Watumishi wa serikali mliwezaje kutoboa, mbona mimi naenda kushindwa

Watumishi wa serikali mliwezaje kutoboa, mbona mimi naenda kushindwa

Unalipa kodi 150K
unanunua chakula 150K
na wife 150K ya nini tena 😀,
  1. mpe angalau 35K asuke ,
  2. 20K anunue mafuta na mambo ya kike nk. ,
  3. 50K ya mambo ya mboga mboga au kodi ya meza si chakula kipo tayari!
Save 50K toka kwa pesa unayompa wife
Nyumbani unawatumia 100K ,basi wapunguzie anza kuwapa 50K endelea kupunguza kila upatapo nafasi huku ukiwajengea uwezo wajisimamie..

Kwa mwezi utakuwa unasave 50K pesa uliokuwa unamwachia wife,na 50K unayotuma maskani !!
Jumla 100K , pia angalia jinsi ya kujiongeza
 
Mali bila daftari huisha bila habari…!

Fanya hiviiiii

Bajeti ya Mwezi – Tsh 500,000​

1. Chakula – Tsh 180,000​

  • Vyakula vya msingi (unga, mchele, maharage, sukari, mafuta)
  • Mboga za kila siku
  • Vyakula vya protini kwa kiasi (mayai, dagaa, maziwa)
  • Nafaka, mikate, matunda kwa wiki mara 1–2

2. Kodi ya Nyumba – Tsh 100,000​

  • Chumba & sebule ya kawaida au nyumba ya kupanga ya gharama ya kati

3. Mengineyo – Tsh 100,000​

  • Umeme & maji – 25,000
  • Usafiri wa kila siku – 30,000
  • Vocha/internet – 15,000
  • Usafi wa nyumba, sabuni, dawa ndogo ndogo – 30,000

4. Akiba – Tsh 120,000​

  • Kuwekwa benki, vikoba au kwa dharura
  • Inaweza kuendeleza mipango kama biashara ndogo au elimu

 
Wenzako wanapata huo mshahara kiduchu na wanaongeza nyingine nyingi zaidi wanazochangiwa na wananchi. Mpaka wananchi wakuchangie ujue njia ya kufungua mianya.
 
Huko kwenu ni wagonjwa hizo laki moja moja had lini na unajitafuta
Mm nimeanza na mshahara mdogo kuliko huo wako ila mzaziwangu ni mzima ana afya

Nikaongea nae hali ya Maisha na nikamtafutia Cha kufanya nilikuwa na friji nikampa na mtaji laki moja tu akapata katoni kma 20 za juis na maji Brenda akaanza kukuza juis mwenyew ikanipunguzia majukumu ya mara chumvi mara sukari baadae akashindwa akaomba mtaji wa biashara ya chakula now akaongeza na juis zake sihangaiki kabisa na hana time na mia mia zangu na baraka juu

Kama ni kijijini washaurinwatafute shamba walime mazao ya biashara sàidia kuhudumua hayo mashamba ikipatikana pesa bas angalia namna ya wao kuweza kusimama hata kwa mahitaji madogo ya buku buku kwako ibaki dharura na ugonjwa my dear usipokuwa na akili ya kujiongeza hutoboi
Kama nimekukwaza sàmahani
wanawake ndio hawa Sasa, hongera kwa mawazo na hatua nzuri.
 
Kwahiyo mnawapa laki 3 Kwa mwezi
Sasa kaeni nyie watatu ongeeni muulíze mzee anaweza kufanya nn Cha mtaji mdogo Mpe idea hata genge na matunda hapo hapo nyumbni Kisha mpeni mtaji then tulieni muangalie mwambieni halinhalis ya maisha muwe mnamsapot pocket money za kawaida km mzazi Kwa muda huu mkiwa matajiri mtaendelea na utaratibu wenu km mzazi muelewa ataelewa
Asante madame ushauri wako unajenga ubarikiwe.
 
Lakin 6 ni ndogo mtu ukiwa na familia. Yaani mm nachukua hiyo hiyo lakini maisha yanakimbiza mpaka sasa sina hata saving shilingi 10.
Utamlaumu tu wife anamatumizi mabaya ila hiyo pesa ni ndogo. Kikubwa tafuta njia mbadala ya kuongeza kipato
Una familia Mzee wangu?
 
Ni ngumu kushindwa kumaintain kidogo ukatarajia kikubwa ndio kikuendeshee maisha muhimu weka tu vipaumbele ni ngumu lakin unaweza kujaribu hata 50 Kwa mwez matumizi yasiyo ya lazima unaepuka tumia exprience hata za wanaoish Kwa mishahara ya laki 3 wanasurvivr vipi hata Kwa muda Ili upate mtaji uanze njia mpya
Asante mkuu
 
Pesa unayo muachia nyumbani mkeo ni kubwa kwa kipato chako duni punguza. Anza kumpa 60% ya hiyo mwambie kazini kuna shida imejitokeza unakatwa mshahara kiasi fulani.
Unapotafuta mtaji au uweze kutunza akiba zingatia yafuatayo:-
  1. Siyo lazima kila siku kula wali.
  2. Siyo lazima kula kitoweo kizuri kila siku.
  3. Usipange nyumba nzima kama familia yako ndogo.
  4. Panga sehemu yenye gharama ndogo ili mradi iwe na usalama. Hama hapo unapoishi sasa.
  5. Ukiweza lima bustani ya mboga mboga hata kwenye makopo.
  6. Zingatia matumizi ya gesi na mkaa visitumike ovyo. Tumia mtungi mdogo wa gesi na usinunue mara mbili ndani ya mwezi mmoja kwa familia ya mke na mtoto mmoja kama unanunua na mkaa. Usipike vitu vigumu kwenye gesi mfano maharagwe.
  7. Mkeo asijifanye ana roho nzuri na kugawa vitu kwa jirani.
  8. Mkeo aweke kibubu (pig bank) cha familia siyo Cha fedha ya kutuma kwao au kujenga kwao.
  9. Mkeo na wewe mwenyewe msishindane na mtu kwenye mavazi, manukato na urembo.
  10. Punguzeni matumizi ya gharama za simu au internet bundles.
  11. Zingatieni matumizi mazuri ya umeme na maji ya kulipia. Vitu vikishika baridi Zima jokofu(refrigerator), asikeshe anaangalia TV, usitumie jiko la umeme kwa sasa au tumia la umeme usitumie mkaa wala gesi.
  12. Mtoto mdogo asishinde amevalishwa diapers (Pampers) kutwa nzima ni gharama na mbaya kwa afya.
  13. Usitumie sigara
  14. Usinywe pombe au ukishindwa kujizuia kunywa mara chache kwa mwezi. Pia usijigeuze tajiri kununulia wengine Pombe.
  15. Usipeleke pesa nyingi kanisani au msikitini.
  16. Usicheze kamari au michezo ya kubahatisha Kamwe.
Don't spend above your average means.
Asante boss mawazo mazuri sana mkuu nimeyapokea
 
Back
Top Bottom