Watu weusi watabaki masikini na duni milele

Si kweli.

Naona umewaza kwenye soko la ajira tu lakini mimi sina dhana hiyo.

Mimi dhana yangu ni kujitegemea kiuchumi kuyatafta maendeleo yetu wenyewe na wala si kwenda kwenye soko la ajira kimataifa.

Lugha yako asilia haiwezi kuwa kizingiti cha wewe kupiga hatua mbele.

Kwani Ujeruamani lugha rasmi ni kingereza ? kwani wao hawajawekeza ?

Ufaransa Je, wanatumia kingereza ? Ulaya in general ukitoa UK wanatumia kingereza kama lugha rasmi ?


Haya DUBAI hapo falme za kiarabu wanatumia kingereza kuwa lugha rasmi ? Saudia Arabia Je, na South Korea au Japan je ?

Hoja ya kuacha kiswahili na kufata lugha zingine haina nguvu kabisa.
 
Wewe sema tu umeridhika na hali uliyonayo ila hakuna kinachoshindikana.

Huo mfumo umeanzishawa na wanadamu ni kipi kishindikane ?

Hivi nguvu ya ROMAN EMPIRE ulikuwa unaijua wewe ?

Na ilitawala kwa miaka zaidi ya 1000 tena takribani nusu ya eneleo lote la dunia lilikuwa chini ya roman empire na bado ilianguka.

Leo USA na kambi yake ya ubepari isianguke kwanini ?

Usiwe na limitation na knowledge broo.

Gharama za ukombozi lazima ziwepo na za muda mrefu, lakini isitufanye sisi tukate tamaa kwamba hatuwezi
 

Vyuo vya nchi zote ulizotaja hapo juu havitoi elimu kwa local language, kwanini?

Hotel na public establishment zote kwenye nchi hizo zinaweka English as a subsidiary medium of instruction, kwanini?

Bidhaa zinazoundwa kwenye nchi ulizoainisha kwa lengo la export zinakua na maelekezo ya lugha za UN, kwanini?

Yaani kuweka hiyari kwenye kujifunza lugha ya Kiingereza ni kugongelea msumari wa mwisho kwenye jeneza. Athari zake hazipo tu kwenye ajira, zipo kwenye biashara, teknolojia, sanaa mpaka afya.

Huwezi kuwa na jeuri hiyo kama nchi yako bado ipo nyuma kimaendeleo. Nakupa mfano wa mama yangu anaenunua dawa na kutumezesha bila kujua kilichoelezwa kwenye maelekezo.
 
Hoja yako ya lugha bado haiwezi kuwa na nguvu hata kidogo.

Kwa sababu sisi ni wategemezi kwao kwenye kila kitu na ndiyo maana unaona lugha ina impacts.

Mfano wa dawa uliotolea, kwani sisi tungekuwa wa wataalamu wetu hapa wa kutengeneza dawa ulikuwa unaona kuna una umuhimu wa wewe kununua hizo dawa ?

Sisi kama tutajitosheleza vitu vingi hapa utaona umhimu gani wa kufata kitu nje ?

Kwa hiyo unataka kunambia taasisi za elimu ya juu huko nje kama iran, china,korea,japan, uturuki, ufaransa, ujerumani n.k lugha rasmi ya kufundishia ni kingereza siyo ?
 

Kwa nukuu yako hii nadhani umeshaelewa ninachokwambia, "Kwa sababu sisi ni wategemezi kwao kwenye kila kitu na ndiyo maana unaona lugha ina impacts."

NDIO. Majority ya vyuo vilivyopo diaspora vinafundisha kwa lugha la Kiingereza. Ni uongo?
 
Kwa nukuu yako hii nadhani umeshaelewa ninachokwambia, "Kwa sababu sisi ni wategemezi kwao kwenye kila kitu na ndiyo maana unaona lugha ina impacts."

NDIO. Majority ya vyuo vilivyopo diaspora vinafundisha kwa lugha la Kiingereza. Ni uongo?
Dogo akili umeficha wapi ? Lugha ya kiingereza haiwezi kuifanya Afrika kuwa Europe au Asia kimaendeleo, Afrika kuna upumbavu mwingi sana unao kwamisha maendeleo ya Afrika mojawapo haya mawazo yako.
 
Miafrika hovyooo!

Mijitu inaiba trillions halafu wenzao hawana hata ule uwezo wa kununua hata Aspirin. Who does that? Hata monkeys huwa wanajaliana na kusaidiana kuliko Mwafrika kwa

Kwa nukuu yako hii nadhani umeshaelewa ninachokwambia, "Kwa sababu sisi ni wategemezi kwao kwenye kila kitu na ndiyo maana unaona lugha ina impacts."

NDIO. Majority ya vyuo vilivyopo diaspora vinafundisha kwa lugha la Kiingereza. Ni uongo?
Ni uwongo ndiyo.

Majority universities kwa nchi za wenzetu wanafundishana kwa lugha zao wenyewe.

Ni vyuo vichache sana tena kwa ajili ya minorities zaidi ndiyo wanafundisha baadhi ya kozi kwa lugha ya kingereza.

Hivi nikuulize swali la mfano : INTERNATIONAL SCHOOL of TANGANYIKA, au ST COSTANTINE INTERNATIONAL SCHOOL, or FEZA SCHOOLS maybe ambazo zote zipo Tanzania na zinatumia mitaala ya elimu ya CAMBRIGE, unaweza kutumia hizo shule kama kigezo cha kusema kwamba shule za msingi na sekondari tanzania zinatumia mitaala ya chuo cha CMBRIGE uwingereza ?
 

