Watumishi wa serikali mliwezaje kutoboa, mbona mimi naenda kushindwa

Watumishi wa serikali mliwezaje kutoboa, mbona mimi naenda kushindwa

Mkuu kwa huo mshahara wako upangie bajeti. Ningekushauri tumia formula hii ya 50/30/10/10 au 50/20/20/10

Hakikisha unakua na akiba.
 

Attachments

  • images (2).jpeg
    images (2).jpeg
    36.4 KB · Views: 28
  • images (4).jpeg
    images (4).jpeg
    34.8 KB · Views: 31
Kama mnaelewana vizuri na mkeo basis tafuta amani katika maisha yenu.Na amani huja kwa kumtambua Mungu ndiye mleta amani.Toa zaka wapende jirani nk.Fedha hazileti amani kama huna Mungu,hata kama utapewa 2m kama mshahara kwa mwezi.Lakini haya yanataka moyo wake uelewe na kuamua.
 
Kuna ndugu yangu mume wake alipoteza kazi ikawa kila mara ni simu mara hiki mara kile. Nikamnunulia unga wa ngano kg 25 na mafuta ya kupikia alizeti lita 20 nikampa na hela kidogo ya mkaa na sukari etc. Nikamwambia aongee na wenye maduka awe anapeleka maandazi na awe pia anawaungisha hao wenye maduka kwa kununua unga na vitu vya biashara yake kwao. Alifanya kama nilivyomuelekeza na akawa anapata hata faida ya 20k kwa siku na hapo nyumbani hawafi njaa mana mama anauza mandazi watoto wanapata vitafunwa maisha yakaenda.

Huyo wife wako mkubaliane afanye biashara yeyote hata kama ni kuchoma mahindi asikae tu nyumbani.

Na hiyo faida anayoipata ndio iwe ya matumizi ya nyumbani na matumizi yake binafsi.

Wewe fanya shopping ya vitu vya ndani tu kwa mwezi matumizi mengine mwachie wife. Kama wife msumbufu mpeleke kwao kwanza akapumzike akirudi akili itakuwa imekaa sawa
 
Weka lengo la kutonunua chakula. Ule cha kujilimia( maharage, mahindi, kunde, njegere nk). Kila mkoa kuna mazao yanastawi.
Lima hata nusu heka ya kula familia yako tu. Lima viazi vitamu hata robo heka.
Panda mboga mboga hapo nyumbani
Panga nyumba yenye space( pembezon mwa mji).
Futa tatizo la kununua nyama kwa kuanza kufuga kuku 5 tu, sungura 3.
Kuku 5 ndani ya miezi 6 utakuwanzo 40, hawa totally kienyeji utawasapoti chanjo tu na dawa za mafua hasa msimu huu wa mvua.
Hili ni zoezi analoweza fanya mkeo kama hana kazi.
Baada ya mwaka 1 utakuwa hununui tena vyakula vya kila siku labda mchele, mafuta ya kula no.
Huwezi hayo anzisha biashara ndogo ndogo hata kuuza nyama choma, au. Chips eu juisi nk. Usiwajali unaofanya nao kazi hawatakupa hela, wafanye kuwa wateja wako.
Learn other skills kama ufundi mdogo mdogo kama simu, tv, computer, kukarabati viatu , ushoni wa nguo nk.
Anzisha genge la kuuza nafaka, mkaa na matunda.
Huwezi jifunze udalali, kuuza mitumba nk.
Hizo ndizo dili za watanzania wengi kipenzi cha Mama Samia.
Hapo ndio kwanza picha linaanza usiombe mzazi/ mke/ mtoto aje apate gonjwa la ajab utajuta.
 
Mpe mke wako mtaji wa biashara hata kama ni genge asikae home tu. Mkubaliane kabisa kwa mwezi na yeye awe anatoa yani mnaweka vipato vyenu juu ya meza mnafanya bajeti pamoja. Mara nyingi wanawake wasiojua kutafuta pesa wanakuwa na matumizi mbaya ya pesa. Mpe jukumu la yeye kutafuta pesa ndio atajua uchungu wa kupata pesa na ataweka bajeti yake vizuri.
 
Habari za jioni.

Nimeshindwa kupata usingizi kutokana na wimbi la mawazo.

Wakuu Take home yangu 613K Mimi ajira mpya mwaka jana ila nimekuwa na wimbi la mawazo na kuona kama sitaweza kutoboa labda nIpate washauri wengine wa maisha labda.

Nnafanya kazi mkoani,ila kadri siku zinavyoenda ninaona maisha magumu ilhali Mimi ni ajira mpya tu wa mwaka jana.

