Nitajitahidi nitumie kiswahili, kwani humu waswahili ni wengi zaidi, Japo Kingereza ni Lugha kubwa ambayo hubeba Maana ya neno kwa upana na fact.
mfano, unajua ni kwa nini pombe kali inaitwa spirit na roho kwa kingereza ni spirit ?
kuna sababu usifikiri mtengeneza maneno alikuwa kaishiwa maneno.
Tusitaabishane sana, naomba ukiona kuna jambo hulijui kabisa, uliza kwa heshima na utulivu tutafundishana..
Maombi (Prayer) hili neno wengi wakilisikia wanafikiri ni kitendo cha kuomba kama ombaomba (beggar).
Ukienda kumtafuta Mungu kwa lugha nzuri usiseme naenda kwenye maombi, sema naenda kuzungumza na Mungu.
Kwasababu Mungu haitaji wewe uongee yeye asiongee kwanza nikuulize wewe na baba yako Nyumbani nani huongea kwanza yapi yakufanya ?
So Prayer is two ways communication.
Maombi ni mazungumzo.
Niseme hivi mifano ipo Mingi sana kwenye biblia nikianza kuitoa hapa mtasoma hadi mshindwe kumaliza kusoma kama jinsi ilivyo watu wengi hawajasoma Biblia yote wala quran yote.
Wengi wanaitazama biblia kama kitabu cha amri za Mungu, na kujikuta wakibeba dini na mapokeo ya wazungu hao walio andika badala ya Kuangalia Maisha ya watu wakuu na waliomjua Mungu waliishi vipi.
Achana na Torati ya Musa, Unajua Musa alikua mtu wa tabia gani ?
Ibrahimu alikua na tabia gani.
Isaka alikua na tabia gani na anazungumzaje na Mungu,
Yakobo alikua na tabia gani na alikua anazungumza vipi na Mungu,
Ayubu mpigwa vitasa alikua na tabia gani, hakua na kanisa, wala worship team, tabia ya haraka alikua mtoaji sana, ni nani alimwambia atoe sana, alitoa kila mwisho wa mwezi, au kila jumapili ? au ijumaa au jumamosi? alimpa kila mtu, alikuwa rafiki wa kila mtu?
Usijifananishe na Danieli aliyeomba mala tatu bila kujua alikua anaombea au anazungumza na Mungu kuhusu kitu gani,
Tuje kwa Paulo huyu ndie Greatest wetu
Yesu alisema nimempa kazi kubwa sana ya Kunitangaza kwa nchi jirani zote,
Unajua aliishi maisha gani ?
Paulo kanisani kwake ilikua ni kufundisha mwanzo mwisho, na kuuliza maswali na kujibiwa full stop.
Sasa sisi wazee wa dini huku kwenye biblia tukachukua mila na sheria za wayahudi tukazipenda sana kuwa na zakwetu tukashindwa..
Mungu anapenda Jambo moja nalo ni Utii tu, akikwambia kitu fanya, au akisema jirekebishe. Ukitaka Mungu akufundishe kwa vitendo utaumia zaidi.
Pole kama unaona ni Ngumu na haiwezekani kumsikia Mungu.
Ukisoma kwenye biblia, ibrahimu kwa mala ya kwanza naya pili anasemeshwa na Mungu unajua aliambiwa nini ?
Na alisemeshwa kupitia njia gani ?
na Baba yake ibrahimu ambaye ni Tera alikuwa mtumikia mizimu.
Matendo ya Mitume 2:42
Wakawa wakidumu katika
fundisho la mitume, na katika
ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.
1. Mafundisho
2. Ushirika na kula
3. Kusali. hii kusali ipo mwisho viongozi walikua wanarudi na Neno kutoka kwa Mungu na kuliambia kundi. nini cha kufanya, sio kutoa sadaka petro na paulo wapate hela ya kuweka mafuta kwenye gari. au kucopy verse za torati na kesema hili ndio neno la Mungu. No hapana.
Walikua hawaruki na kucheza kila ibada ety kumsifu Mungu,? umeona Mungu anashida sana na sifa ety ???
Petro anahubiri kwa Maficho,
Ukiwa mlopolopo mtumishi wa Mungu, ukienda gerezani kama Petro unafikiri Mungu atatuma malaika akufate kukutoa ??
How to receive instruction ?
Three channel.
i. Impression (prophetic impression)
ii. Dream - is the highest form of revelation
iii Vision - is the highest form of sight π
Nimalizie huu mfano mmoja...,
Niseme tu hivi soma la kumsikia Mungu ni pana sana.. ukitaka kijifunza inawezekana Mungu anazungumza na mtu yeyote popote alipo hata jini zuri au baya Mungu akitaka kuongea nalo anaongea nalo tu.
How is your Master?????? Jitafakari.
Nina ushuhuda huu..
unamuhusu mtanzania ndugu yangu.
Ni kijana wa kiume mwenye degree course ya Afya, ni mtoto wa kiume peke yake kwao ana dada zaidi ya watatu.
Kuna Ndoto aliota ya Muhimu akiwa nyakati za maswali yanayotaka Majibu.
Kamaliza degree Safi, kaenda internship mwaka mmoja. kazi mwaka mmoja kisha serikalini ikamwambia nenda katafute ajira.
Ndoto Yake:
Kipindi internship imeisha,
Aliota Ndoto Lango Kubwaa limefunguka, alafu yeye akapita kwenye huo mlango, akiwa hana nguo yupo uchi, sasa kule mbele akakutana na watu ambao wanajaribu kumpa msaada wa Nguo ili kujisitili mwili, asibaki uchi, na yeye hapo akawa anatafuta sasa nguo itakayo mfaa..
Hakufanikiwa kupata nguo iliyomfaa na kumtosha hata moja kwa wale watu aliokutanan nao kwenye hiyo njia alikua akipita.
Maana ya Vazi....
Maana ya Lango au Mlango....
Kwanini alikua uchi ?
Hii ndoto ilikua ya mwaka jana kwa muhusika, hila hadi sasa amekwisha fanya kazi tatu na zote zinampa stress anayofanya sasa hajajua bado mshahara atalipwa sh. ngapi ? private sector kwa wahindi π¬π
kwenye kujiajiri kajaribu biashara mbili tofauti na kubwa tu, zote kwa sasa hana amani nazo tena na kaziacha.
Niko nae yeye hana shida sana kwani Yuko na mimi nitamsaidia vizuri tu muda sahihi ukifika.
Tunaendelea, Nataka sasa nijue kama wasoma biblia wapo nitembeze nondo za biblia.
God use the nature to speak.. Alimwambia adamu go and be fruitful.
Maana yake ni nini ?
Nenda kakue na kuongezeka, au ubarikiwe ni maneno yenye maana na sio wengi wanaelewa maana yake sasa hiyo sio lugha ya Mungu yeye hatumii maneno sana kusudi kufikisha ujumbe mkubwa kwa picha.
Yeye anakuonesha picha ya nini kinakuja, Shamba zuri lenye mazao mbalimbali zilizokuzunguka duniani. Unajua maana yake sasa.
Tunaendelea...... Subscribe ππΎ