Watu wanaosema tunamrudishia Rais mchakato wa Katiba wanachangamsha Genge

Watu wanaosema tunamrudishia Rais mchakato wa Katiba wanachangamsha Genge

Huyo Kitila aliondoka huko ACT, je Zito atafungaje wakati wa kumletea mipira kaondoka? Mahaba niue nayo ni tatizo la aina yake.
Mkuu Tindo , kweli kuna watu wanawakubali watu fulani kwa mahaba niue, bila sababu zozote!, na kuna watu tunawakubali watu for reasons and merrits.
Watu wa mahaba nieu kazi yao ni kumsifia tuu huyo wanae mpenda na kamwe hawawezi kumkosoa!. Sisi wakubali watu objectively, tutamsifu mtu panapostahili sifa na akiboronga, tunamkosoa. Mimi pamoja na kumkubali sana Zitto, anapoboronga, mara kibao ninamkosoa Urais wa ZZK 2015: Ngoma Ikivuma Sana...!.
Na Zitto, Shika lako, ya wengine waachie wenyewe! Epuka kumtaja Lowassa kwa ubaya!
Na Kama tuhuma hii ni kweli, then this is The End of Zitto. Karma Ndio Itamaliza Kila Kitu!
Na Zitto Zuberi Kabwe ni Mchochezi. Akamatwe, Ashitakiwe kwa Uchochezi, adai Rais Magufuli ni...
Na Zitto Kabwe na wapinzani wote, kwanini mnapiga tu kelele kuhusu udikteta bila kuchukua hatua zozote? Isn't it a nuisance? Je, 2020 ni CCM pekee?

Huu ni uthibitisho support yangu kwa Zitto, sio ya mahaba niue ni bonafide genuine!.

P
 
Paskali usipooze mpira tell CHADEMA the bitter truth that they are not only empty shell but also disgrace to this Nation!
They no longer command any respect due to their childish politics!
Politics is the game of give and take lakini CHADEMA wana practice primitive politics za kuzira na kukumbia majadiliano!
Hili tumewaambia sana humu, they never learn!. CHADEMA Hamkujipanga, hamjajipanga, hamjipangi na hamtajipanga!-2015 ni CCM tena! na kuhusu hii tabia yao ya kususa susa, pia tuliisha wapaka humu Swali kuhusu tabia ya kususa, kugomea au kuzira: Je, si tabia za kike, si utoto?
P
 
Mkuu Tindo , kweli kuna watu wanawakubali watu fulani kwa mahaba niue, bila sababu zozote!, na kuna watu tunawakubali watu for reasons and merrits.
Watu wa mahaba nieu kazi yao ni kumsifia tuu huyo wanae mpenda na kamwe hawawezi kumkosoa!. Sisi wakubali watu objectively, tutamsifu mtu panapostahili sifa na akiboronga, tunamkosoa. Mimi pamoja na kumkubali sana Zitto, anapoboronga, mara kibao ninamkosoa Urais wa ZZK 2015: Ngoma Ikivuma Sana...!.
Na Zitto, Shika lako, ya wengine waachie wenyewe! Epuka kumtaja Lowassa kwa ubaya!
Na Kama tuhuma hii ni kweli, then this is The End of Zitto. Karma Ndio Itamaliza Kila Kitu!
Na Zitto Zuberi Kabwe ni Mchochezi. Akamatwe, Ashitakiwe kwa Uchochezi, adai Rais Magufuli ni...
Na Zitto Kabwe na wapinzani wote, kwanini mnapiga tu kelele kuhusu udikteta bila kuchukua hatua zozote? Isn't it a nuisance? Je, 2020 ni CCM pekee?

Huu ni uthibitisho support yangu kwa Zitto, sio ya mahaba niue ni bonafide genuine!.

P

Sina tatizo na mahaba yako kwa Zito iwe for reasons or without. Je huo ushauri wao alifuata, au umehamasika sasa ili ionekane na ww umemkubali kwa hili analosimamia sasa?
 