Attachments

  • Gallery_1691483870243.jpg
    83.1 KB · Views: 1
Una kitu, usikilizwe
 
Lugha na utamaduni ndiyo hoja zake
Anaongoe upuuzi tu. huwezi kufundisha wanafunzi kwa lugha ya kiingereza hapa Tanzania wakati matumizi ya lugha ya kiingereza bongo ni hafifu kabisa ninaweza kusema hayapo.

Watu wanapiga kiswahili mitaani kuanzia asubuhi mpaka usiku hakuna kiingereza sehemu yoyote halafu unataka hawa watu uwafundishe kwa kiingereza lazima uwapoteza ndicho kinacho tokea bongo upuuzi wa wizara ya elimu katika lugha ya kufundishia.
 
Dogo akili umeficha wapi ? Lugha ya kiingereza haiwezi kuifanya Afrika kuwa Europe au Asia kimaendeleo, Afrika kuna upumbavu mwingi sana unao kwamisha maendeleo ya Afrika mojawapo haya mawazo yako.

Huwa sijibu AD HOMINEM mkubwa. Chukua ushindi wa mezani.
 
Upuuzi tena sana.

Mimi naamini lugha kiswahili ingekuwa lugha ya kufundishia kwa ngazi zote, tungekuwa na wapumbavu wachache tu.

Maana kwanza wadogo zetu wa O-level wengi wao wanaendaga kukariri vitu wanavyofundishwa kwa ajili ya kuja kuvifanyia mtihani na siyo kuvielewa vitu vimsaidie.

Japo napo lugha sehemu tu vitu vochache vinavyochangia kufeli kwetu,ila tatizo hasa lipo kwa uongozi mbovu, hawana maono mazuri, wanatusaliti kwa ajili ya maslahi ya mabepari na kuahidiwa kitu kidogo, na pia zaidi watanzania/waafrica hatujafunzwa kujipenda na kuwa wazalendo utaifa wetu
 

Miezi kadhaa iliyopita, embassy ya Japan ilitangaza scholarship kwaajili ya undergraduates. Kwenye web yao, top 10 ya vyuo vyote vilivyoweka vinatoa elimu kwa Kiingereza. Clause ya kujifunza lugha yao kwa muda fulani sio kwasababu ndiyo inayotumika kufundishia courses zote.

Arguably, top 100 universities worldwide zinatumia English.
 

Broo kuwa mwelewa, lugha siyo kikwazo strong cha sisi kuendelea huo ni umbulula.

Mbona zimbambwe wanatumia kingereza umeona wamekuwa matajiri ?

Maendeleo hayana excuse ya lugha bali sisi tuna na maujinga tu mengine ya ki-utawala na kukosa uzalendo wa kujipenda.

Mimi nazungumzia majority universities huko ng'ambo siyo vyuo vya binfsi vya kigeni.

Kwani hapa tanzania hakuna mtu yeyote mgeni akaamua kuanzisha chuo akaanza kufundisha kozi zake kwa kichina ? Sasa hiyo ndiyo utasema vyuma vya nchi husika hiyo vinatumia kichina.

Majority universites kwenye nchi za wenzetu wanatumia lugha zao wenyewe na siyo kingereza kama unavyo ng'ang'ana wewe.

Kwani maendeleo ya wachina kipindi cha MAO ZE DONG yaliletwa na kingereza ?

USSR ya JOSEPH STALIN ilifanya modern industrilization kwa kingereza ?

Mbona kuna vitu vina uelewa wa kawaida sana ?
 
Wewe umefanya nini kusaidia watu weusi wapate maendeleo.

Au unaishia kulalamika na kulaumu tu. Hata ukilaumu, unamlaumu nani sasa?

Mtu unakuta analaumu Afrika ni maskini, sawa ni maskini lakini je? wewe umefanya nini kuondoa huo umaskini?

Mtu anasema Afrika elimu yetu ni mbovu ya kukariri, sawa ni mbovu ya kukariri. Wewe umefanya nini ili kuibadili?

Kulaumu na kulalamika, wakati wewe mwenyewe hujafanya chochote huwa naona nao ni upumbavu tu.
 

Haya umefanikisha jambo lako, tumepata wahitimu waliosoma kwa kutumia lugha ya Kiswahili mpaka walipohitimu chuo, wataisaidiaje nchi kupata maendeleo na wakati mambo yote yatakuwa mageni kwao?

Tumefanikiwa kumpata daktari aliesoma kwa lugha ya Kiswahili, dawa zote tunapokea kutoka nje zikiwa na maelekezo ya lugha ngeni kwake, tuajiri na mkalimani tena?

Tumepata fundi magari msomi ila magari yote na vifaa vyote vimetoka nje ya nchi na vimeletwa vikiwa na maelekezo ya lugha ya kigeni, tuanze kuajiri watafsiri pia?

Sipuuzi umuhimu wa kuendeleza lugha yetu ila ninapinga kuitumia kama lugha kuu katika mambo nyeti ambayo bado hatujawa na uwezo wa kujitegemea.
 
Upuuzi ni wewe kuweka lugha mbele kwamba ndiyo inaleta maendeleo.

Lugha ni chombo tu kinacholeta umoja, mshikamano na ushirikiano maana tukishaanza kuelewena ni rahisi kwenda pamoja kuliko tusipoelewana.

Hivi imagine kiswahili kisingelikuwepo, hii tanzania ingevunjika vipande kuwa nchi ngapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…