Usaili wa kuandika katika kada ya afya umefanyika Septemba 3, 2024 nchi nzima ili kuwapta wataalam wa afya watakaojaza nafasi 9, 483 za ajira.
Wakati usaili huu ukiwa unaendelea ilisambaa video mtandaoni ikionesha binti akiwa anasukumwa na Mwanaume akiwa ameshika karatasi kati ya watu wengine walioshika karatasi ndani ya chumba, huku Watu wanaosambaza video hiyo wakidai ni tukio lililotukia kwenye moja ya vituo vya usaili, Tazama( hapa na hapa)
Ukweli ni Upi?
JamiiCheck imefuatilia video hiyo kupitia utafutaji wa kimtandao kwa kutumia Google Reverse Image ili kufahamu uhalisia wa video hiyo inayodaiwa kuwa ni ya tukio lililotokea kwenye moja ya maeneo yaliyofanyika usaili katika kada ya afya nchini.
Tumebaini kuwa video hiyo si ya Tanzania na haihusiani na usaili katika kada ya afya, video hiyo ni ya Congo na iliwekwa mtandaoni tarehe Agosti 26, 2024 (Tazama hapa) na kuendelea kusambaa, (tazamahapa) ikionesha tukio lililotokea Congo DRC.
Ufuatiliaji wa kimtandao unaonesha tukio hili lilimuhusisha binti wa chuo chaISTA Kolwezi lundi (l’Institut Supérieur des Techniques Appliquées (ISTA)) ambaye alishambuliwa na mwalimu akiwa kwenye mtihani Mwalimu anafahamika kwa jina la Tshipamba Kabwe.
Barua ikionesha kusimamishwa kazi kwa mwalimu aliyemshambulia mwanafunzi huyo
Mkuu Hata kama jamaa katukanwa ndio amfanyie hivi huyo binti? Hii kauli Yako haina tofauti na Ile kauli ya aliyekuwa RPC wa Dodoma kwamba binti aliyebakwa na kulawitiwa alikuwa anajiuza.
Wote wana makosa Mwanzo kamtupia tusi akamziba mdomo na kumrudisha nyuma Binti kaja tena na mashambulizi mengine "Mwanaume utakua Wewe ......" Kilichofuata ni roba za mbao
Mzazi umemaliza kusomesha mwenyewe umepumua unasikia mwanao kaenda " intavyuu mana hiyo ni itavyuu" kumbe mtoto anasiginwa mashavu huko na mibaba ya usaili
Nb, hajakanyonyoa rasta kweli jamani kabinti ketu hilo lijamaa