Binti wa zamani
Platinum Member
- Nov 19, 2011
- 15,052
- 36,866
Haijalishi wewe ni muislamu au mkristo, kama una imani yoyote inayoamini kwenye "Mungu" nina maswali hapo chini kwa ajili yako.
- Kwanini Mungu anaruhusu watoto wazaliwe na changamoto za kiafya ambazo hazina tiba na zitawatesa watoto mpaka wanapokufa wakiwa bado watoto wachanga au wadogo? (cancer za watoto, matatizo ya moyo, ubongo, upumuaji etc.)
- Kwanini mungu wako anaruhusu ujauzito utungwe, mtoto akue mpaka akaribie kuzaliwa halafu afie tumboni?
- Naomba kueleweshwa; kwanini Mungu wako muweza yote, anaruhusu vifo vya watoto wasio na hatia? Na, ni nini sababu ya kuwaumba watoto wakiwa na mapungufu ambayo anajua yatakatisha uhai wao?
SABABU YA KULETA HUU UZI:
Nimeumia ðŸ˜, mtu wangu wa karibu amepoteza watoto wawil mapacha; mmoja amefia tumboni, mwingine amezaliwa na uvimbe kichwani, amemaliza siku tano amefariki. Inaniwia vigumu kuamini kwamba kuna sababu yoyote hawa watoto walistahili hayo waliyoyapitia.
Naomba utumie lugha nyepesi na unifundishe, kama kuna Mungu kwanini anaruhusu mambo ya kikatili namna hii?
Asante na Alamsiki!