukizi wengi kama ambavyo ilivyo kwa hapa kwetu kwa hali ya sasa. Huko hakuna mikusanyiko kabisa kila kitu kimesimama.

Uganda hayuko kwenye lockdown Ila kadhibiti wanao ingia nchini vilivyo. Wengi wa wagonjwa walioongezeka ni wale amvao tayari walikuwa quarantined.

Ni muhimu sana kuona tofauti za hawa wawili na sisi ambao katika hali ya kushangaza tuna hata wagonjwa wa Corona waliofikia kutuhakikishia kuwa huu ugonjwa ni mdogo kuliko mafua.
 
Haujajibu swali.
Mwenzetu UNAFANYA KAZI GANI?..
Ambayo itakuwezesha hata ukikaa ndani wiki 1.
Mambo yako ya yataenda vizuri?
Nilichukua muda kidogo kukuelimisha nikidhani unaweza kutambua hatari ilivyo na guess zilipo kwenye gonjwa hili.

Sinao muda wa kupoteza muda na mtu asiyeelewa wala kuwa na nafasi kujifunza akaelewa.

Si unajua akili zote kubwa na ndogo zimeumbwa na maulana?

Ukipenda rejea mabandiko yangu yote. Ningependa mno binafsi na familia yangu, wewe na yule tukanusurika na janga la ugonjwa huu. Hilo halitatojea kwa kukaa tu au kwa hatua zozote zilizopo sasa.

Utanikumbuka kitakapo nuka sawa sawa. Kwa heri ya kuonana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Haya yalitegemewa na huwa hivyo kwanza had itakapofikia kuwa wagonjwa wote na walioambukizwa wamefagia ndipo sasa hali inaweza kuonyesha kupungua.

Kupungua kunaweza anza kuonekana baada ya hizo siku 14 yaani 11 days to come.

Ni wazi kuwa watafanikiwa wao wameona wakaanza hii vita mapema.
 
Mataifa mengi yanakwenda total lockdown baada ya kuona hiyo ndiyo njia. Haya ni katika mataifa hayo:

Which countries are on coronavirus lockdown and what's going on in Italy?

Wengine wanaoongezeka: Rwanda, South Africa, Uganda, Kenya na wengine wengi wako njia moja. Sisi nani?

China baada ya mafanikio yao ya lockdown kuanzia usiku leo wataanza kuiondoa taratibu kurejea katika maisha ya kawaida isipokuwa jimboni Wuhan.
 
Wakuu kabisa, makamanda na makomredi wote wa nchi hii kuu iliyotukuka, moja kwa moja kwenye mada.

"Siyo siri tena ugonjwa wa Corona umeingia nchini na sasa unasambaa kwa sababu hatua tulizokuwa tumechukua hazikuwa sahihi."

Ilikuwa ni wazi kuwa ugonjwa huu ulikuwa utakuja kutokea nje ya nchi. Hatukuchukua tahadhari za kutosha kuhakikisha kuwa hakika hautaingia.

Hii ni kwa kuwa hatukuwa tumehakiki tumeyafanya haya effectively:

1. mipaka inafungwa
2. wageni wote wanaoingia wanawekwa quarantine siku 14 kabla ya kuruhusiwa kuingia nchini.

Fursa hiyo ya kuudhibiti kabla ya kuingia imeshatutoka kwa maana hatukufanya hivyo na ugonjwa umeshaingia.

Kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi.

Sasa tupo katika hatua ya pili ambapo bahati mbaya zaidi, tukifanya tena makosa ya kutokuwa na umakini kamili kama pale mwanzo sasa itakuwa ndiyo basi tena. Ni vyema kuiona hii kama nafasi ya mwisho kabisa ambayo uzuri ni kuwa ingali mikononi kwetu.

Changamoto kubwa iliyopo katika hatua hii, zaidi iko kwenye kufuatilia watu walio husiana kwa namna yoyote na mgonjwa au mtu mwenye maambukizi au kushukiwa kuwa na maambukizi. Hii ni kuhusiana either directly or indirectly. Hili ndilo linalowakabili vilivyo kwa sasa:

1. Italy ambako vifo ni zaidi ya 800 kwa siku kwa jana tu.
2. Spain ambako wanaokufa ni zaidi ya 300 kwa siku kwa jana tu.
3. Iran ambako anakufa mtu kila baada ya dakika 10 kufikia jana.
4. Nk nk

Kumuweka mtu kwenye isolation kwa siku 14 tu kunatosha kabisa kumfanya afuzu kuwa hana maambukizi au anayo. Kwa kuwaweka watu kwenye isolation kwa siku 14 tu wagonjwa wote na wazima wote watafahamika.

