Hulka moja wapo ya watu wakimya (introverts) ni ugumu wa kujichanganya na kuzoeana na watu wapya. Hii inapelekea wengi wanajikuta hawana marafiki ukitoa watu wachache wale waliofahamiana wakati wa chuo/sekondari, biashara/kazini. Siku zinavyosonga na wanavyozidi kukukua kimaisha "cycle" ya marafiki alionao inazidi kupungua. Anabakiwa na zaidi familia tu na rafiki mmoja au wawili.
Anajikuta imefika weekend mtu anatamani kujiachia kidogo na kubadili mawazo ila akiangalia hana watu wa kujumuika nao. Akiingia bar/mgahawa anakuta majamaa wamekaa kwenye meza kwa vikundi, inabidi aidha akae meza yake mwenyewe au akae counter...lakini anakosa ile ladha ya urafiki na uhusiano walionayo wengine kwenye maisha ambapo hubadilishana mawazo na kupeana changamoto chanya za kimaisha.
Kwa upande mwingine wanakuwa ni watu wanaojitegemea (independent) kifikra na kwa mambo mengi hufanya maamuzi na kuendesha maisha bila kutegemea ushauri au mawazo ya wengine. Pia kutokana na kutokuwa na watu wengi huwa hawana zile drama/changamoto za marafiki.
Faida za marafiki ni nyingi kuliko hasara, hebu introverts toeni mbinu za kupata marafiki wapya ukubwani.