Watu wa mikoani mnatujazia jiji letu

Watu wa mikoani mnatujazia jiji letu

Tupo wenyewe tumenyamaza tu watoto wa Shomvi. Mzaramo hasa hawezi kusema maneno haya, hawa ni wale wakuja tu, si unaona hata Kiswahili kinawapiga chenga mtu anaandika "lafunzi" badala ya lafudhi.

Watu wa asili wa miji mikubwa kikawaida huwa hawana ubaguzi, wanapenda wageni, huko kukosa ubaguzi ndiko kumefanya miji hiyo kufanikiwa.

Kuna siku nilikuwa New York City, naongea na OG mmoja mzee mweusi wa New York City, tulikuwa tunaongelea ubaguzi katika watu wa New York City wanaojiona wao watoto wa mjini. Akaniambia kuwa, wale watu wa New York City wenyewe wa asili miaka nenda miaka rudi huwa hawana noma na mtu, hawana ubaguzi, ila wale waliokuja miaka 10 au 20 iliyopita kutoka the Carolinas, Mississippi, Puerto Rico etc., ndio wenye kujifanya kwamba wao watu wa New York City saanaa, bado wanalimbuka na mji.

Sasa sisi ambao baba za bibi zetu ndio walijenga hayo majumba ya katikati Dar (baba yake bibi yangu kajenga kanisa la Azania Front, wamemaliza kujenga mwaka 1903, na kabla ya hapo familia ilikuwepo Dar es salaam) huwezi kutusikia tunatukana watu wa kuja.

Huwezi kumsikia Ali Tambaza akitukana watu wakuja na kwamba familia yao ya Jumbe Tambaza ndio wenyeji wa Dar. Huwezi kuwasikia kina Pambe wakitoa kashfa hizo.

Na Jumbe Tambaza kamkaribisha mpaka Baba Kabwela Mwalimu Nyerere mjini. Mwalimu Nyerere mwenyewe kasema habari hizi mara kadhaa, mpaka hotuba yake ya kustaafu karudia alivyorushwa makaburini akifanyiwa tambiko la Wazaramo na Jumbe Tambaza.

Sasa Jumbe Tambaza angesema huyu Nyerere wakuja, hatumtaki sisi watu wa mjini, tungepata uongozi uliotupatia uhuru bila ya kumwaga damu wa Mwalimu Nyerere?

Huwezi kusikia sisi kina Chanzi, kina Pazi, kina Shomvi, kina Chamgui tunawasema wakuja, labda kama utani wa jadi na watani wetu kina Rupia na Wanyamwezi, na huu tunafanya kwa kujuana wenyewe bila kuhatarisha mahusiano, kuna sanaa yake. Kwanza tumeoana sana, ukiwatukana Wasukuma utajikuta umewatukana watu wengi sana ambao ni ndugu zako, binamu zako, baba zako, wajomba zako etc.

Ukiona mtu anashikia bango kuwa yeye mtu wa Dar, na wengine ni wakuja, ujue huyo si mtu wa Dar.

Kiranga ChaNgeda Sakala Kandumbwa
Misheni Kota/Mwembetogwa/Mchafukoge/Kinyasini/ Upanga/ Oysterbay/ New York City.
Kweli kabisa...
 
Back
Top Bottom