Kwa kuwaweka watu kwenye isolation kwa siku 28, wagonjwa na waliohusiana nao wote watafahamika na tutakuwa tunaelekea kuumaliza ugonjwa huu.

Hakuna madaladala, masoko, nk "total lockdown" ni njia pekee ya kwenda kama tunataka kuumaliza huu ugonjwa.

Katika lockdown kuna uwezekano wa vifo vya njaa na vifo vya Corona. Ni muhimu kuweka utaratibu wa kuhakikisha kuwa hakuna mtu anakufa kwa njaa. Ni heri ikibidi tushindie uji ili tuwe hai lakini ugonjwa huu uondoke kuliko kula biriani wakati Corona iko mtaani huru pasipo na kudhibitiwa.

Tunaweza kujizatiti kutumia raslimali zote kuhakikisha watu wetu wote wanajikimu vizuri tu kwa chakula kwa kadri ya uwezo wetu. Hii ikiwa ni sisi kama sisi, na sisi kama taifa. Ikumbukwe, serikali pia ni sehemu ya sisi.

Miradi yote isiyo na udharura iwe ya maendeleo au vinginevyo ni wakati wake saaa wa kusimama. Raslimali zote ziende kwenye kuwawezesha wananchi kujikimu katika kipindi hiki kifupi tu.

Huwezi kuwa na shughuli za ujenzi wa nyumba wakati unauguliwa. Hii ni common sense ya kawaida kwa binadamu yoyote mwenye akili hata ya wastani tu.

Bajeti za chaguzi na shughuli zozote zisizo na lazima kwa sasa zielekezwe kwenye wananchi kujikimu kuhusiana na dharura hii.

Tutakaa lockdown muda mfupi zaidi kama hatutaendelea kupoteza muda zaidi kabla ya kuanza. Wenzetu Rwanda wameanza na wanasonga mbele.

Tunavyochelewa itatugharimu zaidi: kwanza maisha ya watu, siku za lockdown na hata raslimali pesa.

Lockdown haiepukiki ni suala la muda tu. Ni au tunakwenda sasa au baadaye wakati hali ikiwa si mbaya zaidi, and "at our own peril."

Corona ni uzembe wetu isingetufikia, na itatumaliza tusipoamka sasa - ukweli mchungu - JamiiForums

Vita dhidi ya Corona: Rwanda ni mfano wa kuigwa Afrika na wanaweza kusalimika iwapo gonjwa hili litakuwa tiishio na hapa Afrika - JamiiForums

Corona virus: Tunajifunza nini toka kwa wengine? - JamiiForums
Si mlisema hatuwezi kuishi bila mabeberu, sasa mnataka mipaka ifungwe,
 
Bila hata ya mabandiko yaliyopo mitandaoni, ni wazi kuwa haihitaji elimu yoyote kubwa kutambua ugonjwa huu ukishaingia ni suala la muda tu kwa watu wengi kama si wote kabisa, kuambukizwa kama hatua stahiki hazichukuliwi.

Haihitaji elimu kubwa pia kufahamu idadi ya watu walioambukizwa inapokuwa kubwa, kasi ya maambukizi inakuwa hata ni kubwa kuliko inavyoweza kumithilika!

Wengine wanasema kasi ya maambukizi kwa wagonjwa waliopo ni zaidi ya "exponential."

Pia haihitaji akili kubwa kufahamu kuwa ugonjwa wa namna hii unaweza kudhibitiwa kikamilifu kwa namna moja tu. Hii ni ya kuwa weka watu wote wakatulia majumbani ili kutumia muda huo kuwabaini wote wenye maambukizi kwa ajili ya hatua stahiki.

Kwa ukweli huo, itakuwa si kweli kwa serikali ya Tanzania iliyo sheheni wakiwamo na ma doctor na maprofesa kiasi like eti kuwa haya yote hawayajui.

Ukweli mchungu, kuna ukweli tunaofichwa hapa. Kwa nini ujasiri huu wa kutuweka hatarini kiasi hiki?

Labda ni muda muafaka sasa kuwa badala ya kujikita kwenye kuonyesha umuhimu wa lockdown iwe kuelekeza nguvu kwenye kutafuta sababu ya hii ficha ficha.

Ni kitu gani serikali inakisubiri kabla ya kutanganaza total lockdown?

