Watu wa aina hii huwa mnaishi nao vipi?

Watu wa aina hii huwa mnaishi nao vipi?

Watu wa aina hiyo si watu wazuri kwakweli, hujikuta wakamilifu sana yaani usikosee hata kidogo. Mimi watu wa aina hii nawaambia Kwa maneno makavu kabisa na hata kutengana naweza nikafanya sijali chochote kile, Kuna mambo mengi ya kufanya. Athari yake hiyo ni kuzaa chuki Kali Kila mnapoendelea kuonana ama kuishi pamoja na kama emotional intelligence yako si nzuri anaweza akakuambukiza mkawa mnafanana.
Ndiyo maana na mimi nimeanza kukasirika hovyo kumbe
 
Kabisa ... wanakuwaga toxic sana watu wa aina hii. Na ni ngumu wao kujikubali kwamba hiyo hali yao ni tatizo kwao na kwa wengine
Nashangaa sana huwa nikimwambia kwanini anapenda kukuza vitu vidogo anapanic
 
Yaani ukimkosea hilo kosa ataliongelea hadi siku nyingine
Nawajua vyema watu wa hivyo na nilishawakataa karibu yangu. Kila kitu kinachomtokea kimesababishwa na mtu mwingine, na wanakuaga wanafki na wachonganishi sana kuwa makini nae. Na kujifanya wapole na friendly.
Mtoe karibu yako utakuja kujuta nae siku
 
Duh! Hapa naona hatutafika mbali
Kumbe ni mwanaume? Achana na hiyo psycho itakudrain energy yako.
Rafiki siwezi weka karibu wewe umewezaje kumfanya baby kabisa? Umejichanganya hapo akikuoa utakua mtumwa wake atataka kila muda uwe unavalidate hisia zake za yeye kujisikia mwanaume
 
Nasikitika kusikia hivi, ngoja nimkaushie kwanza kwa muda
Mgeuzie kibao umfanye yey ndo aanze kukufukuzia.
  • fanya kama humjari sana. Ata akipga sim usipokee mpgie baadae na maneno yacwe meng mwambie npo busy ntakuchek na ucmtafte tena. Had akutafte yey..
  • jikipu busy to making your life yey awe kama ziada tu, make kila mtu anamapungufu. Ila ukigundua anamtu kimbia
 
Hao Kwa jina la kitaalam wanaitwa NARCISSIST ama MANIPULATOR. Ukiwa na mtu wa hivi jiandae kuwa na huzuni maisha Yako yote.
 
Wanaitwa watu wenye vichwa vigumu & wasiopenda maelewano.
Wanaongozwa na roho ya mashindano.

Kuishi nao ,kwanza waachie uhuru wao lakini usikubali kushindwa . Waonyeshe ujasiri wako.

Weka like yako hapa kama umekubali
 
Watu ambao anakosea badala ya kuomba msamaha anakutafutia na wewe kosa ili muonekane wote ni wakosefu au wewe ndiyo mwenye makosa.

Ukimfanyia kitu kidogo tu anakikuza kiwe kikubwa na kukasirika sana.

Mtu ambaye yeye akikosea anaweza hata asiombe msamaha.

Mtu ambaye anakasirishwa na vitu vidogo, huwa mnaishi vipi na watu kama

Watu ambao anakosea badala ya kuomba msamaha anakutafutia na wewe kosa ili muonekane wote ni wakosefu au wewe ndiyo mwenye makosa.

Ukimfanyia kitu kidogo tu anakikuza kiwe kikubwa na kukasirika sana.

Mtu ambaye yeye akikosea anaweza hata asiombe msamaha.

Mtu ambaye anakasirishwa na vitu vidogo, huwa mnaishi vipi na watu kama hawa nipate idea🤔
ltakuwa wewe ni jirani yangu kabisa, yaani umejuaje hizo tabia zote za mke wangu! 😂
 
Back
Top Bottom