Watumishi wa serikali mliwezaje kutoboa, mbona mimi naenda kushindwa

Daahh poleee aiseee me nlianza kazi kipindi hchohcho ww umeanza na Ela nayopata ni km yako ila saving yangu now ni 2.1m ila ninaishi kiroho ngumu sanaaaaaaaaaa..
unajibana afu ukifa wafaidika wengine
 
ww uutakua mkongwe kwenye salary slip, amini kwamba.
 
Na hii ndio ideas yangu.

Ila kichwa kinawaka moto mshahara haukai maana Kila siku mshahara unaishia kwenye chakula tu na expensive nyingine Nina kitanda na godoro pekee mpaka Sasa
kwani ulioa kabla haujapata kazi
 
Jipage vizuri kwani hayo matumizi yako bado hayana uhalisia wa maisha kutokana na kipato, kwa sababu zifuatazo:-
1. Unaishi kwa cash bajet kitu ambacho ni hatari sana ukizingatioa uko mkoani
2. Unawazoesha nyumbani kuwa tegemezi badala ya kujitegemea
3. umeanzia maisha ya juu kwenye kupanga nyumba ukilinganisha na kipato chako
5. Wife unamzoesha vibaya mtoto mmoja matumiz ya 5k kila siku hayo maisha yatakuja kuwaponza.
USHAURI:
1. Jishughulishe na kilimo, ufugaji mfano kuku wa kienyeji, n.k
2. Nyumbani wajitegemee kwani kabla ya wewe kupata kazi walikuwa wanaishije? pia wasaidie panapokuwa na tatizo kubwa mfano ugonjwa hadi utakapokuwa vizuri kiuchumi
3. Tafuta nyumba ambayo kodi haizidi 50k per month
4. Mzoeshe wife kubana matumizi na kujiongeza kwenye biashara ndogondogo.
Wengine wenye uzoefu wataongezea.
 
uko sahihi mkuu.
 
UMENENA MKUU
 
Titicomb, asipotoboa kwa haya uliyoweka hapa, hatoboi milele. Mkewe atafute mifuko minne ya cement iliyotumika. Aijaze udongo na badala ya kupanda maua apande veggies. Chinese, swiss chard, mchicha nk.
Awe na kawaida ya kununua vifaranga 10 vya KUKU Kila mwanzo wa mwezi na atenge 30k ya kuwalishia. Atakula KUKU 2 Kila wiki. Akibana atakula KUKU mara 4 Kila wiki. Life isn't that tough, shida malezi, jamii inayotuzunguka, elimu tuliyofundishwa shuleni nk vyote vinatufanya tusiwe problem solvers. Na Hilo linatugharimu.
 
Mkuu Asante, una lugha Kali lakini yenye ujumbe ndani yake. Hasa hapo kwenye matumizi ya friji. Chemcha kwa wingi kusave fuel Kisha inakuwa ni kuunga tu.
 
Umeongea mambo mazuri sana.
 
600k mtu analipwa kwa mwezi! Hizo kazi samtaimu.. bakini nazo tuu kazi zenu mazee. 😁
Wewe ni WA muda mrefu humu pia ni mtanzania nashangaa kuona unashangaa hali hii ktk jamii zetu.
No offense intended ila mnatudharau tusiofanikiwa kiuchumi au tulioajiriwa ktk kazi za mishahara midogo. Mi naona unamkatisha tamaa huyu jamaa. Kazi yenyewe amesema kaitafuta muda mrefu hawezi kuiacha ila anaomba mbinu za kufanikiwa kupitia mshahara anaoupata.
 
Kuishi nje ya ukweli hiyo mkuu labda ungechanganua iyo 150 kwa wife bila dharura ina tekete vp itakua rahisi kushauriana mkuu... pia chakula na bills za 150 kwa mwezi mkuu serious? Kuna mahali hakupo sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…