Tatizo letu kubwa ni kukosa kujiamini au kujikubali. Hali hii imetokana na hao wazungu walipokuja wakatuvuruga na kuona kile tulichokuwa tunafanya si chema.
Kama historia inasema kweli juu ya mabadiliko na hatua za maendeleo ya watu wa kwanza, kuwa walichonga mawe, wakafikia hatua ya kufua vyuma ili kupata vifaa mbali mbali na mambo mengi ya kimaendeleo. Je, kama wageni wasingeingilia mifumo yetu ya ubunifu unadhani leo hii tungekuwa wapi? Tungewaza utegemezi kama unavyowaza?
Wageni walipoona tuna hatua fulani ya ubunifu, wakadai kuwa tuyafanyayo Ni ya kishenzi. Wakazidi kutu-terrorise kwa kukamata viongozi wetu, kuharibu tamaduni zetu. Wakeleta mambo ya kwao ili kuwanufaisha wao. Hapa ndipo tulipoanza kuharibikiwa. Wakatubwetesha kutuletea elimu ambayo kwa wale ambao walionekana wabunifu miongoni mwetu waliwachukuwa kwenda kuwafanyia kazi zao, hii ilifanyika kuzima maono ya wale walioonyesha upeo wa kufahamu mengi.
Mambo ni mengi Ila kijumla ni uzuzu kuwaza nchi kuikabidhi kuendeshwa au kuingizwa na wazungu. Ni kujidharau kusikofaa. Ningekuunga mkono Kama ungekaribisha mjadala na michango mbali mbali namba gani juhudi zifanyike ili kupata maendeleo.
Kama wewe huna akili juu ya nini tufanye ili tuijenge nchi na kupata maendeleo; wapo watu humu wana maono mazuri Ila tu hawako katika nafasi za maamuzi.