KERO Watumishi wa Halmshauri ya Wilaya ya Chemba bado hatujalipwa fedha za kujikimu na hakuna majibu kamili

KERO Watumishi wa Halmshauri ya Wilaya ya Chemba bado hatujalipwa fedha za kujikimu na hakuna majibu kamili

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari, hali ya kutolipwa au kucheleweshewa malipo imekuwa kama desturi kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, Dodoma.

Hakuna hatua zinazoonekana kuchukuliwa kuhakikisha tunalipwa fedha zetu kwa wakati, licha ya kuwa tunatumia fedha zetu wenyewe kujikimu na kutekeleza majukumu yetu.

Mbali na kucheleweshwa kwa malipo, hata yanapofanyika, hulipwa kwa kiasi kidogo sana ambacho hakifiki hata nusu ya fedha tunazostahili kupata.

Tunaomba mtusaidie kupaza sauti zetu ili mamlaka husika zichukue hatua na kuhakikisha tunalipwa stahiki zetu kwa wakati na kwa ukamilifu.
 
Back
Top Bottom