Mleta Uzi asipuuzwe, pengine ametumia lugha kali kuwasilisha hoja yake lkn tumsamehe tu, tujikite kwenye maudhui ya hoja yake.
Waafrika tuna shida kubwa sana ambayo ni ubinafsi. Hatuna uzalendo kwa Mataifa yetu hata kidogo. Si viongozi wala Wananchi wa kawaida.
Hii haimaanishi kwamba hawapo wachache waadilifu, la hasha! Wapo, ila wakiibuka tu huwa wanapigwa sana vita au hata kuuawa!
Mbaya zaidi hata wazungu wameshaufahamu huu udhaifu wetu, kwahiyo wanatupeleka watakavyo.
Kuna wakati huwa natamani nijitokeze kwenye media niwachane live halafu nianzishe movement , kama wananiua waniue tu. Mwanazuoni mmoja aliwahi kusema, "matumizi bora ya maisha ni kufanya kitu kitakachodumu kuliko maisha yako", kwahiyo wakiniua walau nitaacha alama ya kudumu kuliko kukaa kimya tu, kwanza ni dhambi hata kwa Mungu kwa kutokemea mabaya.
Mungu atusaidie sana!