Watu wa sheria mtusaidie hapa

Nyie ni watu wazima ila basi ni wapuuzi 💩 yaani mtoto/mjukuu anawazuia kuuza mali yenu? Tena hata hiyo m10 msimpe mapumbavu huyo... Sasa nyie chekeni naye awatilie sumu mfe, nyuma yake mjue kuna ndug/watu wanampandikiza maneno...
 
Mungu awabariki kwa busara zenu, tumieni watu wazima kutoka kwenye ukoo ili afungue account ambayo ni fixed awekewe hela yake huko
Changamoto ni kwamba mimi ni mdogo wangu tumezaliwa kila mtu na mama ake. Sasa ndugu wote wamelalia upande wa huyu dogo ndo wanampa jeuri na yeye ndo anaishi nao huko mwanza. Na hao ndugu kwa upande wangu na mdogo wangu haziivi. Hao ndugu nao wanapataka, nilifanya juu chini nikachukua document zote za kiwanja wakakosa nguvu. Sasa kilichobaki wao nikumpa kiburi huyu dogo
 
Kwa mtizamo huu ni kama vile agenda ya kuuza ni ya kwako wewe tu.
 
🤣🤣🤣🤣🤣
 
Nyie ni watu wazima ila basi ni wapuuzi 💩 yaani mtoto/mjukuu anawazuia kuuza mali yenu? Tena hata hiyo m10 msimpe mapumbavu huyo... Sasa nyie chekeni naye awatilie sumu mfe, nyuma yake mjue kuna ndug/watu wanampandikiza maneno...
Mawazo yako ni mazuri lakini the way unavyoya deliver sio mazuri kwa lugha ya kiutuuzima
 
Kwa mtizamo huu ni kama vile agenda ya kuuza ni ya kwako wewe tu.
Hapana, agenda ya kuuza kwanza mie nilikua sina, nilitaka kujenga pale ili tupangishe kama hostel ya wanafunzi maana hiyo sehemu ipo jirani na chuo cha mzumbe cha tegeta pale. Lakini mdogo wangu akasema italeta shida mbeleni akasema bora tupauze kila mtu afe na chake.
 
Ushauri wangu msimdhulumu huyo dogo haki ya mamake hapa duniani tunapita tu tunachoenda kaburini hakizidi milioni moja endapo tutaamua kutumia gharama kubwa sana. Tukumbuke kuwa huyu ni damu ya dada yenu ambaye ni ndugu yenu ana haki kama ilivyo kwenu na watoto wenu ama wake au waume
 
Upo sahihi mkuu.!
Binafsi mimi ndo nataka hiki kiwanja kikiuzwa kwa bei yoyote ile, itagawanywa sawa kwa watu watatu. 30m kila mtu 10m, shida imekuja kwamba yeye anakataa eneo lisiuzwe na mwanzoni niliongea nae akakubali nikatuma nauli ili aje huku dar maana yupo mwanza sengerema. Cha ajabu shangazi yetu anaekaa nae akamwambia kwamba, kitu chochote nitakachomwambia akatae, na huyo shangazi kwa upande wangu na mdogo wangu tatuelewani naye. Ndo maana nikaona hili swala tulipeleke kisheria. Lengo langu sio kumdhulumu huyu dogo, atapewa haki yake kama sisi.
 
Kwa busara zilezile walizotumia kumshirikisha ... Wamfungulie akaunti yake ya fixed mpaka miaka yake hiyo anayoitaka ..atakuta imezalisha ....
 
Mtoto wa kiume unakuwa dhaifu dhaifu hivi ktk mambo ya usimamizi?

Mrithi alikuwa ni mama mtu na sio yeye. Na endapo mkaamua kumpa sehemu basi angalieni pia watoto wengine wa marehemu nao wapate. Chukua hiyo 10m igawe kwa watoto wengine wote wa marehemu maana wakijua mlimpa mmoja na wao hamjawapa inaweza ikaleta shida mbeleni.

Binti ameshajiona kasomi na mnamuogopa kwahiyo anajua kila anachosema basi ninyi mnahema.
 
Labda nikujuze kitu kimoja, ukifanya maamuzi ya pupa kwenye masuala ya mirathi inaleta shida kubwa, hilo la kwanza, la pili mimi sio mwanasheria sijui chochote kuhusu mambo ya mirathi na kwa sababu hiyo ndo maana wakawepo wanasheria. La nyongeza, binti yetu huyu elimu aliyonayo ni ndogo sana ukilinganisha na elimu yangu na ya mdogo wangu, na kuwa na elimu kubwa haimaanishi ndo kujua sheria, ndo maana unakuta mtu ni profesa lakini anakwambia ana mwanasheria wake. Nimeleta huu uzi kwa watu waliobobea kwenye masuala haya nipate moja mbili za kisheria. Maamuzi ya mihemko sio mazuri
 
Mkuu ubarikiwe Kwa kumjali mtoto wa ndugu Yako,ila kisheria huyo hahusiki, tena awe makini Kama si huruma ya ninyi wawili hapaswi kupata kitu,huyo mtoto ANa baba yake akadai urithi Kwa baba yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…