Fumbo mfumbie mjinga mwerevu atang'amua.

Acha tuingie chimbo kusaka sababu ya hii ficha ficha ya kuhusiana na ufumbuzi wa huu ugonjwa iliyo wazi kiasi hiki.
 
Jilock mwenyew Mkuu, sisi tutaenda kutafuta ili mkono uende kinywani! Nina familia ya watu 9 afu unilockie. Hata wew nikikupa nafasi ya kuwalisha ukiwa huko unakoita total lockdown utaumbuka.

Usilete mchezo aisee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninaipenda hii:

Amesema katazo hilo la watu kutoka ndani halitawahusu watu wa idara ya majanga, polisi na watumishi wa afya ambao watakuwa wakiwazungukiwa wananchi kuwapatia mahitaji muhimu ambayo ni pamoja na chakula.

“tusipochukua hatua hii sasa wagonjwa wataendelea kuongezeka na hatua hii inaweza kuwa na athari zake kiuchumi lakini tusipoichukua sasa athari zitakuwa ni kubwa zaidi, uamzi huu utaokoa maisha ya maelfu,” amesema Ramaphosa.


Shikamoo Cyril Ramaphosa wewe kweli jembe!

Corona itakuwa historia kwako baada muda huo.

Source:

Afrika Kusini: Nchi nzima yawekwa karantini sababu ya corona - JamiiForums
 
Jilock mwenyew Mkuu, sisi tutaenda kutafuta ili mkono uende kinywani! Nina familia ya watu 9 afu unilockie. Hata wew nikikupa nafasi ya kuwalisha ukiwa huko unakoita total lockdown utaumbuka.

Usilete mchezo aisee.

Sent using Jamii Forums mobile .

Mkuu hata wakijilock 99% hausaidii. 1% inayobakia itaiambukiza bado hiyo 99%. Ndiyo maana inaitwa total lockdown. Partial au kujilock mmoja mmoja kama unavyopendekeza haimsaidii yoyote.

Hii njaa mnaiongelea wapi mkuu? Hebu ona hapa:

Amesema katazo hilo la watu kutoka ndani halitawahusu watu wa idara ya majanga, polisi na watumishi wa afya ambao watakuwa wakiwazungukiwa wananchi kuwapatia mahitaji muhimu ambayo ni pamoja na chakula.

“tusipochukua hatua hii sasa wagonjwa wataendelea kuongezeka na hatua hii inaweza kuwa na athari zake kiuchumi lakini tusipoichukua sasa athari zitakuwa ni kubwa zaidi, uamzi huu utaokoa maisha ya maelfu,” amesema Ramaphosa.
 
Mkuu hapo nafikir unaiona dhamira ya Mkuu wa nchi. Unaona kabisa kuwa serikali imeamua kuchukua jukumu. Kwa hapa Tz brother, hali ni tofauti. Inaonekana ni mapigano ya mmoja mmoja. Aliye na uwezo wa kufanya hivo anafanya hivo, asiye na uwezo huo anaenda kuchakarika Kama kawaida.
Mkuu hata wakijilock 99% hausaidii. 1% inayobakia itaiambukiza bado hiyo 99%. Ndiyo maana inaitwa total lockdown. Partial au kujilock mmoja mmoja kama unavyopendekeza haimsaidii yoyote.

Hii njaa mnaiongelea wapi mkuu? Hebu ona hapa:

Amesema katazo hilo la watu kutoka ndani halitawahusu watu wa idara ya majanga, polisi na watumishi wa afya ambao watakuwa wakiwazungukiwa wananchi kuwapatia mahitaji muhimu ambayo ni pamoja na chakula.

“tusipochukua hatua hii sasa wagonjwa wataendelea kuongezeka na hatua hii inaweza kuwa na athari zake kiuchumi lakini tusipoichukua sasa athari zitakuwa ni kubwa zaidi, uamzi huu utaokoa maisha ya maelfu,” amesema Ramaphosa.
Wazo lako ni zuri, Kama Rais wa South Africa alivonena. Lakini Kama nchi, tumejiandaa kwa hilo? Linatokea Janga mtu anakwambia yeye hajaleta Janga! Hata kwa hili tafsiri ni ile ile Kaka.

Serikali ikisema iko tayari kutuhudumia Kama sehemu ya tahadhari tuko tayari, lkn ikisema haijaleta majanga tujipambanie bado hatujapata uwezo huo.

