ambacho huwa najiuliza, kwanini wanadamu wampiganie mtume wao, si ajipiganie yeye mwenyewe kama ana nguvu? kwanini wanadamu wampiganie mungu, si ajipiganie yeye mwenyewe kama ana nguvu? kama mungu au mtume anapiganiwa na wanadamu basi mungu huyo au mtume huyo hana nguvu wala uwezo wowote kwasababu anategemea msaada toka kwa wanadamu. hiyo ni fikirishi ya kawaida tu, au mimi sielewi mnieleweshe?
utaendaje kumwomba au kumwabudu Mungu ambaye wewe ndiye unampigania? unamtetea? kama anatetewa na mimi basi huyo anatakiwa aniabudu mimi sio mimi nimwabudu yeye. Mungu pekee asiyepiganiwa wala hahitaji msaada wa wanadamu ni "MUNGU WA IBRAHIMU ISAKA NA YAKOBO" Mungu wa Israel na huwezi mwona bila kupitia kwa Yesu Kristo tu. uamini usiamini ukweli ndio huo.
sisemi hivi ili kukashifu dini, nasema hivi ili kuwaambia wanadamu waache kutunga sheria za kumtetea mungu wao, kufanya hivyo ni kumshusha hadhi. pia watu waache tabia za kumpigania mungu wao ati kwa jihad n.k, kufanya hivyo wanamchafua na kumshusha hadhi.