Watu wakimya (introverts) mnapataje marafiki wa kawaida ukubwani?

Watu wakimya (introverts) mnapataje marafiki wa kawaida ukubwani?

Ukija kwenye maisha ya madili Introvert utamuacha mbali sana,lakini inapokuja kutafuta pesa kwa kutumia akili lazima akuache mbali sana.Maisha ya madili ni lazima ushirikiane na watu wengi ndio utoke, lakini inapokuja kwenye kutumia akili hapo ni ubongo wako tu ndio utakufanya utoboe..
 
Kuna muda natamani kujichanganya na kuwa na marafiki nashindwa.

Kila nikijaribu kuingia kwenye ulimwengu wa marafiki nayokutana nayo huko ni unafiki chuki fitan nk. Naamua kujiondoa naona wanayofanya si sahihi

Unakuwa na marafiki ukishapata maendeleo kidogo kuwazidi wao tayar chuki zinaanza yalinishinda
Ukiumwa nitakutembelea ukiwa na shida nitakusaidia

Lakini mazoea siyawezi hujenga chuki
 
Hahahah! mfano mimi ni mpole halafu sio muongeaji huwa najaribu sana kujilazimisha niwe muongeaji lakini wapi imeshindikana. Nimeamua tu nikubari yaishe ingawa muda mwingine hii hali huwa inanitesa, nyumba niliyopanga nimezoena na watu wawili tu tena na wenyewe ni watu ambao tupo wote kozi moja.
Wewe ni introvert ,unakuta mzazi ana mtoto ila hajui kuwa kuna introvert anamsema mtoto mbona umezubaa sana kumbe ni asili kuwa hivyo. Kwa ujumla introvert wanakutana na changamoto mbalimnali hasa za mtazamo wa watu wengine wasioelewa kuwa hii ni asili.
 
Introvert's circle of friends is very small and tight.

Usishangae ukakuta watu kama hawa wana marafiki hawafiki watatu au watano.
Mfano Mimi sina rafiki, nimejaribu hata humu kujenga urafiki na baadhi ya watu lakini tatizo sina story zaidi ya salamu tu wanaishia kukukwepa.
 
Mi wengi wanasemaga nina kiburi na madharau maana naweza kuwa tunakutana na wewe mara kibao tu hata zaidi ya miezi kazaa na nisijui hata jina lako wala nisiulize na hata number zako nisi zisave
[emoji23] [emoji23] duu mimi huyu.Mwanamke wangu nilikua nakutana nae kwa miezi 7 ofisini namhudumia na sikuwahi kumjua jina wala kumuuliza, siku nimeumwa sikwenda job siku kama 3 akaomba no akanicheki akajitambulisha nikamjibu mbona sikujui dah [emoji28][emoji28] leo ndo demu wangu mwaka wa 2 huu.
Ananiamini sana anasemaga kuna mda alikua hadi anajiuliza huyu kaka vipi hata kuomba no kama sio mwanaume huwa anadhani ni ngumu sana wanawake kunipata sababu sipendi shobo.
 
Ila uliyemuongelea hapo sio Introvert. Huyo ni mtu mwenye tatizo mahali. Introvert hana kabisa hiyo habit yakutaka jichanganya and yeye anaona its Ok.

Ila sasa kuna hawa watu wengine wenye matatizo yakujumuika kutokana na ama uoga, viburi, majivuno, ugomvi na mauzi tu. Nao siku hizi naona wanajificha kwenye kivuli cha introvert [emoji23]
 
Kwa mtu yeyote yule simshauri kuwa na marafiki kabisa,watakuumiza

Nadhani marafiki sio tatizo tatizo ni pale unapokuwa na matarajio yoyote kwa hao marafiki yaani lazima uwe dissappointed tu!.

Mimi nina marafiki kila sehemu niliyowahi kufika/kuishi. Shule karibu kila mtu alikua rafiki yangu, chuo napo ivyo ivyo hadi nilipo leo kila mtu rafiki yangu tu si muuza duka au dada mwenye kibanda cha mboga mboga mimi ni rafiki tu. Watoto wadogo ndio hadi kero nikitokea tu mtaani wakiniona watakuja mbio mbio wananiita uncle!!uncle!! uncle!! na huwa sijivungi stori mbili tatu nao maisha yanaenda.

Sijawahi jutia kuwa na urafiki na watu. Binafsi huwa naona kama ni tabia mbaya vile kuwa mwenyewe mwenyewe.
 
Kuongea na watu naona tabu sana. Hata kuongea na simu huwa sipendi. ninaye rafiki mmoja naye yuko mbali. Ndugu zangu wenyewe huwa hawanielewi. I live in solitude, am not lonely
Uchawi huu unafundishwa au unaandaliwa jini mahaba
 
Marafiki wenyewe wa kizazi cha sasa ni vurugu tupu. Akili hazina utulivu kabisa, bora kuwa na rafiki simu janja.
Ingawa shemeji zenu wanahisi tunatafuta mademu huku. Ugomvi kila siku.
 
Sometimes kuwa na marafiki wengi ni stress tu. Naongea honestly hili. Kwenye simu yangu Nina namba zisizozidi 20 ikiwemo namba ya bi Mkubwa, mama wa Wakubwa na rafiki wachache sana. Hata nikiwa nimekwenda clubs kuenjoy.

Weekend huwa na kuwa na earphone zangu [emoji16] Naona ni njema tu kuwa na ishu zangu. Hata nikipata marafiki wawili watatu siku tukipishana tu basi na kuwa mwepesi wa kumpa nafasi atafute mtu Mwingine.
Ila kuwa mkimya kumeniepusha mengi sana [emoji16]
 
Back
Top Bottom