MIRA01
JF-Expert Member
- Sep 18, 2023
- 319
- 695
Nikuongezee na mfalme suleimani! Wimbo ulio bora 1:5 sasa kama yy ni mweisu baba yake je? Mfalme daud?1: Mwanamke Zipora
Alikuwa mke wa kiongozi bora wa taifa la kiyahudi, Musa. Alikuwa mweusi. Ushauri wake uliongeza ufanisi wa wayahudi. Baba yake Alikuwa na akili kuliko Musa. Yeye ndiye alimfundisha ugatuzi wa madaraka Musa na Mungu akamwambia Musa aufuate asiupotezee ushauri wa baba mkwe..
2: Simon Mkirene
Huyu alikuwa muafrika kutoka Libya zamani Kirene. Huyu alimsaidia Yesu msalaba kuelekea Goligota. Wenda pasipo yeye Yesu angefia njiani na ukombozi kupata dosari. Mwafrika ni mtu muhimu kwa wokovu wa mwanadamu tangu miaka 2000 iliyopita.
3: Muethiopia
Huyu ndiye mtu wa kwanza kurekodiwa katika biblia asiyemuyahudi kubatizwa. Alikuwa tajiri mkubwa maana mtu wa kawaida ilikuwa vigumu kutoka ethiopia hadi Jerusalem kwenye ibada za kiyahudi. Waafrika matajiri na wenye ushawishi walianza kumpokea Yesu na kumuabudu Mungu wa biblia miaka zaidi ya 1500 kabla ya mzungu kukanyaga Afrika. Mwafrika alianza kumjua Mungu wa kwenye biblia kabla ya mzungu wa magharibi.
Afrika pia imewatunza na kuwalea magwiji wakubwa katika biblia.
Yusufu na israel yote imekulia afrika. Misri.
Ibrahim alipopigwa njaa, alipona kwa kukimbilia misri.
Yesu alipotaka kuuwawa utotoni alikimbizwa misri.
Mwafrika Farao Neko aliwahi kumuua mfalme wa israel Yosia kwa sababu tu alimzuia asipite kwenda kufanya kazi ya Mungu wa israel huko iraq (babeli). Mungu amekuwa akuwatumia waafrika kwa kazi zake tangu siku nyingi.
Kwa hiyo kuendelea kuabudu mizimu, mababu, na ushirikina kisa dini ya Biblia ni ya wakoloni ni mtazamo uliojengwa katika hofu za kujitungia.
Barikiwa.
Samson
Hakuna mzungu wala kabila lolote linaloweza kufuga nywele zijisokote na kuwa vishungi saba! Ni mtu mweusi pekee amepewa hiyo neema ya kufuga rasta, au wewe umemuona mzungu rasi wap?
Waisrael ya kale
Huwezi kupita juani miaka 40 na usipate madhara ya ngozi never waisrael sio wazungu wana asili ya africa yaani nyeusi