Tutanawa mikono tutachapa kazi. Nafikir ulilisikia. Ndo hivo Kaka, mi nakuelewa lkn wenye maamzi ndo wanatufanya tuseme hivi brazaj

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hapo nafikir unaiona dhamira ya Mkuu wa nchi. Unaona kabisa kuwa serikali imeamua kuchukua jukumu. Kwa hapa Tz brother, hali ni tofauti. Inaonekana ni mapigano ya mmoja mmoja. Aliye na uwezo wa kufanya hivo anafanya hivo, asiye na uwezo huo anaenda kuchakarika Kama kawaida.Wazo lako ni zuri, Kama Rais wa South Africa alivonena. Lakini Kama nchi, tumejiandaa kwa hilo? Linatokea Janga mtu anakwambia yeye hajaleta Janga! Hata kwa hili tafsiri ni ile ile Kaka.

Serikali ikisema iko tayari kutuhudumia Kama sehemu ya tahadhari tuko tayari, lkn ikisema haijaleta majanga tujipambanie bado hatujapata uwezo huo.

Tutanawa mikono tutachapa kazi. Nafikir ulilisikia. Ndo hivo Kaka, mi nakuelewa lkn wenye maamzi ndo wanatufanya tuseme hivi brazaj

Sent using Jamii Forums mobile app

Hapana mkuu tusikate tamaa mapema hivyo. Serikali ni yetu na sisi ndiyo serikali. Serikali yetu ni sikivu hakuna mtu ataachwa kufa njaa.

Ninakuelewa hofu yako. Ondoa shaka mkuu.

Rwanda lockdown survival iko hivi:

1. Kila mtu kukaa ndani
2. Miamala ya pesa kwenye simu hakuna tozo
3. Wale wanaoishi kwa kutegemea yalipo ya siku wanagharimiwa na serikali.
4. kodi kadhaa zikiwamo za mapango zimeahirishwa.
5. Kuna vikorombwezo vingi tu ikiwamo mfuko unaochangiwa kuhakikisha hakuna anaye kufa njaa.

Hakuna atakaye kufa njaa.

Kutakuwa na ugumu lakini tutashinda.
 
Si mlisema hatuwezi kuishi bila mabeberu, sasa mnataka mipaka ifungwe,

Sina hakika unaposema "mlisema" unamaanisha kina nani?

Si haba kufahamu kuwa huu ugonjwa hauna chama.
 
Total lockdown Uganda:

1. Hakuna ndege inayoruhusiwa kuruka kutoka au kutua Uganda.
2. Hakuna basi, kubwa au dogo, bodaboda au baiskeli au mtembea kwa miguu anaruhusiwa kuingia Uganda. Mipaka yote imefungwa.
3. Mikusanyiko yote ni marufuku.

Uganda wanafanya vizuri sana katika hili.

Mgonjwa waliyenaye aliwasili na Ethiopian airlines tokea Dubai. Alithibitika airport Entebbe kwenye screening. Yuko mahali salama na wasafiri wote waliokuwa naye kwenye ndege wako quarantined passports zao zikiwa seized.

Manifest ya abiria wote walioanza safari naye iko available.

Uganda bado ni salama.

Shikamoo General Museveni.
Hiyo sentensi ya mwisho, marahaba kwa.niaba take! Wa kwetu bado anazurura kwenye mawe!
 
Hiyo sentensi ya mwisho, marahaba kwa.niaba take! Wa kwetu bado anazurura kwenye mawe!

Kazi kweli kweli. Ila cha kushangaza labda ni wote tu. Wako wapi wengine be it wa serikali, upinzani, makanisa au misikiti?

Mbona hili goma limeachiwa mitandaoni tu?
 
Senegal, Ivory coast, Sudan na Uingereza ni mataifa ya karibu zaidi kwenda total lockdown.

Sisi tumemshitakia Mungu. Acha tusubirie hukumu yake.
 
Wacha tuone baada ya siku 20 ili tujiridhishe kibaya zaidi ni hofu lkn trend ya ugonjwa sehemu nyingi duniani inatupa moyo,wagonjwa wengi wanaotangazwa ni wageni
Mkuu nasema hali ni mbaya kwa sababu hao wenzetu waliofikia 800 leo nao walianza hivi hivi vifo kidogo kidogo tu.

Kinachotokea kwetu hivi sasa si kigeni na kitapofikia haitakuwa kigeni pia. Kwa mwendo huu muelekea ni huo huo wa 800 na hata zaidi muda si mrefu unaokuja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom