Watu wote mnaomuamini Mungu mje, nina swali kwenu 😢

Watu wote mnaomuamini Mungu mje, nina swali kwenu 😢

Kama aliweza kumfukuza Adam na Eva bustanini akawapa adhabu.. huyu akatafute kwa jasho, huyu akazae kwa uchungu. basi wacha tuendelee kunywa hicho kikombe, ukiachana na maswahibu ya ulimwengu wa giza wa kina Mshana
 
JIbu lako lipo kwenye maswali yangu

1.kwenye huu ulimwengu je ni binadamu peke yake mwenye akili ya kiwango cha juu?

Kama ni ndio naomba uthibitisho

2. Ikiwa wewe unaweza kuunda vitu kwa kutumia kanuni fulani, je hakuna mwingine mwenye uwezo wa kuunda vitu fulani kwa kanuni zake zilizo ndani ya uwezo wake?
 
Hakuna Hali iliyokamilika, Kila Hali ina upungufu wake na uimara wake.
giphy 22.GIF

Hakuna maana ya kuwepo kiumbe chochote duniani ikiwa Kila kitu Kipo 100%, hii ni fikra ya kawaida tu inayozunguka sayari na nyota zote za ulimwengu...
Hii ina apply vipi kwenye vifo na mateso ya watoto wachanga?
 
Mwanadamu ana duo, katika duo ya mwanadamu ipo governed na spiritual principal and laws. Ukiona kuna baya limetokea kwa mwanadamu ujue kuna rules and principal zimekuwa violated kwa will katika namna ya direct au indirect kwa muhusika kujua au kutojua, ambayo sheria hiyo hiyo ina funga uwezo wa Mungu kufanya intervision kwasababu zinaongiwa na kanuni na sheria ambazo yeye mwenyewe alijiwekea kuhusu na utawala kwa mawanadamu

Naona hoja yako umechanganya Mungu na Sayansi au hizo Laws. Ila ni ngumu kidogo kuoanisha.

Na hata kama.
Sasa kama Mungu ataruhusu hizo laws zifanye kazi.
Kwanini yeye asiingilie kati hasa kwenye watoto ambao hawana hatia?.

Mtoto anaweza kufariki kwa mambo kadha wa kadha. Labda genes. Ukuaji usio wa kawaida wa seli au magonjwa na maambukizi.
Why Mungu asizuie haya kwa watoto ambao hawajafanya dhamb yoyote? .
 
Mungu ni business za wajanja ndio maana mungu waliye aminishwa Waafrica na kumkarili siye mungu ambaye wachina wana muamini au wahindi na Bado wana mafanikio makubwa kuliko watu Waafrica it means mungu wanaye Muamini Waafrica ambaye walifundishwa na wazungu + Waarabu ameshindwa kuwa mungu mtatuzi wa kero zao kiasi kwamba amezidiwa na mungu wa Wa china na wahindi !!!

Shtuka
Mkuu endelea, nakusikiliza!
Bored Kanye West GIF.gif
 
Haijalishi wewe ni muislamu au mkristo, kama una imani yoyote inayoamini kwenye "Mungu" nina maswali hapo chini kwa ajili yako.
  1. Kwanini Mungu anaruhusu watoto wazaliwe na changamoto za kiafya ambazo hazina tiba na zitawatesa watoto mpaka wanapokufa wakiwa bado watoto wachanga au wadogo? (cancer za watoto, matatizo ya moyo, ubongo, upumuaji etc.)

  2. Kwanini mungu wako anaruhusu ujauzito utungwe, mtoto akue mpaka akaribie kuzaliwa halafu mtoto afie tumboni?

  3. Naomba kueleweshwa; kwanini Mungu wako muweza yote, anaruhusu vifo vya watoto wasio na hatia? Ni nini sababu ya kuwaumba watoto wakiwa na mapungufu ambayo anajua yatakatisha uhai wao?

    SABABU YA KULETA HUU UZI:
    Nimeumia 😭, mtu wangu wa karibu amepoteza watoto wawil mapacha; mmoja amefia tumboni, mwingine amezaliwa na uvimbe kichwani, amemaliza siku tano amefariki. Sitaki kuamini kwamba kuna sababu yoyote hawa watoto walistahili hayo waliyoyapitia.

    View attachment 3588755

    Naomba utumie lugha nyepesi na unifundishe, kama kuna Mungu kwanini anaruhusu mambo ya kikatili namna hii?

    Asante na Alamsiki!
Kwanini kabla mtu wako wakaribu hayajamsibu hukuuliza?

Acha tuupe jibu liliozoeleka na ninyi mungu hayupo
 
hizi dini tatu hizi za Abrahamic Religions huwa hazihitaji mtu utumie reasoning wala logical thinking.
Ukianza kufanya reasoning na logical thinking tu, kuna maandiko mengi utaanza kuya-doubt kwenye dini yako.

Hawataki maswali ya ku-reasoning.
Ukifanya reasoning, starting asking questions, watakushambulia na kukwambia "imani yako haba."

Faida kubwa ya hizi dini, zimeongeza ustaarabu, otherwise dunia ingekuwa troubled mno.

Ukizichukulia hizo Abrahamic Religions kwa mtizamo huo, ni poa sana.
Just lower your expectations lakini lenga mbali (aim very far) tufute chozi kisha tusogeze siku, when our time is up (death) tutarudisha nutrients kwenye food chain - food web.

Tutarudisha nutrients ili viumbe vingine vistawi kwa hizo nutrients (directly or indirectly) na hivi viumbe vingine navyo muda wao utaisha, vitarudisha nutrients na vyenyewe, the circle goes over and over again.

