A
Anonymous
Guest
Watumishi wa ajira mpya wa kada ya afya katika Halmashauri ya Mkalama wamepewa fedha za kujikimu, lakini sisi walimu wa ajira mpya hadi sasa hatujapokea hata shilingi moja.
Hali hii inakatisha tamaa na inazua maswali kuhusu usawa katika kuwahudumia watumishi wa umma.
Tunaomba mamlaka husika zitupatie ufafanuzi na kuhakikisha kunakuwa na usawa katika utekelezaji wa stahiki za watumishi wote. Tunaamini kila mtumishi anastahili kutendewa haki bila ubaguzi.

Wiki chache zilizopita kupitia Fichua Uovu hapa JF tuliwasilisha hoja kuwa sisi Watumishi wa Ajira Mpya Kada ya Afya katika Manispaa ya Singida Mjini Mkoani Singida tiilipewa nusu ya malipo ya Fedha za Kujikimu.
Tunashukuru Uongozi umesikia kilio chetu na tumepokea hela ya kujikimu, asanteni JF kwa kutupambania.
Hoja ya awali ~ Ajira Mpya (Kada ya Afya) Singida Mjini na Mkalama tumepewa nusu Fedha ya Kujikimu, wanasema Serikali haina fedha