Watu tisa waliozaliwa na viungo vya ziada na kuishangaza dunia

Mazee unapenda kuona dramatic refutations with bombastic reputation siyo?

Mimi nimeuliza swali dogo tu hapa.

Kuna mtu anaweza kuthibitisha huyo Mungu yupo?

Mpaka leo sijapewa jibu.
Unazungumziaje sula la hao viumbe kuzaliwa na idadi kubwa ya viungo kuliko kawaida.
 
Ana makusudio yake kufanya hivyo maana yeye ni mjuzi zaidi ndio maana kuna weupe na weusi ,wafupi na warefu.
Sijakataa kama inawezekana ana makusudio yake.

Tatizo linakuja mtu anakwambia "ana makusudio yake" halafu hawezi kuyaelezea hayo makusudio ni yapi.

Kusema hivyo si kutoa jibu, ni kukubali kwamba hujui jibu unaungaunga habari tu.

Sasa kwa nini Mungu kaweka weusi na weupe na hali hiyo ikasababisha ubaguzi wa rangi kama alikuwa na uwezo wa kuumba duniaisiyowezekana kuwa na ubaguzi wa rangi?
 
Kila kitu kinatokea kwa sababu maalumu , halafu ukae ukijua hapa duniani siyo makazi yetu ,hapa duniani ni njia tu .
 
Hao hawajaumbwa na Mungu, kama wameumbwa na Mungu basi sisi wengine katupunja.

Sasa Mungu gani anapunja wengine na kupendelea wengine?
Hapa umebifikirisha maana yule bwana mdogo George Lipert kapewa miguu mitatu kana stuli wakati sisi mamilioni tuna miguu miwili
 
Kila kitu kinatokea kwa sababu maalumu , halafu ukae ukijua hapa duniani siyo makazi yetu ,hapa duniani ni njia tu .
Kauli hizo zina matatizo mengi sana.

1. Mtu anaposema kila kitu kinatokea kwa sababu maalum, halafu hawezi kuzielezea hizo sababu maalum ni zipi, hii katika kanuni za kuchambua mambo tunaiita weakness ya "Deus ex Machina". Unamaliza mjadala kwa kumshusha Mungu wa kuchongwa asiye na maelezo ya kutosha.Yani ni kama Rambo kazungukwa na jeshi la watu 1,000, unaona kabisa hapa hawezi kutoka, halafu eti linashuka bonge la radi linaua wale maadui wote 1,000 halafu Rambo peke yake anapeta.

Hapo kama movie unaweza kupotezea ukasema hili movie tu.

Lakini kama mtu anakuelezea hii fact lazima uone unauziwa mbuzi kwenye gunia.

2. Hapa duniani si makazi yetu, tunapita tu, hii ni argument weak sana.

Kwa sababu gani? Mimi kama baba, nikikodi nyumba ufukweni New Jersey Beach huko nikae na wanangu kwa wiki tatu napunga upepo wa baharii, hapo nitakapokodi si kwangu, ni "vacation stay" tu, napita.

Lakinihilo halina maana eti kwa sababu napita tu ndio pawe pachafu, niruhusu maji yamwagike kila pahali, watu wapate magonjwa niachie tu, watu wapigane risasi wauane, niseme hapa si makazi yetu tunapita tu, wakati uwezo wa kupafanya hapo tunapopita na nyumbani tunakoenda kote kuwe pazuri kabisa.

Huyo Mungu aliyeumba ulimwengu huu akafanya mabaya yawepo tu, wakati aliweza kufanya mabaya yasiwepo, alifanya hivyo kwa sababu kuondoa mabaya kunatumia umeme na yeye aliogopa kumaliza LUKU yake?

Kwa nini hakuumba hapa pakiwa hapawezekani kufanyika mabaya na huko tunakoenda kusiwezekane kufanyika mabaya pia?

Na unaweza kuthibitisha kwamba huko mnakosema tunakwenda nyumbani kupo kweli na si hadithi tu?

Kuna mtu anaweza kuthibitisha hilo?
 
Last edited:
Hapa umebifikirisha maana yule bwana mdogo George Lipert kapewa miguu mitatu kana stuli wakati sisi mamilioni tuna miguu miwili
Kwahiyo kama unaamini Mungu yupo, hapo itabidi uulize, Mungu ana ubaguzi kuwapa wengine miguu mitatu na wengine miwili?
 
dunia ina maajabu
 
Kwahiyo kama unaamini Mungu yupo, hapo itabidi uulize, Mungu ana ubaguzi kuwapa wengine miguu mitatu na wengine miwili?
Naomba niweke wazi
Mimi sijui kama Mungu yupo au hayupo yaani sipo upande wowote
 
Naomba niweke wazi
Mimi sijui kama Mungu yupo au hayupo yaani sipo upande wowote
Umesiamama pazuri sana.

Profesa Yuval Noah Harari ameelezea vizuri sana katika vitabu vyake "Sapiens: A Brief History of Humankind" na "Homo Deus: A Brief History of Tomorrow" kuhusu dhana nzima ya kuamini kuwepo Mungu kuwa ni jitihada za watu kuziba pengo la ujuzi, kwamba pale ambapo hatujui jibu, watu tuko tayari sana kuziba pengohilo kwa kusema habari za Mungu, halafu tukija kujua, tunamsukuma huyo Mungu kwenye jambo lingine ambalo hatulijui.

Kifupi ni kwamba, watu tunakuwa wagumu sana kusema "sijui jibu, ngoja nitafute jibu".

Kwa hiyo, nikisikia mtu anasema hajui, nafurahi sana.

Kwa maana, ukisema hujui na kutafuta jibu lakweli kwa juhudi, utalipata.

Lakini ukiw ahujui na kusema unajua jibu, jibu ni "kazi ya Mungu", hutakaa upate jibu la kweli.
 
hahaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…