Watu wanasema mimi ni nani? Swali alilouliza Yesu linalofungua ubongo wa mwanadamu kujitambua

Watu wanasema mimi ni nani? Swali alilouliza Yesu linalofungua ubongo wa mwanadamu kujitambua

Unaweza kuthibitisha hizo Assumptions potofu..?

1. Una assumption kwamba kuna Mungu - Mungu huyu unayemsema habari zake zina contradictions nyingi sana kiasikwamba kuamini yupoinabidi ujitoe akili, chiefly being the problemof evil

2. Una assumption kwamba Biblia ina majibu - Biblia ina contradictions nyingi sana kiasikwamba kuiamini inabidi ujitoe akili, ukiwasoma wataalam wa Biblia kama Professor James L Kugel, mtaalam wa Biblia na masomoya Kiyahudi aliyefundisha mpaka Harvard, utaona Bibliani maandiko ya watu tu, wanaosemwa wameandikahawajaandika, ime badilishwa mara nyingi sana, habari nzimaza kuwapokwaMungu na kuumbwa kwa Adam niza kutungwa tu.

3. Una assumption kwamba purpose nikitu cha lazima - Ukisoma Quantum physics utaona kwamba at the core of this universe, probabilities rule, not purpose.
 
Mtu Kama wewe hutakiwi Kukosea Kitu Basic Kama Hiki.. Anaitwa Sir Isaac Newton bila kutaja Sir utakuwa umemtaja mtu Mwingine..
Bahati nzuri umeelewa nilikua namlenga nani...
 
sitaki kuwa upande wowote hapa ila nimejaribu kumuelewa Da'Vinci na ametuelimisha kulingana na uelewa wake na References zake,

na wewe pia unaweza ukawa na mawazo yako (assumptions) ambazo either zikakubaliana hizi au zikapingana...muhimu ni tuwekee hapa tuzidi kufungua fahamu zetu,

2. Biblia inaweza ikawa na majibu na isiwe na majibu inategemea na wewe msomaji.

3. Purpose inaweza isiwe kitu cha lazima kwa mtazamo wako lkn inaweza ikawa ni muhimu pia....sitaki kuamini kama kuna mtu anaweza kulala asiwe na hata jambo moja analonia kulifanya kesho yake au siku za usoni baadae!


mimi ni mtazamo wangu huu....nipo hapa kukosolewa na kujifunza pia.
Biblia ni kama methali za Kiswahili, nafikiri na sisi tungeendeleza methali zetu, hadithi zetu na historia zetu, tungeweza kuwa na kitu kama Bibliayetu.

Kwa nininasema Biblia ni kama methali za Kiswahili? Biblia ina mambo mengi sana, ila haina majibu, majibu unayo mwenyewe na utachagua Biblia ikuambie nini wewe mwenyewe.

Biblia ni kama methali za Kiswahili, useme unatakakujua, kipi ni kizuri, kwenda haraka, au kwenda polepole, kwa kuangalia methali za Kiswahili.

Ukitaka jibu la swali hili, utahamanika.

Kwa sababu, utakutana na methali moja inakwambia "haraka harakahaina baraka" halafu ukiangalia methali hizo hizo utakutana na methali nyingine inakuambia "Ngoja ngoja yaumiza matumbo".

Utaanza kujiuliza, sasa nifuate ipi hapa? Niende haraka kwa sababu ngoja ngoja itaumiza matumbo? Au niende polepole kwa sababu haraka haraka haina baraka?

Kumbe mambo yanategemea na muktadha, na ukiujua muktadha, unaweza kuchagua methali nzuri ya kutumia pale ulipochelewa kwenda kazini na speed limit inakuruhusu kuongeza mwendo, au pale ambapo hujachelewa kazini na ushapita speed limit.

Ukisema "purpose inaweza kuwa kitu muhimu pia" hilo halina mjadala. Chochote kinaweza kuwa kitu muhimu kutegemea na muktadha. Sijaongelea kinachoweza kuwa muhimu kulingana na muktadha, naongelea kilicho cha lazima katika muktadha wowote.

Unaweza kukuta jani limepeperushwa na upepo kutoka mtini likafika mlangoni mwako kwa ajali ya upepo tu, ukaanza kujiuliza "what is the meaning and purpose of this leaf being here?".

Unaweza kupata kichaa kutafuta purpose katika mambo ya chance tu ambayo hayana purpose wala direction.
 
Hilo swali la mimi ni nani..? huwa najiuliza ninapokuwa na mgogoro(mawazo mawili kinzani)mimi binafsi!,hivyo naamua kwa kuangalia sifa zangu,kanuni zangu au nitakavyo ikiwamo faida na hasara za kitu husika and then naamua kuwa nani kati ya hiyo mitazamo miwili inayokita kichwani.
 
Back
Top Bottom