Naomba nikuulize swali moja tu Pascal Mayalla...je unaamini ndani moyo wako kuwa mimi nina uhusiano wowote na Chadema? Toka nijiunge na JF niliwataka wana JF wajue bila kuficha kuwa mimi si mwana CCM na siwezi kuiunga mkono CCM kwa sababu imepoteza dira.

Lakini hakuna hata mara moja nilipojitambulisha kama mwana Chadema. Badala yake nilikiri bila kificho kuwa chama chochote ambacho kitaonesha nia na ujasiri wa kupambana na CCM nitakiunga mkono na nimefanya hivyo toka mfumo wa vyama vingi uruhusiwe mwaka 1992.

Kiukweli Chadema siwajui na sidhani kama uongozi wa Chadema una habari na uwepo wangu popote pale. Katika maisha yangu kitu ambacho nakichukia kuliko yote ni unafiki, unafiki kwangu mwiko. Kama ningeamua kuwa mwana Chadema nisingesita kujitambulisha hivyo.

Unaponijibu kwa kejeli za kijinga za kiCCM, sitasita, narudia, sitasita kukuweka sawa. HIvyo ondoa wasi wasi, unaongea na Mtanzania mwenye uchungu na hii nchi ilipo na inapoelekea full stop. Pamoja na kung'ang'ania madaraka, CCM haina uwezo wala sifa za kulikwanua taifa hili.

Katika msingi huo Chama chochote kile kinacholala kitanda kimoja na CCM kwangu kimekosa sifa. CCM ni chuo cha uharibifu na ninapowakumbuka wasomi waliotumbukia katika shimo la CCM na mara ghafla pamoja na kuwa na macho hawaoni, kuwa na masikio hawasikii na ubinadamu kuota mbawa.

Adui mkubwa wa taifa hili ni CCM!
 
Mkuu Fumadilu Kalimanzila, hiki unachowaambia ni ukweli mchungu. Chadema hawezi kukubali walifanya makosa sana kupoteza zile think tanks zake mbili, Zitto na Kitila.

Kuna baadhi ya maeneo, mafanikio yanapatikana kwa a good team work, ili mfungaji bora afunge mabao, anahitaji watu wa kumpelekea mipira.

Chadema bado ina few good brains akiwemo JJMyika, Heche, Mdee, Bulaya etc, ila haina wachezaji wa links nao is , hivyo Chadema kuonekana kama wote waliobaki, ni empty shells, wakati they are not!.
P
Kitila alifanya nini akiwa Katibu mkuu na baadae Waziri?
 
Sina tatizo na mahaba yako kwa Zito iwe for reasons or without. Je huo ushauri wao alifuata,
Ushauri hakufuata na huu ni moja ya udhaifu mkubwa wa ZZK nilio uzungumza hapa Zitto ni Mzalendo wa kweli, Baada ya kumsikiliza leo, nimebaini haya...
au umehamasika sasa ili ionekane na ww umemkubali kwa hili analosimamia sasa?
Mkuu Tindo, Zitto na Mdee tumeanza nao kitambo tangu enzi za UD kabla hajawa recruited into Chadema, Zitto is a born leader and not a made leader. Hivyo sikuanza nae jana!.
P
 
Kitila alifanya nini akiwa Katibu mkuu na baadae Waziri?
Prof. Kitila ni think tank, ma think tanks ni watu wenye good brain hivyo ni ma strategist wa kupanga strategies na mipango mkakati, hivyo wao kazi yao ni policy fomulation, walihitaji good implementors behind them, kama alivyo Nyerere na Azimio la Arusha na siasa ya Ujamaa na Kujitegemea!, tulikwama kwenye utekelezaji!.
Tanzania tuna tatizo za watekelezaji!.

Sasa mbona alishindwa kumfanya Zitto Kabwe awe Mwenyekiti wa Chadema na kuishia kufurushwa chamani?
 
