Watu wawili Mbaroni kwa wizi wa Tsh. milioni 105 Dar es Salaam

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watuhumiwa wanne, wakiwemo wawili wanaodaiwa kuhusika na wizi wa Shilingi milioni 105 na wawili waliokutwa na pikipiki za wizi, katika msako uliofanyika mwishoni mwa Julai na mapema Agosti 2025.

Tukio la kwanza lilitokea Julai 27, 2025, ambapo Mathias Charles Joakim @ Chingila (24), mkazi wa Salasala Kinondoni, na Kassim Abdallah @ Kipae (30), mkazi wa Tegeta, walikamatwa kwa tuhuma za kuvunja nyumba usiku na kuiba fedha taslimu mali ya Xue Huaxion, Mkurugenzi wa Kampuni ya Huaren.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam SACP Jumanne Muliro akizungumza na wanahabari siku ya Jumapili Agosti 10, 2025 amesema: “Baada ya upelelezi na kuhojiwa kwa kina pesa taslimu Tsh. Milioni 82 na Dola za Marekani 267 zilizoibwa zilipatikana. Hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wahusika”.

Katika tukio jingine, Agosti 8, 2025, polisi wamemkamata Hamad Mohamed Kamea @ Mpemba (49), mkazi wa Kigogo, na Abul Ramadhan @ Ally (20), mkazi wa Yombo, kwa tuhuma za kupokea mali za wizi, hasa pikipiki. Watuhumiwa hao walikutwa na pikipiki mbili — MC 537 EWT aina ya Boxer na MC 951 ESS aina ya TVS — ambazo zilidaiwa kuibwa katika maeneo tofauti.

Polisi pia wameeleza mafanikio katika kushughulikia kesi za ukatili na unyang’anyi, ikiwemo hukumu ya kifungo cha maisha kwa Musa Bakari (36), dereva mkazi wa Mbezi Makabe, aliyepatikana na hatia ya kulawiti, na kifungo cha miaka 30 kwa Khalifani Ramadhani (25), mkazi wa Kiponza Chamazi, kwa kosa la unyang’anyi kwa kutumia kisu.
 
Watafungwa maisha kwasababu ya wizi kwa kutumia nguvu robbery with violence.

Safi sana jeshi letu la polisi.
 
Majambazi wengi ni vijana wa miaka 24-39. Miaka ya hatarii sana kwa maisha ya mwanadamu.
 
Back
Top Bottom