Mr independent
New Member
- Dec 24, 2020
- 4
- 3
01. Hakuna pesa nyingi siku zote.Habari za jioni.
Nimeshindwa kupata usingizi kutokana na wimbi la mawazo.
Wakuu Take home yangu 613K Mimi ajira mpya mwaka jana ila nimekuwa na wimbi la mawazo na kuona kama sitaweza kutoboa labda nIpate washauri wengine wa maisha labda.
Nnafanya kazi mkoani,ila kadri siku zinavyoenda ninaona maisha magumu ilhali Mimi ni ajira mpya tu wa mwaka jana.
Nina mahitaji ya lazima mengi sana Nina familia ya mke na mtoto mmoja na ndugu wananitegemea.
Kila mwezi lazima.
Nitume nyumbani laki 1.
Nanunua chakula laki 150K.
Nampa mke wangu 150K ya matumizi na bills nyingine.
Kodi nimepanga chumba sebule 100K.
Sijaweka dharura Wala other charges.
Huu ni mwezi wa sita kazini sijanunua shati Wala Chochote juu ya familia yangu. Nimekuwa mtu wa mawazo na ninayeona nakuwa maskini kabisa.
Kazi yangu Ina posho ila ofisini wanatudhulumu tu hivyo hatuna Constant.
Jamani wazoefu naombeni mnishauri kama naona naenda kufeli mapema jamani.
Wengine mmewezaje?
02. Kwa hiyo bajeti uliyonayo hata ukianza kupokea zaidi ya milion 2 bado hela haitatosha kwani naamini utaiongeza tena.
03. Kaa na mke wako tena muambizane kwa pamoja kuwa ninyi ni masikini na msijizime data.
04. Hiyo bajeti yenu mmeipanga kutokana na mkumbo usiowahusu kwa sababu zifuarazo.
4A. Unaishi kijijini una mke wako na mtoto mmoja, kuna ulazima gani wa kupanga nyumba ya 100k kwa mwezi wakati mshahara ni 613k na unataka kufanikiwa?
4B. Nyumbani kila mwezi unatuma 100K, je wanauguza, kuna mtu anaumwa, hawana uwezo wa kupata chakula? Kama haya maswali ni ndiyo basi endelea kuwatumia (Wazazi wetu ni muhimu). Kama jibu ni hapana, nakushauri acha hiyo tabia badala yake watumie pale una nafasi ya kutuma chochote au pale kuna sharura imetokea.
4C.Bro mwambie mke wako asiridhike na hiyo ajira uliyoipata, nimeshangaa sana eti mkeo unampa 150K harafu inaisha kabla ya siku na bado anakasirika na wakati anajua unachopokea ni kidogo.(Mungu awasaidie muwe wamoja kwa mipango yenu).
NAKUSHAURI RAFIKI YANGU:
1. Tafuta nyumba yenye kodi angalau isizidi 60,000 kwa mwezi inaweza kuwa ngumu lakini mkikubali inawezekana na mtazoea tuu.
2.Nyumbani waelezee hali yako na malengo yako wakuelewe, then watumie hela pale wanapohitaji au pale una nafasi nzuri.
3. Achana na bajeti ya kukabizi 150k kwa mwezi eti kwa ajili ya chakula. Hapa ikiwezekana hela ya chakula itoke kutokana na kile mtakula siku husika, au mpatie mkeo hela ya chakula kwa kila siku na si lazima iwe 5000/= kila siku. Siku zingine iwe chini ya hapo au hamna kabisa kwa kupika mboga zinazoweza kutumika kwa siku mbili.
4. Kama mke wako anaweza mambo ya biashara basi jibaneni mpate ka mtaji na aanze kufanya.
5. Malengo yako yaanze saizi kwa kuanza na ulichonacho.
NB. mimi nmeishi kwa mshahara wa 443k kwa mwezi kwa miaka minne na nilikuwa jijini na mwisho wa siku niliweza kujibana na kujenga nyumba na kuondoka kwenye ulipaji wa kodi.