Sasa mbona alishindwa kumfanya Zitto Kabwe awe Mwenyekiti wa Chadema na kuishia kufurushwa chamani?
Huyu ndie mwandishi wa ule waraka wa mabadiliko, tatizo kule Chadema hawana watu wa kiwango hicho cha uelewa wa waraka ule, waraka ule ni waraka wa mabadiliko kuunda kitu kinachoitwa a winning coalition, Chadema wangezingatia hoja za waraka ule, saa hizi, siku nyingi, Chadema ingekuwa imeisha ingia ikulu!.

Kama ni hivyo, ilikuwaje Zito na Kitila walipohamia ACT hawakuingia ikulu? Au uwezo wa kuchukua ikulu ilikuwa lazima wawepo ndani ya CDM tu?
 
..kitendo cha Chadema kutokushiriki kumekifanya kikosi kazi kupuuzwa na kukosa uhalali.

..wengi wanaojitokeza kuzungumza badala ya kutetea mapendekezo ya kikosi kazi wanailaumu na kuilalamikia Chadema kwa kutokushiriki.
 
Kama ni hivyo, ilikuwaje Zito na Kitila walipohamia ACT hawakuingia ikulu? Au uwezo wa kuchukua ikulu ilikuwa lazima wawepo ndani ya CDM tu?
ACT mpaka sasa ni the under dogs, uchaguzi wa 2025 ndio wanakwenda kuwa Chama kikuu cha Upinzani kwa kuanza na SMZ, kisha 2030 huku bara. Hapo kati yule "the game changer" alitibua kumchukua yule think tank wao, 2025 atapigwa chini kule kutosimamishwa pale, atarejea nyumbani with a full force kulitwaa tena jimbo lake na 2030 Ikulu. Kiukweli, Kama Sio Nguvu ya Soda, Then ACT ni Tishio. Hawa ni The Underdogs, Huwezi Kuwapuuza
P
 
..sielewi kwanini Zitto na wenzake ktk kikosi kazi wameshindwa kupendekeza zuio la mikutano ya hadhara liondolewe sasa hivi bila kuchelewa.
 
Mjumbe wa Kikosi Kazi cha Prof. Mukandala Mhe. Zitto Kabwe yuko mubashara kipindi cha Kipima Joto ITV.

SWALI: Ripoti ya Kikosi Kazi kuhusu Demokrasia ya Vyama Vingi. Je, imejibu matarajio ya wananchi?

Karibu!

=======

Zitto Kabwe

Kwa mazingira ya Tanzania, mchakato wowote hauwezi kumkwepa Rais, wanaoongea wanachangamsha genge tu.

Tulichopendekeza kikosi kazi, Rais wa Tanzania kwa kushirikiana na Rais wa Zanzibar kuunda jopo la wataalam sababu mchakato wa Katiba ni wa kisheria.

Watu wanaosema tunamrudishia Rais mchakato wanachangamsha tu genge.

Deodatus Balile
Kuwepo kuaminiana, inavyoonekana vyama vya upinzani vimejeruhiwa, ndo maana hata Rais alisema hiyo siyo amri, sisi tumeonesha njia, ukisema Rais unamkwepa ipo siku tu utamhitaji.

Mimi ukinuiliza, mapendekezo haya ya kikosi kazi yanatoa mwanga. Mjadala wa kitaifa utarahisisha jambo hili, hata wabunge watakuwa sehemu ya mjadala wa kitaifa, Bungeni ni kupitia tu hivyo hawawezi kwenda kinyume cha mapendekezo ya mjadala wa kifaifa.

Nitoe wito, muda huo ukifika siyo muda wa kususa. Waje watoe maoni

Zitto Kabwe
Mchakato wa katiba unaongozwa na Sheria ya mabadiliko ya katiba, naona tunatiana tu hofu isiyo na msingi.

