Watu wanaosema tunamrudishia Rais mchakato wa Katiba wanachangamsha Genge

Watu wanaosema tunamrudishia Rais mchakato wa Katiba wanachangamsha Genge

Hapa hakuna suala la uelewa bali nimehoji wa Zitto.
Ili mtu kumwelewa Zitto ni lazima kwanza uwe na kiwango fulani cha uelewa!. Issue ya kumwamini mtu au kutomwamini ni very tricky, kwasababu huko ZZK anakoripoti, pia hao unao waamini nao wanaripoti pia!, the payroll is big and huge!, no one can tell for sure who is who!.
P
 
Fumbo la Imani hili
 
Kama Magufuli alituongoza kama wake zake na bado taifa liko vile vile ukiacha uhasama uliopo, ni nani atashindwa kuongoza nchi hii kwa utashi wake? Na yoyote ambaye hatafuata aliyeko madarakani atakacho, anapotezwa tu.

Hii ni presidence iliyowekwa tayari. Kubaki intact sio kwa wananchi kupenda, bali ni kwa madaraka ya Rais, penda usipende.
Usifananishe mbingu na nchi!. Zitto is a statesman, ana all signs za statemanship!.
P
 
Mjumbe wa Kikosi Kazi cha Prof. Mukandala Mhe. Zitto Kabwe yuko mubashara kipindi cha Kipima Joto ITV.

SWALI: Ripoti ya Kikosi Kazi kuhusu Demokrasia ya Vyama Vingi. Je, imejibu matarajio ya wananchi?

Karibu!

=======

Zitto Kabwe

Kwa mazingira ya Tanzania, mchakato wowote hauwezi kumkwepa Rais, wanaoongea wanachangamsha genge tu.

Tulichopendekeza kikosi kazi, Rais wa Tanzania kwa kushirikiana na Rais wa Zanzibar kuunda jopo la wataalam sababu mchakato wa Katiba ni wa kisheria.

Watu wanaosema tunamrudishia Rais mchakato wanachangamsha tu genge.

Deodatus Balile
Kuwepo kuaminiana, inavyoonekana vyama vya upinzani vimejeruhiwa, ndo maana hata Rais alisema hiyo siyo amri, sisi tumeonesha njia, ukisema Rais unamkwepa ipo siku tu utamhitaji.

Mimi ukinuiliza, mapendekezo haya ya kikosi kazi yanatoa mwanga. Mjadala wa kitaifa utarahisisha jambo hili, hata wabunge watakuwa sehemu ya mjadala wa kitaifa, Bungeni ni kupitia tu hivyo hawawezi kwenda kinyume cha mapendekezo ya mjadala wa kifaifa.

Nitoe wito, muda huo ukifika siyo muda wa kususa. Waje watoe maoni

Zitto Kabwe
Mchakato wa katiba unaongozwa na Sheria ya mabadiliko ya katiba, naona tunatiana tu hofu isiyo na msingi.

Wito wangu, hatua muhimu kuliko zote ni muswada wa mabadiliko ya katiba. Hatuwezi kujenga hoja barabarani, zinajengwa mezani. Taifa linajengwa kwa majadiliano, halijengwi kwa kukimbiana.

Deodatus Balile
Ikiwa kila mtu anakuja na kauli za iwe mvua iwe jua lazima apate anachotaka hatutafika. Tunataka mazungumzo, na yeyote anayedhani ana nia njema na nchi yetu aje na mapendekezo yanayopelea kwenye kikosi kazi, inaweza kuchukua muda.

Zitto Kabwe
Katiba yetu na sheria zetu hazikatazi mikutano ya hadhara, kikozi kazi kimesema katiba inaruhusu, ni haki ya chama cha siasa ndiyo maana tumesema iendelee, iruhusiwe kwa mujibu wa kisheria.

Mwanzoni kulikuwa na katazo, kwa waliokuwa wanalitekeleza walikuwa wanavunja sheria na sisi pia tuliokuwa tunatii agizo hili tulikuwa tunavunja sheria.

Tuliona kuna sheria zinaweza kutumika vibaya, mwaka 2019 yalifanyika mabadiliko, sehemu inayotoa haki ya vyama vya siasa kufanya mikutano kikachomekwa kipengele cha polisi kuingilia mikutano. Kikosi kazi kinataka hicho kipengele kiondolewe.

Tuligundua pia kuna kanuni za vyama vya siasa za mwaka 2019, kuna masharti ya hovyo sana. Kikosi kazi kikasema sheria hizi zifanyiwe marekebisho.
Zitto anasema KATIBA yetu na Kikosi Kazi havikatazi Mikutano ya Hadhara sasa Nani kakataza Wakati KATIBA haikatazi?
 
