Searching for the truth
JF-Expert Member
- Mar 22, 2022
- 903
- 1,851
- Thread starter
- #161
Hayo matatu uliyoyasema ni miongoni mwa mazuri sana.Huwezi kujiona sahihi iwapo unaweza kuiga mfumo wa mtu mwingine na hauwezi kuutumia au kuufuata, lazima uwe tofauti naye tu na yeye akuongoze maana ndiyo mwenye mfumo wake uliotokana na akili yake
Waafrika ni watu Bora sana kuliko unavyotaka kujidharau, kilichokosekana ambacho kilitokea mbali ni mambo makuu matatu tu
Ilipaswa kua hivi:
1. Africa iwe nchi moja
2. Yenye Lugha moja na pesa moja ya kwake
3. Yenye mfumo wa elimu ya kwake nje kabisa na mfumo wa mtu mwingine kama wafanyavyo Russia na China
Katika hayo mambo matatu Kuna matawi mengi sana ndani yake ambayo yangetufanya tujiendeshe na si kujidharau kama mtu mweusi sijui ni wa hovyo, basi tungekua wa hovyo hivyo hivyo kupitia hayo mashina matatu niliyosema na tungefanya nao biashara hivyo hivyo kulingana na u hovyo wetu
Sisi ni watu wagumu,wenye ngozi nzuri,nywele nzuri,wavumilivu wa hali ya hewa, wenye akili ya kwetu na MUNGU alituweka kwa makusudi Bora kabisa Duniani
Kamwe sita udharau utu wa mtu mweusi hata siku moja
Na hata waasisi wa mataifa yetu kama kina nyerere, nkurumah na Gaddafi walishawahi kuwa na hayo mawazo.
Lakini mabeberu wakawafelisha kwa kuwatumia waafrica hao hao.
Sasa kama tumeshindwa kufikia malengo hayo na tuona kabisa dalili za kufikia hazipo, kama si laana ni nini ?