Watu wa Dar mbona miili yenu haitoi jasho, mna AC mapafuni

Watu wa Dar mbona miili yenu haitoi jasho, mna AC mapafuni

Nina siku kadhaa nikikaa tu mahala kupata safari lager, watu laZima waniulize bro vip umetoka mkoa?

Nasema hapana

Wanasema unavyotoka jasho hivi wewe ni wa mkoa nami naamua kukubali.

Jua na joto la Dar linachoma kama pasi, lakini watu miili mikavu wala hawajali wapo kawaida, nashangaa hawa watu washakuwa Sugu na joto.

Wacha jumamoto pakuche nirudi zangu nyumbani Ngara niwahi mvua nipande mahindi na maharage,
Tukutane tena baada ya mavuno mwezi January

Waacha niawaachie joto na shida zenu watu wa Dar
Ni kawaida hii ukitoka mkoa,ila hubadilika baada ya mwili ku adapt mazingira kwa kipindi kifupi tu.
 
Back
Top Bottom