Achana na hao wamama watano, unaweza kupata mifano hata zaidi ya 1M ya ndoa zinazosumbua lakini ikawa si tafsiri ya ndoa yako itakavyokuwa. Ndoa ni nyinyi wawili kuamua jinsi itakavyokuwa. Na lazima muelewe kuwa wote wawili mna mapungufu mengi hivyo muwe tayari kurekebishana na kusameheana ingawa kuna mengine jua lichomeze au lizame hutaweza kuyabadili katu kwenye maisha yenu yote. Sisi binadamu kuna udhaifu tunao ni wa kudumu ni kama kilema. Kwa hali hii itakubidi uvumilie. Kuna mambo mache yasiyovumilika kwa wenzi wa ndoa kama, usaliti( uzinzi), kunyimwa tendo la ndoa, na kipigo.
Kwa kweli hayo mambo matatu ni hatari kwenye ndoa na ndio maana hata sheria za nchi hata vitabu vitakatifu yanaonyesha kuwa chanzo cha ndoa kuvunjika kama yapo na chanzo cha furaha ya ndoa kama hayatakuwapo. Hata uwe mcha Mungu namna gani au mwaminifu kwa kiwango chochote, mambo yote yatavumilika lakini kama mwenzi wako ni mzinzi na unafahamu, anakupiga kila siku, hakupi ulichofuata kwenye ndoa ( lile tendo ndio kiunganisho kikuu cha ndoa na sababu zingine ndogo zinafuata) basi jua uhai wa ndoa haupo na kama upo hiyo ndoa haina furaha.