Watu kusalia majumbani (total lockdown) hakuepukiki, ndiyo njia pekee ya uhakika itakayo tunusuru na kusambaa kwa Corona nchini

Watu kusalia majumbani (total lockdown) hakuepukiki, ndiyo njia pekee ya uhakika itakayo tunusuru na kusambaa kwa Corona nchini

Huko iliko anza china taarifa zake zikoje?

Sent using Jamii Forums mobile app
JK alitwambia akili ya kumbiwa changanya na ya kwako. Kuhusu corona tumeambiwa tusitishwe, tuchape kazi tu. Mh mimi nimestuka na bila kuambiwa na mtu mimi na familia yangu tuko kwenye lockdowan hadi hapo tutakaporishika kwamba ni salama kutoka kwenda kuchanganyikana na kadamnasi. Akili za kuambiwa changanya na za kwako.
 
Uoga ni kitu kibaya sana na miongoni mwa vitu rahisi kumu induce mwanadamu.

Umeshawahi kujiuliza kama takwimu za vifo vya maralia, ukimwi, TB au saratani zingekuwa zinawekwa hadharani basi hofu ya dunia ingekuwa kiasi gani?

Pia jiulize kwanini hawazitangazi?

Sahihi kabisa. Inashangaza kuona watu wanakomalia lockdown lakini wako mitaani. Kwa nini usijifungie uwe salama uwaache wanaopuuza waje waione joto ya jiwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uoga ni kitu kibaya sana na miongoni mwa vitu rahisi kumu induce mwanadamu.

Umeshawahi kujiuliza kama takwimu za vifo vya maralia, ukimwi, TB au saratani zingekuwa zinawekwa hadharani basi hofu ya dunia ingekuwa kiasi gani?

Pia jiulize kwanini hawazitangazi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi binafsi nikimbaini mtu mwoga huwa nakaa naye mbali. Woga ni hatari kuliko hatari yenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
jifungie mwenyewe, familia yangu tuko 8 kula yetu kwa siku tu shida, nijifungie tutakula mawe?
 
Uoga ni kitu kibaya sana na miongoni mwa vitu rahisi kumu induce mwanadamu.

Umeshawahi kujiuliza kama takwimu za vifo vya maralia, ukimwi, TB au saratani zingekuwa zinawekwa hadharani basi hofu ya dunia ingekuwa kiasi gani?

Pia jiulize kwanini hawazitangazi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ujasiri wa kijinga utawaua.
Mnahimizwa kuchukua tahadhari
ili mpate kuishi.
Marekani wanakufa 700 kwa siku
Hispania 700 kwa siku
Uingereza 450 kwa siku
Italia 800 kwa siku

Na kwa vigezo vyovyote hao wakubwa wana fedha kukuzidi, wana mahospitali mazuri kukuzidi, wana madaktari wengi na mabingwa kukuzidi.

Ni upumbavu tu(tofauti na ujinga, maana umeshaona) kutolielewa hilo.
 
Uoga ni kitu kibaya sana na miongoni mwa vitu rahisi kumu induce mwanadamu.

Umeshawahi kujiuliza kama takwimu za vifo vya maralia, ukimwi, TB au saratani zingekuwa zinawekwa hadharani basi hofu ya dunia ingekuwa kiasi gani?

Pia jiulize kwanini hawazitangazi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani na vyenyewe havina tiba au chanjo? na vinambukizwa kwa msongamano wa watu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gonjwa hili la Corona tulikuwa tunlipuuzia .
Sasa tumeona madhara yake dunia nzima.
Nchi kubwa , tajiri na zenye uwezo zinapigishwa magoti.
Nchi za Marekani, Uingereza, Spain ambazozilibeza ugonjwa huu sasa zinajutia.
Wamesikika wakilaumiana kwa nini hawakuchukua hatua mpema kufunga mipaka, kupunguza kujmuika kwa watu katika jamii na hata kwenda mbali zaidi kulazimisha atu wajifungie majumbani ili kuondoa kabisa mgusano au ukaribu kati ya mtu namtu.

hina kulikotokea mwanzoni kabisagonjwa lenyewe, wao walitekeleza hatua za kujikinga kama wenda wazimu.
Wengine walienda mbali uwaita makomunisti wenda wwazimu.
Hatimaye walifanikiwa na virusi vikakauka na hivyo kuokoa wananchi zaidi ya bilioni 1.4

India nayo imeafuata hatua hizo hizo ili kulinda wananchi wake 1.2 bilion.

Trump alianza kwa mzaha mzaha kuwa gonjwa litakaukalenyewe, sasa vifo USA vinaelekea 6,000 kwa ujumla na vinaendelea kwa vifo aidi ya 700 kwa siku.

Watanzania tujionee na kuchukua tahadhari, hatu za kuepusha gonjwa hili kwa sasa bado hazijakidhi tishio.
Hapa lockdown ni ngumu kila mtu atapambana na hali yake
 
Ujasiri wa kijinga utawaua.
Mnahimizwa kuchukua tahadhari
ili mpate kuishi.
Marekani wanakufa 700 kwa siku
Hispania 700 kwa siku
Uingereza 450 kwa siku
Italia 800 kwa siku

Na kwa vigezo vyovyote hao wakubwa wana fedha kukuzidi, wana mahospitali mazuri kukuzidi, wana mdktari wengi na mabingwa kukuzidi.

Ni upumbavu tu(tofauti na ujinga maana umeshaona) ktolielewa hilo.
Usiwe na haraka kusoma mkuu.!

Hakuna sehemu nimesema watu wasichukue tahadhari ila jikite kwenye hoja yangu kuwa je hayo magonjwa mengine yangekuwa yanatangazwa vifo vyake kama ilivyo corona dunia ingekuwa na hali gani?

Mfano liwepo swala la kupublish leo wamekufa watu kadhaa kwa vvu au leo malaria imeua kadhaa au kadhaa wamepata maambukizi.

Marekani vimetokea vifo 700 sawa ni vingi.! Je umewahi pata takwimu kwa siku wanakufa watu kiasi gani kutokana na njaa katika nchi za kusini mwa janga la sahara?

Je umewahi kuchukua tahadhari yoyote kuhusu njaa isije ikakupukuta na wewe?

Je hali kadhalika kifua kikuu, homa ya ini n.k?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom