Watu wa sheria mtusaidie hapa

Uko sahihi mkuu, sisi tunataka kutumia ubinadamu tu kwamba kila mtu apate 10m bila kujali ni mtoto wa kike au wa kiume. Huyu dogo yupo mwanza mimi na mdogo wangu tupo dar, na mteja alikua ameshapatikana ilikua ni ku deposit pesa tu kwnye account. Mpaka sasa mteja kashagaili kununua hiko kiwanja. Lakini kwa ushauri wenu ngoja niendelee kutafuta mteja mwingine ili twende kibabe kama anavyotaka yeye
 
Nahisi hiki ndo alichomaanisha, maana kama atapata hizo 10M anajua kabisa hana pa kuzipeleka, au labda wao walimuuliza sababu nyengine nje ya hiyo?
Huyu dogo ni above 18 yrs. Sasa swala la yeye pesa atazipeleka wapi ni juu yake as long as sisi tumempa mgao wa mama yake ambao ni sawa na mgao wetu. Nilijaribu kumshauri pia kama walivyoshauri wadau wengine kwamba tumfungulie fixed account ili pesa yake ibaki kwa muda anaotaka yeye.
 
Yaani mjukuu anawazidi akili? Uzeni gawaneni fedha, yeye si ana Baba yake akadai urithi huko, hicho hakimuhusu...
Ninachokitaka ni kwamba huyu dogo nae apate kwa niaba ya marehemu mama yake ambae ni dada yangu. Lakini hili swala kama walivyoshauri wadau wengine inabidi nilipeleke kibabe.
 
Ninachokitaka ni kwamba huyu dogo nae apate kwa niaba ya marehemu mama yake ambae ni dada yangu. Lakini hili swala kama walivyoshauri wadau wengine inabidi nilipeleke kibabe.
Acha uzembe, mwambie haikuhusu tunauza...
 
Fata ushauri wa wadau hapo binti ashauriwe kufungua fixed account ili asizitapanye hizo pesa
 
Fata ushauri wa wadau hapo binti ashauriwe kufungua fixed account ili asizitapanye hizo pesa
Nimemshauri sana lakini nimekuja kugundua kwamba kuna baba yetu mdogo analitaka lile eneo ndo anamshauri yule binti akatae eneo lisiuzwe. Ndo maana nkaona kabla sijalianzisha nijue kwanza kisheria imekaaje
 
Huyo kachanganyikiwa mapema sana.

.........Mwambieni kwa Babu hakuna urithi.
 
Nani alikwambia ukiwa na kiwanja unamiliki mpaka madini yaliyoko chini ya ardhi? Ukimiliki kiwanja unaishia kuwa mpangaji kwenye ardhi ambayo iko chini ya serikali kwa maana ya Rais. Kwa maana nyingine wewe kwenye ardhi unamiliki ardhi na maotea yaliyoko juu ya ardhi. Chochote kilichopo chini ya ardhi ni mali ya serikali kama huamini chimba kifusi kutoka kwenye kiwanja chako pita nacho barabarani kama haujadaiwa kibali cha machimbo
 
Yeye sio msimamizi wa mirathi ila tunachokifanya sisi ni kwamba tunataka tumgawie fungu la pesa kwa niaba ya mama yake aliyefariki ambae ni dada yetu.
Mmetumia uungwana sanaaaaaaaa uyo mtoto hakustahili kupata lolote as mama ake katangulia
 
Tunatumia busara tu lakini dada yetu hakumuorodhesha popote kuhusu urithi wake.
 
Kwa mama yake kazaliwa peke yake tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…