sitaki kuwa upande wowote hapa ila nimejaribu kumuelewa
Da'Vinci na ametuelimisha kulingana na uelewa wake na References zake,
na wewe pia unaweza ukawa na mawazo yako (assumptions) ambazo either zikakubaliana hizi au zikapingana...muhimu ni tuwekee hapa tuzidi kufungua fahamu zetu,
2. Biblia inaweza ikawa na majibu na isiwe na majibu inategemea na wewe msomaji.
3. Purpose inaweza isiwe kitu cha lazima kwa mtazamo wako lkn inaweza ikawa ni muhimu pia....sitaki kuamini kama kuna mtu anaweza kulala asiwe na hata jambo moja analonia kulifanya kesho yake au siku za usoni baadae!
mimi ni mtazamo wangu huu....nipo hapa kukosolewa na kujifunza pia.
Biblia ni kama methali za Kiswahili, nafikiri na sisi tungeendeleza methali zetu, hadithi zetu na historia zetu, tungeweza kuwa na kitu kama Bibliayetu.
Kwa nininasema Biblia ni kama methali za Kiswahili? Biblia ina mambo mengi sana, ila haina majibu, majibu unayo mwenyewe na utachagua Biblia ikuambie nini wewe mwenyewe.
Biblia ni kama methali za Kiswahili, useme unatakakujua, kipi ni kizuri, kwenda haraka, au kwenda polepole, kwa kuangalia methali za Kiswahili.
Ukitaka jibu la swali hili, utahamanika.
Kwa sababu, utakutana na methali moja inakwambia "haraka harakahaina baraka" halafu ukiangalia methali hizo hizo utakutana na methali nyingine inakuambia "Ngoja ngoja yaumiza matumbo".
Utaanza kujiuliza, sasa nifuate ipi hapa? Niende haraka kwa sababu ngoja ngoja itaumiza matumbo? Au niende polepole kwa sababu haraka haraka haina baraka?
Kumbe mambo yanategemea na muktadha, na ukiujua muktadha, unaweza kuchagua methali nzuri ya kutumia pale ulipochelewa kwenda kazini na speed limit inakuruhusu kuongeza mwendo, au pale ambapo hujachelewa kazini na ushapita speed limit.
Ukisema "purpose inaweza kuwa kitu muhimu pia" hilo halina mjadala. Chochote kinaweza kuwa kitu muhimu kutegemea na muktadha. Sijaongelea kinachoweza kuwa muhimu kulingana na muktadha, naongelea kilicho cha lazima katika muktadha wowote.
Unaweza kukuta jani limepeperushwa na upepo kutoka mtini likafika mlangoni mwako kwa ajali ya upepo tu, ukaanza kujiuliza "what is the meaning and purpose of this leaf being here?".
Unaweza kupata kichaa kutafuta purpose katika mambo ya chance tu ambayo hayana purpose wala direction.