Isaack Newton
JF-Expert Member
- Apr 15, 2013
- 594
- 291
Habari.!
Nina kitu kimoja nataka nijue kutoka kwa wenzetu wa sheria.
Kuna kiwanja kipo maeneo ya Tegeta ambacho ni cha baba yetu ambae alishafariki miaka 20 iliyopita, aliacha watoto watatu, wa kiume mmoja ambae ni mimi na wa kike wawili.
Kwa bahati mbaya katika watoto wa kike, mmoja alifariki pia akaacha mtoto mmoja wa kike ambae yupo kidato cha sita. Kila mtoto ana mama yake.
Sasa kiwanja tunakiuza ili kila mmoja apate mgawo wake, sasa changamoto inakuja kwamba huyu mtoto wa dada yetu aliyefariki anapinga kisiuzwe tusubiri mpaka amalize masomo miaka mitano mbele huko.
Sasa je kisheria huyu mjukuu wa baba yetu ana nguvu ya kuzuia sisi tusiuze kiwanja? Maana kiwanja twauza 30m kila mtu atapata 10m. Kisheria imekaaje hii?