Watu weusi ndio walivuka bahari kuu na kufanya ustaarabu kote Asia na Ulaya

Watu weusi ndio walivuka bahari kuu na kufanya ustaarabu kote Asia na Ulaya

Wasomi wa zamani wa Mexico waliamini kwamba athari za watu weusi katika Dunia Mpya zilikuwa kubwa na za kudumu. Mwandishi mmoja, J.A. Villacorta, anasema: "Kwa njia yoyote unayoona, ustaarabu wa Mexico ulikuwa na asili yake Afrika." Uchunguzi wa kisasa nchini Amerika ya Kusini unaonekana kuthibitisha hitimisho la Villacorta. Ustaarabu wa Olmec, ambao unaonekana kuwa na asili ya Kiafrika au kuwa ulisabishwa na Waafrika ulikuwa Utamaduni Mama wa Mexico. Kati ya hayo, Michael Coe, mwanahistoria wa kwanza wa Marekani wa Mexico, ameandika kuwa, "hakuna Shaka hata kidogo kwamba ustaarabu wote baadaye [Mexico na Amerika ya Kati], ni wa waafrica Ivan Van Sertima, amekiri juu ya uwepo wa Kiafrika huko Amerika ya kale, amejenga kesi kali inayoonyesha kuwa tabia nyingi za kitamaduni za Olmec zilikuwa za asili ya Kiafrika: "Uchunguzi wa ustaarabu wa Olmec unaonyesha vipengele ambazo ni karibu na tabia za kawaida za ibada katika Dunia ya Misri-Nubian ya kipindi hicho ambacho ni vigumu kudumisha [kwamba] yote haya yanatokana na tu bahati mbaya. " Wataalamu wengine wanaamini kwamba Waafrika walianzisha kalenda, kuandika, piramidi na ujenzi wa kaburi, mummification, pamoja na mifumo fulani ya kisiasa na mila ya kidini kwa Wamarekani wa asili. Ni Wao Waafrika ambao walikwenda Amerika kabla ya Columbus. Msomi wa Kihindi R.A. Jairazbhoy anasema kwamba wasafiri na mafundi wa kale wa Wamisri wakiongozwa na Mfalme Ramesis III, wakati wa nasaba ya 19. Van Sertima pia anaamini kuwa wengi wa wachunguzi walihamia kutoka Misri, lakini wakati wa baadaye wa nasaba ya 25. Wasomi wengine wengi wanasisitiza kuwa wavumbuzi walikuja kutoka mataifa ya Magharibi mwa Afrika, kama vile Ghana, Mali na Songhay watu mweusi , kwa hakika walihamia Marekani kwa nyakati za kale na za kati na wakaacha alama kubwa juu ya udongo wa Dunia Mpya. Kama Jairazbhoy anavyosema: "weusi walikwenda kitambo mno Ulaya na Amerika si kama watumwa bali kama mabwana."
Legrand H. Clegg II
 
Tuache hii ujinga. Mimi binafsi nilisoma sana haya mambo yanayohusiana na Afrocentrism na blah blah nyingine kibao. Mwisho wa siku nikaona ni ujinga tupa kule. Hoja ni mufilisi. Sisi tupambane kuwafikia wenzetu. Ni sawa na wale wanaokaa vijiweni na kuanza kusema 'enzi zangu nilikua...'. Waafrika tuna safari ndefu sana sana.
 
Tuache hii ujinga. Mimi binafsi nilisoma sana haya mambo yanayohusiana na Afrocentrism na blah blah nyingine kibao. Mwisho wa siku nikaona ni ujinga tupa kule. Hoja ni mufilisi. Sisi tupambane kuwafikia wenzetu. Ni sawa na wale wanaokaa vijiweni na kuanza kusema 'enzi zangu nilikua...'. Waafrika tuna safari ndefu sana sana.
Mawazo yako
Appreciated
Lakini mpaka umeijua kamba ilokufunga, ukaifungua fundo kwa fundo huchomoki kamwe, tatizo takwimu, ...watu wana husianisha matatizo ya Africa na miaka 2000, iliyopita, kumbe ni marefu mno kuliko hapo
 
Hakuna ushahidi unaoonyesha Imhotep alijenga pyramids Imhotep alikuwa biologist akihusika hasahasa na mambo ya aulitcation.

Lakini pyramid zimejengwa before Imhotep Kwenye first kingdom hukoo.
Upon sahihi,nilichanganya, imhotep alijenga pyramid ya djoser...lakini awe asiwe, whoever built the great pyramid was a black man, ni kama kubishana Eiffel tower ilijengwa na mzungu, sa tunabishana nini,ufaransa kwa waswahili?????
 
Kitu cha ajabu hiki kama tuliwafunza mbona wametuzidi maarifa ilhali sisi ndiyo tulikuwa wajuzi wa yote hayo??
India wanawaficha wahindi weusi wenyeji asilia China kuna wachina weusi ,brazili, spain , portugal, Spain kote wenyeji, ugiriki na Roma, kote duniani, na walikuwa huko maelfu ya miaka kabla ya biashara ya utumwa, mtaficha mpaka mchoke na dhambi yenu ya ubaguzi itawatafuna tu MTU mweupe kaja juzi hapa duniani....hata hapo Zanzibar mwazani mtaificha histori ya mweusi mwenyeji????
 
Ukishamaliza wewe kunionyesha ustaarabu mmoja wa weupe pekee Bila ya mchango na msingi wa watu weusi kwanza kabla na baada ya kuzaliwa kristo
Hii ni dalili ya kukwepa kutoa jibu la moja kwa moja nililokuuliza, ingependeza zaidi ukajikita kwenye kutoa jibu ili utoe mwanga na kwa wale ambao hatuoni popote palipo jaa weusi pakawa mfano wa kuigwa kwa maendeleo ya kiuchumi
 
Hii ni dalili ya kukwepa kutoa jibu la moja kwa moja nililokuuliza, ingependeza zaidi ukajikita kwenye kutoa jibu ili utoe mwanga na kwa wale ambao hatuoni popote palipo jaa weusi pakawa mfano wa kuigwa kwa maendeleo ya kiuchumi
Zile piramidi za Zimbabwe zilijengwa na wazungu pia sio????
 
Mbona mwenzio anakuletea data we huleti ???? Wabisha tu kufurahisha jopo ama wataka kujenga hi nyumba ya bibi na babu zako iliyobomolewa????
Mimi nilimuuliza swali wala sikuhitaji mjadala wa hoja, hivyo baada ya swali langu kushindwa kunipa majibu ndipo akaanza kuleta habari zisizo na mahusiano yoyote juu ya swali langu
 
Watu walikatwa mikono mafundi, watu waliuliwa, maarifa yaliibiwa, system ilichafuliwa, we vipi ndugu?????
Ilichukua miaka kama elfu sita 6000 hivi kuharibu utu na bara la mtu mweusi,kabla ya kuzaliwa kristo ukijumlisha hiyo 2000 baada ya kuzaliwa kristo ni karibu millennia 8, nyie vipi ndugu? Afu ukimwambia MTU, ana kuletea habari za mkutano wa Berlin karne ya 17
 
Back
Top Bottom