kajekudya
JF-Expert Member
- Sep 24, 2015
- 2,466
- 4,916
Kwa wale ambao tumewahi kuwa watumishi wa umma tunakubaliana kuwa wapo Watanzania wengi tu wenye uwezo mkubwa kiakili.
Tatizo moja la nchi hii, watu hupandishwa na kupewa nafasi kubwa kwa kigezo cha nidhamu na utii kwa wakubwa. Yaani wale watumishi wasiohoji chochote,
wazee wa ndiyo ndio huonekana wanafaa na ndio hupendekezwa kwenye nafasi fulani fulani.
Mwisho wa siku hawa ndiyo wanakuja kuwa senior civil servant na decision makers. Bahati mbaya 90% ya watu hawa ni C student silaha yao kubwa ni kujipendekeza na unafiki, ndiyo maana siku hizo maofisini watu wamewekza kwenye uchawa kuliko weledi. Maana weledi haulipi. Sasa hawa watu wapofikia level ya senior civil servant na kuwa na majukumuu makubwa ya kutoa maamuzi ndiyo hapo madudu tupu. Refer Clip ya Job Ndugai kuhusu negotiations.
Shida ya big brain huwa wanajiamini, wanaamini katika uwezo wao, hawaamini katika unyenyekevu na kujipendekeza ili kufanikiwa kwenye utuminishi, hawapendi kujitembekeza. Matokeo yao wengi wao huishia kipigwa vita na kushafuliwa mafaili kwa hoja ya kutokuwa watiifu. Kwahiyo tuendelee kuwa wavumilivu kwakuwa tumechagua utiifu Kama njia ya kupata tija badala ya uwezo wa mtu.