Watu wakimya (introverts) mnapataje marafiki wa kawaida ukubwani?

Watu wakimya (introverts) mnapataje marafiki wa kawaida ukubwani?

Kwa mtu yeyote yule simshauri kuwa na marafiki kabisa,watakuumiza
Kisayansi mwanadamu ni kiumbe mwenye mtindo wa maisha wa kijamii (social being) ndio maana baadhi ya adhabu za wafungwa ni kutengwa wenyewe (solitary confinement) kwasbabu huathiri sana kisaikolojia.

Naamini tunawahitaji marafiki angalau wachache wanakuwa kama "support system" yetu.
 
Natamani sana kuwa na marafiki wengi, naweza kuvutiwa na mtu tena wa jinsia yangu na nikatamani awe rafiki, Ila kuconnect inakuwa ngumu. Kwa sasa Nina marafiki wa nne tu, na tunaishi mbali,wote nilikutana nao shule. O level mmoja, A level mmoja, chuo wawili.Natamani sana kujichanganya Ila nafail, cjui ni nini hiki ata!!!
Utakuwa ni introvert hivyo utapata rafiki ikitokea fursa ya wewe kuwa karibu na mtu akuzoee ndio mnakuwa marafiki kama hao wa shule/chuo.
 
Hulka moja wapo ya watu wakimya (introverts) ni ugumu wa kujichanganya na kuzoeana na watu wapya. Hii inapelekea wengi wanajikuta hawana marafiki ukitoa watu wachache wale waliofahamiana wakati wa chuo/sekondari, biashara/kazini. Siku zinavyosonga na wanavyozidi kukukua kimaisha "cycle" ya marafiki alionao inazidi kupungua. Anabakiwa na zaidi familia tu na rafiki mmoja au wawili.

Anajikuta imefika weekend mtu anatamani kujiachia kidogo na kubadili mawazo ila akiangalia hana watu wa kujumuika nao. Akiingia bar/mgahawa anakuta majamaa wamekaa kwenye meza kwa vikundi, inabidi aidha akae meza yake mwenyewe au akae counter...lakini anakosa ile ladha ya urafiki na uhusiano walionayo wengine kwenye maisha ambapo hubadilishana mawazo na kupeana changamoto chanya za kimaisha.

Kwa upande mwingine wanakuwa ni watu wanaojitegemea (independent) kifikra na kwa mambo mengi hufanya maamuzi na kuendesha maisha bila kutegemea ushauri au mawazo ya wengine. Pia kutokana na kutokuwa na watu wengi huwa hawana zile drama/changamoto za marafiki.

Faida za marafiki ni nyingi kuliko hasara, hebu introverts toeni mbinu za kupata marafiki wapya ukubwani.
Hapo yaani umenigusa maisha yangu kabisa.mi nina marafiki watatu tu ambao mmoja ni tokea shule ya msingi mwingine sec na mmoa wa ukubwani kwenye kutoka huyo mmoja tu ndo mtu wa viwanja kwa hiyo mi ukinikuta nipo bar au viwanja vya starehe utanikuta mimi na huyo jamaa angu mmoja tu labla na washkaji wengine ambayo ni sio washkaji zangu.kwangu mimi inakuaga ngumu sana kumzoea mtu hata mwanamke
 
Kisayansi mwanadamu ni kiumbe mwenye mtindo wa maisha wa kijamii (social being) ndio maana baadhi ya adhabu za wafungwa ni kutengwa wenyewe (solitary confinement) kwasbabu huathiri sana kisaikolojia.

Naamini tunawahitaji marafiki angalau wachache wanakuwa kama "support system" yetu.
Yaan daa
 
Introvert's circle of friends is very small and tight.

Usishangae ukakuta watu kama hawa wana marafiki hawafiki watatu au watano.
hivi hii ndo wanaita introvert eeh
 
Back
Top Bottom