Sikiliza kwanza wewe kenge wa bara! Ugali unaweza kugawa robo tatu ukiwa solid kwa kukata 😅😅kama slices ila unga huwezi kupima kwa robo tatu ,una mengi ya kujifunga ila anza na kuoga kwanza.
Unga unataja vipimo exactly kutokana na mawe ya kupima ,hizo robo tatu labda ugali ushapikwa upo solid 😅😅kama unataka kula ukataka hiyo robo tatu .
Hivyo vipimo vya robo tatu mtapeleka mpaka kweny mafuta 😅😅kenge wa bara mna mengi sana ya kujifunza .
Mafuta tunatumia lita kama vimiminika vingine hata mazima ..Vipimo vingine ni mm .
Nasikitika sana namna ilivyoshindikana mjadala huu kuwa ni wa kuelimishana na kugeuka nafasi ya kutukanana.
Mimi kwetu nilikozaliwa ni bara tena bara ya mbali huko Ngara mkoani Kagera jirani na Rwanda na Burundi.
Lakini nimeishi Tanga mjini miaka 9 na nimeoa mwanamke wa kitanga na kuzaa nae watoto kadhaa.
Lakini pia mimi ni mwalimu wa madrasa, nasomesha elimu ya dini ya kiislamu kwa lugha ya kiarabu pamoja na masomo ya lugha ya kiarabu.
Mke wangu kwa kuwa ni mtanga neno nusu na robo hulitumia mara kwa mara na mimi mda mrefu nimekuwa nikomwambia hicho sio kiswahili sanifu bali kiswahili sanifu ni
robo tatu!.
Watetezi wa nusu na robo nimeona hoja yao kubwa na mawe ya mizani ya muuza duka na wamesahau kwamba sio mizani yote inayokuwa na mawe bali kuna mizani yenye umbo la saa ambapo mshale huzunguka kulingana na uzito wa kitu kinachopimwa.
Kuna mizani ya kisasa kidijtali yenye screen ambayo huandikwa namba kwenye screen kipnyesha kiasi Cha uzito wa kitu kinachopimwa. Kwahiyo mizani ipo aina nyingi na siyo kwamba yote inatumia mawe ya kupimia uzito. Kwa mfano tukipima uzito wa mtu mwenye kilo sabini na mbili na 3/4 ndio tuseme ana kilo 72 na nusu na robo au kilo 72 na robo tatu.?!
Lakini pia tukifananisha kiswahili na kiarabu mwarabu 3/4 hasemi
النصف و الربع!!!
Ukimwambia maneno hayo mwarabu ambayo maana yake ndio nusu na robo hawezi kukuelewa unazungumza nini lakini ukisema
ثلاثة أرباع
Atakuelewa vizuri na hiyo maana yake ndiyo robo tatu!
Mimi sina utaalamu na lugha ya kiingereza lakini hapo juu Kuna mwenzetu kaonyesha kwamba waingereza neno wanalotumia kwa hiyo mnayoita nusu na robo inafanana zaidi na robo tatu. (three quarters)
Mwisho ndugu zanguni wazanzibari nikuusieni kumcha mola wenu.
Mtu hujafa hujaumbika , usiseme huwezi kuja bara, eti utakuja kufanya nini.?!
Nyinyi sio werevu sana kumshinda kiongozi wa NCHI yetu ambaye ni mzanzibari na katika vyuo alivyosoma ni pamoja na Mzumbe chuo kilichomo Morogoro na yeye kwa sasa anaishi Bara.
Kwenye Baraza la mawaziri wapo wazanzibari ambao ofisi zao zipo Dodoma.
Dare s salaam kuna wafanya biashara wengi toka Zanzibar ambao wamejenga nyumba na kuifanya Dar kuwa makazi yao ya kudumu.
Ukienda chuo kikuu Cha Dar es salaam, Udom Cha Dodoma , Sua Cha Morogoro na vingine wapo wazanzibari wanasoma huko na wanaishi kwa amani bila bugha Wala chuki na yeyote . Tanga wapemba wamejaa na kwa Sasa nipo Moshi mjini pia Kuna mpemba yupo hapa kikazi na tunaswali pamoja na kunywa kahawa pamoja asubuhi.
Sasa wewe unayesema huwezi kuja bara ni kwakuwa wewe ni mwerevu kushinda wazanzibari waliopo huku bara?!