Kiukweli kiwango cha uelewa wa mambo makubwa kwa Watanzania wengi ni mdogo, hivyo hauko peke yako wengi wenye avarage understanding, wako kama wewe, kati ya wapinzani wote waliopo sasa, Zitto ndio the one and only capable kuwa rais wa JMT na nchi ikabaki salama!. Zitto ni Mzalendo wa kweli, Baada ya kumsikiliza leo, nimebaini haya...
P
Mr Pascal Mayalla may be, you're right...

Lakini kwangu mimi, nasema HAPANA KUBWA..

I know Zitto Kabwe to some extent...

Lakini he's not the best substitute ever compared na wale wengine walio nje ya serikali a.k.a wapinzani...

Let's be honest ingalau kwa dakika moja kwa kujibu swali hili...

Hebu ndugu Pascal Mayalla toa mapenzi yako binafsi (personal interests) kwa yeyote kati ya hawa wapinzani wawili, yaani Zito Kabwe na Tundu Lissu...

Kisha mchuke Zito Kabwe upande huu na kisha mchukue Tundu Lissu mweke upande ule. Then take a deep breath. Think very carefully...

Kisha waambie watu nani aweza kufaa kuwa kiongozi mkuu wa nchi hii iwapo tungepaswa kufanya maamuzi sasa au jana...?

I know exactly that both of them are human beings...

And therefore both of them have strengths and weaknesses ktk eneo fulani...

But, remember that, from the strengths and weaknesses, we get the BEST....

Kwa hiyo, hebu watazame hao watu wawili, kwa kutumia vigezo hivi tu vichache, then make your choice...

✓ Uaminifu na ukweli...
✓ Upendo kwa wengine/asiye na ubinafsi..
✓ Ujasiri wa kukabiliana na changamoto ..
✓ Ufahamu na uelewa mambo ya kisiasa, kisheria, diplomasia ya kimataifa na kiuchumi..
✓ Patriotism (aliye tayari kufa kutetea ukweli juu ya taifa lake)
✓Ushirikishaji ktk kufanya maamuzi nk nk..

Sasa tumia vigezo hivyo tu kufanya maamuzi yako ya nani ni bora zaidi ya mwenzake...

Nakuhakikishia kuwa, kama ukiamua kuitendea haki nafsi yako, utapata jibu kuwa Tundu Lissu is far more better than Zito Kabwe...

Don't think that I hate Zito Kabwe. No, I don't...
 
Kikosi kazi chini ya wachumia tumbo kina zitto! Siasa biashara nchi bado inasafari ndefu sana!
 
Nami nimebahatika kuwasikiliza vizuri,ni wajuvi wa kutetea hoja zao vizuri.

Katika mazungumzo yao,ni kama wanasisitiza mambo karibia yote Nchi hii yaongozwe kwa sheria,kwa lengo la kutoruhusu utashi binafsi wa kiongozi.

Wanachosahau hata wao kikosi chao,kiliundwa kwa utashi binasfi wa mtu mmoja tu.hakijaundwa kwa sheria yoyote.kwa hiyo mtu akisema kilikuwa kikosi kisichokuwa chini ya sheria yoyote,na kula pesa tu hatakosea.
Yani aliyekiunda kile kikosi akiamua yale maoni ya kikosi yakatupwe jalalani,hatakuwa amevunja sheria yoyote.
Nadhani ndiyo sababu aliwaambia mapendekezo yao siyo amri
 
Haya ni baadhi ya mapendekezo ya Kikosi Kazi.

1. Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi wateuliwe na Raisi [ mwenyekiti wa Ccm.]

2. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uendeshwe na kusimamiwa na Tamisemi / Ofisi ya Raisi [ mwenyekiti wa Ccm ].

3. Watumishi wa umma [ makada wa Ccm ] waendelee kusimamia Uchaguzi wa Raisi, Madiwani, na Wabunge.

Kwa mapendekezo hayo matatu utaona kabisa kwamba Kikosi Kazi ni ujanja-ujanja na kupotezeana muda.
 
Kikosi cha kula ubwabwa tu hicho n aliyekiweka anaweza kukipiga chini tu
 
Haya ni baadhi ya mapendekezo ya Kikosi Kazi.

1. Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi wateuliwe na Raisi [ mwenyekiti wa Ccm.]

2. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uendeshwe na kusimamiwa na Tamisemi / Ofisi ya Raisi [ mwenyekiti wa Ccm ].

3. Watumishi wa umma [ makada wa Ccm ] waendelee kusimamia Uchaguzi wa Raisi, Madiwani, na Wabunge.

Kwa mapendekezo hayo matatu utaona kabisa kwamba Kikosi Kazi ni ujanja-ujanja na kupotezeana muda.
Huu ndio utumbo waliopendekeza?🤣🤣
 
Back
Top Bottom