Watu zaidi ya 50 wanusurika kifo katika ajali basi la Abood

Watu zaidi ya 50 wanusurika kifo katika ajali basi la Abood

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,741
Reaction score
25,681
Watu zaidi ya 50 wamenusurika kifo baada ya basi la Abood (T 266 DBV) walilokuwa wakisafiria kutoka Morogoro kwenda Dar es salaam kupinduka mara mbili katika eneo la Ruvu wilayani Kibaha.

Baadhi ya abiria walionusurika katika ajali hiyo wameiambia TBC kwamba ajali hiyo imetokea majira ya saa moja asubuhi wakati dereva wa basi hilo akipita lori lililokuwa mbele yake bila tahadhari na kukutana na gari lingine na alipojaribu kulikwepa basi hilo likayumba na kumzidi nguvu na kupinduka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema idadi kamili ya watu waliojeruhiwa zaidi ni wawili.

Kamanda Wankyo amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe uliosababishwa na dareva basi hilo ambaye alikuwa akikimbizana na mabasi mengine mawili ya kampuni hiyo yote yakitokea Morogoro kuelekea Dar es Salaam.

Kufutia ajali hiyo kamanda hiyo ameligiza jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kuwatafuta na kuwakamata mara moja madereva wa mabasi hayo.

©TBC
 
Source ya hii habari Ni TBC? mh siamini. Inaweza kweli Hilo gari limeanguka lakini sio sehemu hiyo au siku husika au sio Basi la Aboud.
 
Uhai wa mtu hauna uhusiano na siasa imagine wewe upo ndani ya hilo basi au mama yako,baba yako au mkeo na wanao au ndugu zako.
Je Ungethubutu kuingiza siasa?

Waafrika sio binadamu sababu binadamu ana akili na utu pia sio mjinga.

Mzungu na mabaya yake yote sidhani kama angeingizia siasa kwenye maisha ya watu.

Nilikuwa sahihi kuandika wengi wa waafrika wamedumaa ufahamu na nazidi kuprove hilo kila sehemu.
 
Tulia wewe dawa ikuingie vizuri. Uhai wa mtu hauna uhusiano na siasa??? Unasahau mapema sana ehh? Kule Pemba watu hawakuumizwa kwa sababu ya siasa chafu? Wewe katika akili yako unaamini CCM inaweza kushinda Pemba viti vyote? Sie wapemba twajua. Ninyi wengine myasikie tu.
 
Basi limepata ajali kwenye sehemu inaitwa bonde la mpunga, karibu na hiyo sehemu pana kiwanda cha kutengeneza mifuko, pia kwa mbele kidogo kuna kituo cha Polisi kama unakuja Mlandzi na kama unaenda pale njia ya kwenda Ruvu jkt club huwa pana Maaskari wa barabarani wa kutosha.
Sasa nimeamini maana Kipangaspecial is a credible source.
 
Tulia wewe dawa ikuingie vizuri. Uhai wa mtu hauna uhusiano na siasa??? Unasahau mapema sana ehh? Kule Pemba watu hawakuumizwa kwa sababu ya siasa chafu? Wewe katika akili yako unaamini CCM inaweza kushinda Pemba viti vyote? Sie wapemba twajua. Ninyi wengine myasikie tu.
Mkuu jaribu kuwa na akili.
Siasa za africa ni sawasawa na ujinga.

Pia mimi sina chama cha siasa.

Unadhani sababu gani itakayo nifanya niwe na ushabiki na chama cha siasa.
 
Ni ujinga kusema huna chama cha siasa wakati machungu ya maamuzi mabovu ya wanasiasa yanawachapa wote bila kuangalia sura wala rangi
Unafikiri ukiwa na chama cha siasa kuna chochote unaweza ukafanya ili kuondoa machungu na maamuzi mabovu ya wanasiasa?
Ukiondoa matusi dharau na kejeli kuna chochote unaweza ukafanya ili kuondoa hayo machungu?

Well mimi jibu ninalo "Hakuna"
Then why kuwa na chama cha siasa?
Ukiondoa kupoteza muda na kujiondolea heshima au kujidharirisha.

Now unapata definition ya ujinga ndani ya kuwa na chama cha siasa.

Badala yake kutumia huo muda wa kushabikia siasa kuondoa hayo machungu.

Serikali/Wanasiasa kamwe haitoweza kubadirisha maisha ya mtu yoyote bila hao watu kujitambua.
 
Back
Top Bottom