Watu wengi wa Dar huwa wanajua huku Mwanza ukiwa na buku unapata ndoo ya samaki

Waeleze kuwa samaki wanauzwa kiasi gani, anahitaji wangapi? Mpe gharama.
 
Hata ukiwa mbeya wanadhani mchele unajchotea tu hawajui Bei vzr

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Hahahh kwl huyu mm kabisa. Nilienda mwanza nikaingia mgahawa mmoja mdogomdogo tu wakisela sela nkasema hapa niagize ugali na samaki wakutosha kuhisi kwamba itakua bei chee. Hee kuuliza eti Ugali na samaki ni 6,000 tena samaki mwnyew mdogo hana afya. Nikachoka.
 
Nashangaaga sana mtu akisema eti mkoani kuna maisha simpo
 
Kama ambavyo watu wa mikoani mnafikiri Dar kazi zimejaa Tele zinasubiri watu....Utasikia mdogo wako huyo mpokee umtafutie kazi
Enhe! Na hapo kazi inapokosekana ndipo anageuka kuwa miongoni mwa panyarodi.Vinginevyo akitua tu Dar we chap mpe kazi ya kugeuka kurudi alikotoka mikoani.Usimwache ajichanganye katika magenge - huenda akatwangwa risasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…