Nina mahitaji ya lazima mengi sana Nina familia ya mke na mtoto mmoja na ndugu wananitegemea.

Kila mwezi lazima.
Nitume nyumbani laki 1.
Nanunua chakula laki 150K.
Nampa mke wangu 150K ya matumizi na bills nyingine.
Kodi nimepanga chumba sebule 100K.
Sijaweka dharura Wala other charges.

Huu ni mwezi wa sita kazini sijanunua shati Wala Chochote juu ya familia yangu. Nimekuwa mtu wa mawazo na ninayeona nakuwa maskini kabisa.

Kazi yangu Ina posho ila ofisini wanatudhulumu tu hivyo hatuna Constant.

Jamani wazoefu naombeni mnishauri kama naona naenda kufeli mapema jamani.

Wengine mmewezaje?
Kama upo mkoani na upo mwenyewe tafuta chumba kimoja na Kodi iwe 30,000/=kushuka.
Kama wife yupo mbali na wewe na Hana shughuli ya kufanya I mean na yeye hajaajiriwa yupo tu home mwite mje mjae wote. Ila akija ndo utapanga vyumba Viwili standard na Kodi isiwe kubwa zaidi ya 80k, mkiwa sehemu Moja gharama za maisha hupungua, Sasa wewe uko uliko umepanga, wife nae umempangia nyumba,huoni hapo cost ni kubwa, Bado maji, umeme usafi nk. Hata Mimi nipo mkoani vyumba Bei ni 50k ila nilitafuta Cha 30k, familia IPO dar ,ila dar nimejenga. Wazazi ukiwaendekeza watakurudisha nyuma hautasogea other wise labda wanaumwa, Tena ukiwa unawatumia hivyo 100k wanajua unapata pesa nyingi tu,kumbe unajibana sana. Mimi nisingekuwa nimeshahenga dar ningehama na family sema na watoto shule walishaanza kwahiyo kuhamasisha familia Kuna mchakato kidogo.
 
Habari za jioni.

Nimeshindwa kupata usingizi kutokana na wimbi la mawazo.

Wakuu Take home yangu 613K Mimi ajira mpya mwaka jana ila nimekuwa na wimbi la mawazo na kuona kama sitaweza kutoboa labda nIpate washauri wengine wa maisha labda.

Nnafanya kazi mkoani,ila kadri siku zinavyoenda ninaona maisha magumu ilhali Mimi ni ajira mpya tu wa mwaka jana.

Nina mahitaji ya lazima mengi sana Nina familia ya mke na mtoto mmoja na ndugu wananitegemea.

Kila mwezi lazima.
Nitume nyumbani laki 1.
Nanunua chakula laki 150K.
Nampa mke wangu 150K ya matumizi na bills nyingine.
Kodi nimepanga chumba sebule 100K.
Sijaweka dharura Wala other charges.

Huu ni mwezi wa sita kazini sijanunua shati Wala Chochote juu ya familia yangu. Nimekuwa mtu wa mawazo na ninayeona nakuwa maskini kabisa.

Kazi yangu Ina posho ila ofisini wanatudhulumu tu hivyo hatuna Constant.

Jamani wazoefu naombeni mnishauri kama naona naenda kufeli mapema jamani.

Wengine mmewezaje?
Unaishi maisha ya kufurahisha watu au kutaka kuonekana na watu kuwa ni wa status flani na hapo ndipo tatizo lilipoanzia.
Kwa mshahara wa laki sita matumizi yako hayapaswi kuwa zaidi ya laki nne kwa mwezi.
Una Mke na mtoto mmoja halafu unakaa nyumba ya kodi ya laki moja kweli, kwa kukadiria tu ni kama umeamua kuchukua nyumba kubwa sana ambayo kwa haraka haraka tu nayo inachangia kuongeza gharama za maisha yako.
Panga nyumba hata ya elfu 40/50 ujipange utafute kiwanja chako hata upate chumba kimoja tu.
Unatuma kwenu laki kila mwezi wewe ukiwa kama nani hapo kwenu? Kabla ya wewe kuajiriwa hiyo laki alikuwa anawatumia nani?
 
Hili swala la mishahara nadhani liangaliwe upya maana gharama za maisha zinapanda kwa kasi mno
 
Mali bila daftari huisha bila habari…!

