Watu wa Mwanza hizi rangi mnapaka kwenye nyumba huwa mnawaza nini?

Huwa napenda kupita mtandao wa Jiji.co.tz kuangalia nyumba na vitu mbalimbali. Nimeshangazwa na rangi ya baadhi ya nyumba za Mwanza. Ukipita humo utaziona. Huwa mnawaza nini watu wa Mwanza?









Hawako peke yao. Mji wa St John's Newfoundland and Labrador Kanada unasifika kwa sababu kama hii ya kupaka majumba rangi kiasi cha kuwa kivutio.
 
Kwahiyo rangi ya nyumba inaakisi akili ya mwenye nyumba au. Hii ni mada nzuri ambayo inatakiwa kupata michango ya watu kwanini wanapaka rangi za nyumba zao na nini maana ya Kila rangi katika ulimwengu wa wanadamu. Je maana rangi ipo kwenye biblia au msahafu. Rangi ipo Toka nizaliwe. Je nani alizaliwa bila kukuta rangi.
 
Hawako peke yao. Mji wa St John's Newfoundland and Labrador Kanada unasifika kwa sababu kama hii ya kupaka majumba rangi kiasi cha kuwa kivutio.
Kweli, Hata kwenye Favelas huko S America kunakuwaga na hizi crazy colors. Na huvutia. Lakini hapa zinaonekana out of place kabisa. Unakutana na nyumba zina rangi tulivu, mara ghafla hii hapa ya pinki na njano. Inakuwa kama ajali hivi.
 
Mswahili ye yake wivu na choyo tu.Hujachangia chochote katika ujenzi wake halafu unampangia apake rangi gani huo ni upumbavu Kila mtu ana chaguo lake na jinsi anavopenda.Ama kama vipi Jenga ya kwako halafu pakaza rangi ya kijanja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