Wito wangu, hatua muhimu kuliko zote ni muswada wa mabadiliko ya katiba. Hatuwezi kujenga hoja barabarani, zinajengwa mezani. Taifa linajengwa kwa majadiliano, halijengwi kwa kukimbiana.

Deodatus Balile
Ikiwa kila mtu anakuja na kauli za iwe mvua iwe jua lazima apate anachotaka hatutafika. Tunataka mazungumzo, na yeyote anayedhani ana nia njema na nchi yetu aje na mapendekezo yanayopelea kwenye kikosi kazi, inaweza kuchukua muda.

Zitto Kabwe
Katiba yetu na sheria zetu hazikatazi mikutano ya hadhara, kikozi kazi kimesema katiba inaruhusu, ni haki ya chama cha siasa ndiyo maana tumesema iendelee, iruhusiwe kwa mujibu wa kisheria.

Mwanzoni kulikuwa na katazo, kwa waliokuwa wanalitekeleza walikuwa wanavunja sheria na sisi pia tuliokuwa tunatii agizo hili tulikuwa tunavunja sheria.

Tuliona kuna sheria zinaweza kutumika vibaya, mwaka 2019 yalifanyika mabadiliko, sehemu inayotoa haki ya vyama vya siasa kufanya mikutano kikachomekwa kipengele cha polisi kuingilia mikutano. Kikosi kazi kinataka hicho kipengele kiondolewe.

Tuligundua pia kuna kanuni za vyama vya siasa za mwaka 2019, kuna masharti ya hovyo sana. Kikosi kazi kikasema sheria hizi zifanyiwe marekebisho.

Rais anaweza kuamka na kuchagua makamishna wa tume ya uchaguzi, kikosi kazi kimesema hapana.

Matokeo ya Rais yahojiwe kwenye mahakama ya juu pindi itakapoanzishwa.

Uchaguzi uliopita baadhi ya wagombea walikatwa kwa sababu za kipuuzipuuzi tu, mapendekezo ya kikosi kazi ni kuwa watu wakienguliwa pasipo kufuata taratibu wahusika wawajibishwe kisheria.
Hivi wapi ukiona CCM ikijenga hoja mezani! Ikiwekwanwakigeuka wanabadili angani.

Zitto kama kweli uko na udhati wa kuleta mabadiliko ungekutana na viongozi wenzio wa upinzani mkajengea hoja na sio unajikita kulamba asali Inakuja na kuingia mkono wabomoa KATIBA.
 
Kikosi kazi kimekwepa kipengele wasimamizi wa Uchaguzi wasiwe makada wa CCM. ZITO hapo unapiga porojo tu tume ya Warioba, Tue ya Nyalai, tume ya Kisanga zilishamaliza kazi.
 
ACT mpaka sasa ni the under dogs, uchaguzi wa 2025 ndio wanakwenda kuwa Chama kikuu cha Upinzani kwa kuanza na SMZ, kisha 2030 huku bara. Hapo kati yule "the game changer" alitibua kumchukua yule think tank wao, 2025 atapigwa chini kule kutosimamishwa pale, atarejea nyumbani with a full force kulitwaa tena jimbo lake na 2030 Ikulu. Kiukweli, Kama Sio Nguvu ya Soda, Then ACT ni Tishio. Hawa ni The Underdogs, Huwezi Kuwapuuza
P

ACT Zanzibar ina nguvu, sio kwa sababu ya sera, bali ni historia ya kisiwa hicho, kuwa Wapemba na CCM ni mwiko. Zito aliokota dodo chini ya mwembe baada ya ugomvi wa CUF kutokana na kibaraka wa CCM Lipumba kuivuruga. Maalim Seif akahamia ACT. Na kwakuwa Maalim Seif alikuwa mtume wa Wapemba basi wote wakahamia ACT.