Fanya hiviiiii

Bajeti ya Mwezi – Tsh 500,000​

1. Chakula – Tsh 180,000​

  • Vyakula vya msingi (unga, mchele, maharage, sukari, mafuta)
  • Mboga za kila siku
  • Vyakula vya protini kwa kiasi (mayai, dagaa, maziwa)
  • Nafaka, mikate, matunda kwa wiki mara 1–2

2. Kodi ya Nyumba – Tsh 100,000​

  • Chumba & sebule ya kawaida au nyumba ya kupanga ya gharama ya kati

3. Mengineyo – Tsh 100,000​

  • Umeme & maji – 25,000
  • Usafiri wa kila siku – 30,000
  • Vocha/internet – 15,000
  • Usafi wa nyumba, sabuni, dawa ndogo ndogo – 30,000

4. Akiba – Tsh 120,000​

  • Kuwekwa benki, vikoba au kwa dharura
  • Inaweza kuendeleza mipango kama biashara ndogo au elimu

Hii nzuri kaka nakutafuta soon
 
Asante kaka je Kodi ya 100K Kwa huo mshahara ni sahihi maana Niko town niliwaza nipunguze nitafute hata nyumba hata ya ovyo ya 40 Kodi ili nipate muda wa kuutuliza kichwa
Mkuu, 613k take home unalia hivi? Nilianza kazi na take home ya 400k, nikamfungulia wife kitu kwa mkopo, wife akawa sasa ananisevu hivyo kutokana na kukopa take home yangu ikawa 180k. Nilikuwa nasomesha mtoto shule private lakini nilimudu. Kodi ya nyumba ninalipa 100k pia, bado kodi ya biashara lakini kila mwezi lazima niweke 50k kama akiba ambayo naiona mwisho wa mwaka tu. Kwa Sasa, take home yangu ni 250k. Wife nimempanulia mtaji ili asimamie vizuri kwa sababu muda mwingi kama mtumoshi naupoteza kazini hivyo kukaa na pesa nyingi wakati sina muda wa kuizalisha naona ni kukaribisha umasikini.

USHAURI:
Mwamini mkeo, mtafutie kitu afanye na uhakikishe kimefanikiwa na umsaidie baada ya muda wa kazi asimamie. Kama zipu ipo wazi, funga kwanza ufanikiwe. Kuhusu ndugu, jifanye ni yatima. Kupata kazi haimaanishi uanze kubeba majukumu ya wazazi kuanza kusomesha ndugu au kutoa misaada ya mara kwa mara. Jaribu ku-isolate maisha yako, uwe kama vile upo peke yako na familia yako dunia hii.
 
Mali bila daftari huisha bila habari…!

Fanya hiviiiii

Bajeti ya Mwezi – Tsh 500,000​

1. Chakula – Tsh 180,000​

  • Vyakula vya msingi (unga, mchele, maharage, sukari, mafuta)
  • Mboga za kila siku
  • Vyakula vya protini kwa kiasi (mayai, dagaa, maziwa)
  • Nafaka, mikate, matunda kwa wiki mara 1–2

2. Kodi ya Nyumba – Tsh 100,000​

  • Chumba & sebule ya kawaida au nyumba ya kupanga ya gharama ya kati

3. Mengineyo – Tsh 100,000​

  • Umeme & maji – 25,000
  • Usafiri wa kila siku – 30,000
  • Vocha/internet – 15,000
  • Usafi wa nyumba, sabuni, dawa ndogo ndogo – 30,000

4. Akiba – Tsh 120,000​

  • Kuwekwa benki, vikoba au kwa dharura
  • Inaweza kuendeleza mipango kama biashara ndogo au elimu

Hii nzuri sana
 
Usilalamike tafuta solution Average people watakwambia save mimi ntakwambia tafuta other sources za income itz never too late mimi net yangu baada ya deductions zote (mikopo included) ni chini ya 500k lakini ili famili yangu iende kwa mwezi naahitaji 1.5 M inawezekanaje? Nina multiple incomes i make money any where any time iwe kwa jeans au kwa Tai, kwa kifupi mimi ni Hustler Dont complain Be one
 
Kupitia huu Uzi nimegundua asilimia kubwa ya waajiriwa wa serikali Wana roho mbaya alafu wanaishi kwenye lindi la umaskini.

Kuna kaka yangu ni Mwalimu ngazi ya degree Yuko kazini huu unaenda mwaka wa 20 juzi tu nimetoka kugombana naye na nimeapa sitamtafuta Tena na yeye Wala asinitafite sababu kubwa ni kwamba Kila likitokea tatizo nyumbn ukimwambia tuchangishane kama familia tu solve tatizo jamaa hatumii hata sent Tano ukimpigia yeye Kila saa "Niko kwenye kikao" yaani hata usiku Yuko kwenye kikao tu na kibaya zaidi hana maendeleo yyte useme labda hizo pesa zake Kuna kitu cha maana anafanyia.
 
Back
Top Bottom