Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Wananchi wa kata ya Ifumbo wilayani Chunya wameripotiwa kuugua ugonjwa usiofamika ambao mtu akiugua anatapika damu mpaka anapoteza maisha, na mpaka sasa tayari watu zaidi ya 15 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 50 wanaendelea kuugua, hali ambayo imesababisha halmashauri hiyo kuomba msaada wa kitaalam katika ngazi za juu ili kuubaini na hatimaye kupata tiba yake.
Taarifa ya kuwepo kwa ugonjwa huo usiofahamika imeibuliwa na diwani wa kata ya Ifumbo Mhe.Weston Mpyila mbele ya kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Chunya huku akiomba msaada wa kuwanusuru wananchi wake.
Mganga mkuu wa wilaya ya Chunya, Dk.Felister Kisandu amethibitisha kuwepo kwa ugonjwa huo ambao wameshindwa kuutambua na kudai kuwa ofisi yake imeomba msaada katika ngazi za juu ili wasaidiwe kuutambua na kukabiliana nao.
Chanzo: ITV
---
KANUSHO: Serikali kupitia Wizara ya Afya imekanusha taarifa za mlipuko wa ugonjwa huo. Zaidi soma Serikali yakanusha kuwepo mlipuko wa Ugonjwa wowote kata ya Ifumbo, Mbeya. Wizara ya Afya kuichukulia hatua ITV