Hakuna cha uthink tank wa kina Kitila wala nini. Kwa huku bara bado ACT inachezea ngome za iliyokuwa CUF hasa ukanda wa pwani kwenye waislamu wengi. Na huko hawapati watu kwa ajili ya sera, bali masalia ya wana CUF wanauliza tu chama cha Maalim Seif ni kipi basi wanaingia humo. Na wakiona Zito ni muislamu hawaulizi tena.

Ikitokea uchaguzi wa halali CCM haina uwezo wa kupata 2/3 ya kuamua watakacho bungeni. Na CDM itafuata. Na CCM wakiona hivyo watavuruga tena uchaguzi maana sio rahisi wao kuelewana na CDM. ACT itapata viti vingi Pemba na hata urais huko kama CCM itakubali kuwa zama zake zimeisha, lakini wabunge wa Zanzibar huku kwenye bunge la muungano hawana madhara.
 
ACT Zanzibar ina nguvu, sio kwa sababu ya sera, bali ni historia ya kisiwa hicho, kuwa Wapemba na CCM ni mwiko. Zito aliokota dodo chini ya mwembe baada ya ugomvi wa CUF kutokana na kibaraka wa CCM Lipumba kuivuruga. Maalim Seif akahamia ACT. Na kwakuwa Maalim Seif alikuwa mtume wa Wapemba basi wote wakahamia ACT.

Hakuna cha uthink tank wa kina Kitila wala nini. Kwa huku bara bado ACT inachezea ngome za iliyokuwa CUF hasa ukanda wa pwani kwenye waislamu wengi. Na huko hawapati watu kwa ajili ya sera, bali masalia ya wana CUF wanauliza tu chama cha Maalim Seif ni kipi basi wanaingia humo. Na wakiona Zito ni muislamu hawaulizi tena.

Ikitokea uchaguzi wa halali CCM haina uwezo wa kupata 2/3 ya kuamua watakacho bungeni. Na CDM itafuata. Na CCM wakiona hivyo watavuruga tena uchaguzi maana sio rahisi wao kuelewana na CDM.
Good analysis
ACT itapata viti vingi Pemba na hata urais huko kama CCM itakubali kuwa zama zake zimeisha,
ACT inaweza kupata urais wa Zanzibar kwasababu Mama ni muwaza haki, msema haki na mtenda haki, hivyo ACT ikishinda kwa haki, watapewa. Kumuepushia Dr. aibu ya kushindwa, 2025 hili linaweza kutokea Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke
Humo nimesema
Wanabodi

Hili la Mwinyi kuja huku, sio la sauti, hili ni langu tuu, maana usikute pia ni mpango ya YEYE, kumfanya huyu jamaa Dr. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii maana
wakati nikiandika hayo, Dr. Shein alikuwa hajui, hivyo hata saa hizi ninapoandika hapa, usikute huyu jamaa wala hajajijua kuwa yeye ndiye anapaswa aje awe rais ajaye wa Zanzibar!. Hii nibkufuatia dhulma kubwa iliyokuwa ikifanyika Zanzibar kwa miaka na miaka, Elections 2015 - Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda lakini sasa kwavile Samia ni mpenda haki, msema haki na mtenda haki, for the first time in Zanzibar tangu baada ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya January 12, 1964, uchaguzi wa 2025 unaweza kuwatendea haki!.

P.
P
 
Good analysis

ACT inaweza kupata urais wa Zanzibar kwasababu Mama ni muwaza haki, msema haki na mtenda haki, hivyo ACT ikishinda kwa haki, watapewa. Kumuepushia Dr. aibu ya kushindwa, 2025 hili linaweza kutokea Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke
Humo nimesema

P

Nani mpenda haki? Hakuna uwezekano wa yeye kutenda haki akiwa ndani ya CCM. Maana kitendo cha yeye kutenda haki ni kuleta tatizo kwa chama chake. Na sitegemei kama wanaccm wenzake hasa wa huku bara watamkubalia.
 
Back
Top Bottom