Life! Ukiliwaza sana logically , unaweza usione umuhimu wa kuwepo duniani, kila pakikucha tunazidi kusogea kwenye kifo.

Uzuri ni kwamba kila binadamu anayo ile mentality kwamba "kesho will be a better day" ila without this one, aiseeee tungekuwa "wanyama (cruel)" mno, the end of humanity.
 
Naona hoja yako umechanganya Mungu na Sayansi au hizo Laws. Ila ni ngumu kidogo kuoanisha.

Na hata kama.
Sasa kama Mungu ataruhusu hizo laws zifanye kazi.
Kwanini yeye asiingilie kati hasa kwenye watoto ambao hawana hatia?.

Mtoto anaweza kufariki kwa mambo kadha wa kadha. Labda genes. Ukuaji usio wa kawaida wa seli au magonjwa na maambukizi.
Why Mungu asizuie haya kwa watoto ambao hawajafanya dhamb yoyote? .
Hamna nilicho changanya mkuu, nachoo ongea nakijua na nimefanya tafiti kwa miaka 20. Mambo ya rohoni yana kanuni kibao na sheria zake na ndio zina athiri maisha yetu ya kila siku
 
Naona hoja yako umechanganya Mungu na Sayansi au hizo Laws. Ila ni ngumu kidogo kuoanisha.

Na hata kama.
Sasa kama Mungu ataruhusu hizo laws zifanye kazi.
Kwanini yeye asiingilie kati hasa kwenye watoto ambao hawana hatia?.

Mtoto anaweza kufariki kwa mambo kadha wa kadha. Labda genes. Ukuaji usio wa kawaida wa seli au magonjwa na maambukizi.
Why Mungu asizuie haya kwa watoto ambao hawajafanya dhamb yoyote? .
RC tunaambiwa kuna dhambi ya asili.. tuliyorithi kwa kina Adam na Eva. So watoto wanazaliwa nayo.. ndio maana tunabatizwa… kwa wengine sijui.. so kikombe hakiepukiki
 
Mwenyezi Mungu atasalia kuwa Mungu milelena milele haidhuru ni hali gani ikutayo mwanadamu .

Kwanza mwanadamu ni kiumbe mdogo sana katika viumbe wa ulimwengu ni vile tu amejipa umuhimu kuliko vyote.

Mwenyezi Mungu ni mkamilifu na mwanadamu na viumbe vingine vyote ni dhaifu, udhaifu wetu ni pamoja na changamoto hizo za afya mazingira nk ila hayo yoote ni ili ukuu wa Mungu uwe.
 
Dah inatia huruma na simanzi ..pole yao sana . I can feel pain za hao wazazi. 😓😓😓 twins dah!. My prayers to them.
Asante 🙏 (on their behalf)
Kwakuwa umesema tunaomuamini Mungu. Tunaamini pia hapa duniani sio mbinguni/peponi. Na Kama kungekuwa hakuna hatari, ugonjwa, kifo au maumivu kabisa, dunia ingekuwa peponi.
Sawa
kwahiyo hayo mambo yako kutukumbusha kuwa kuna sehem hayo mambo hayatakuwepo. Na ndio inaweka tofauti.
Watoto ni Malaika. Tutawakuta mbinguni.
Kwahiyo hawa watoto wanaumbwa, wanazaliwa na kuteseka au kufia tumboni ili kuwa ishara ya kuwakumbusha nyie mlio hai na wazima kwamba kuna mbingu?
Hitimisho ni kuwa tunateseka kwa sababu hii dunia sio pepo. Kuna kila aina ya mateso, dhiki na tabu.
So mafunzo kwenu ndiyo yanajustify mateso kwa wengine wasio na hatia? Mungu wenu hakuona namna nyingine yoyote ya kuwakumbusha nyinyi kuhusu maisha yajayo huko peponi bila kutesa wale wasio na hatia?

Was this the best design or solution he/she could come up with?
 
RC tunaambiwa kuna dhambi ya asili.. tuliyorithi kwa kina Adam na Eva. So watoto wanazaliwa nayo.. ndio maana tunabatizwa… kwa wengine sijui.. so kikombe hakiepukiki
Nimekuelewa.
Nadhan Kubatizwa hakufuti dhambi.
Ila ni kujitambulisha kuwa ww ni wa nani.

Nakumbuka pia Imeandikwa kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe.

Hapa umeongelea Dini.
Ila AYnay anaunganisha iman hizi na kanuni na mambo ya rohoni.
Je ni sayansi au nn?
 
Mwenyezi Mungu atasalia kuwa Mungu milelena milele haidhuru ni hali gani ikutayo mwanadamu .

Kwanza mwanadamu ni kiumbe mdogo sana katika viumbe wa ulimwengu ni vile tu amejipa umuhimu kuliko vyote.

Mwenyezi Mungu ni mkamilifu na mwanadamu na viumbe vingine vyote ni dhaifu, udhaifu wetu ni pamoja na changamoto hizo za afya mazingira nk ila hayo yoote ni ili ukuu wa Mungu uwe.
Umemaliza kila kitu!
 
So mafunzo kwenu ndiyo yanajustify mateso kwa wengine wasio na hatia? Mungu wenu hakuona namna nyingine yoyote ya kuwakumbusha nyinyi kuhusu maisha yajayo huko peponi bila kutesa wale wasio na hatia?

Was this the best design or solution he/she could come up with

For sure. Almight Planed and designed cannot be judged.
 
Back
Top Bottom