MAONO:
Nilipopata ujumbe huo, niingia u tube kutaka kujua undani wa ujumbe huo,
Nilifungua video ya you tube UNYAKUO TV iliyokuwa ikieleza juu ya Mafuriko.
Wakati naendelea kusikiza video, uliopita USINGIZI wa ghafula, nikajikuta naona yafuatayo,
Nilijikuta nipo kwetu nilikozaliwa, nimo ndani ya nyumba nikiwa na watu kadhaa,
Cha kushangaza ni kuwa, nilikuwa ndani lakini niliweza kuona Kila kitu vizuri kilichoendelea nje na angani.
Niliona Mbinguni juu mawingu yakizunguka juu na yalitengeneza kitu kama duara mithili ya sahani flat, na sahani hiyo ilikuwa RANGI ya birauli izungukayo Kwa Kasi,
Wakati nikiona hayo juu, niliweza kuona nje upepo na wingu juu Kwa mbali,
Kasi ya sahani Ile ilizidi kuzunguka Kwa Kasi, na ghafula ukatokea mfuniko Kutoka sahani Ile uliomimina maji kiasi huku duniani na kujifunga tena.
Baada ya kuona tukio lile, nilihusi hatari inaenda tokea,
Sasa kitendo Cha kugeuka niwambie watu niliokuwa nao ndani ya nyumba tujiokoe,
Ghafula nilijikuta nikielea ndani ya maji mengi na vitu vyote vilifunikwa ikiwemo milima.
Nikastuka Kutoka maono Yale huku mapigo yakienda Kasi.
Nakushauri upatapo kumbe za kutatanisha, ingia katika maombi Mungu atasema nawe!!
Aamen