Maelezo yako pamoja na comments za wadau wote nilizosoma hapo chini, ukiachana na mambo sijui ya kisheria, zipo sawa na ndizo familia mbali mbali hufuata kugawana mirathi.
Huyo mtoto wa marehemu dada yako hana haki ya urithi wa moja kwa moja hapo.
Mlivyopanga na nduguzo kwamba muuze kisha mgao wa mirathi mumkumbuke na marehrmu ndugu yenu mmefanya jambo jema linalostahili pongezi, hamna tamaa za kijinga.
Kitu ambacho sijaelelewa, huyo mtoto wa marehemu, kazaliwa peke yake kwenye tumbo la marehemu?
Kama kazaliwa na wenzake, pia mgao mtakao mgawia marehemu ndugu yenu, inatakiwa muwagawanye na wenzake sawa kwa sawa.
Zoezi la kuuza liendelee na yote mliyopanga na dada zako yatekelezeni.
Huyo mtoto wa marehemu hana haki yoyote kuwapangia ama kuingilia suala hilo.