Watumishi wa serikali mliwezaje kutoboa, mbona mimi naenda kushindwa

Watumishi wa serikali mliwezaje kutoboa, mbona mimi naenda kushindwa

Sibeti kaka.
Mshahara ukitoka.

1.CHAKULA.
Michele 2200×20=44000
Sukari kilo 5 ×3000=15000
Mafuta lita 5 =30K
Unga =15K
Gas 25K
Tambi 8000
Maji 5000
Umeme 1000
Maahrage 15K
Waifu Nampa 30 ya kusuka
Dogo pampas 5K per week

Na hapo ninamwachia waifu 150K Kwa kigezo Cha kununua nyama ,au samaki sabuni Kwa ajiri ya kubadilisha mbona Kwa maana elfu 5 Kwa siku na huyu ananiambia eti haitoshi Sasa ni kweli kabisa issue kama hii.

Kodi ndo nalipa laki 1.



Umeona hiyo bajeti mkuu
Haitoshi elf5 Kwa siku na mko 3? 😳🤔mnakuka nn wenzetu? Ikiwa Bado mnajitafuta?
Mke,mume na mtt? Heee huyo ni mke? Anakukomoa?
Bado unampa 30 ya kusuka Kila mwezi?

Muongo
Punguza matumizi yasiyo ya lzm eti ununye vitu vyote ndani Bado umpe 250, Bado 30 ya kusuka acha ujinga huyo mwanamke uwann hakushauri?
 
Yani unatuma laki 1 kwenu then ukweni hutumi kitu halafu unalalamika hiyo laki na nusu unampa mkeo haitoshi hata hujiongezi kuwa mkeo nae anatuma kwako laki 1 kila mwezi. Ngoma droo 😂
Sijaona wapi unampa mkeo hela ya pedi, chupi, kusuka, mafuta nk
 
Hairoshi elf5 Kwa siku na mko 3? 😳🤔
Mke,mume na mtt? Heee huyo ni mke? Anakukomoa?
Bado unampa 30 ya kusuka Kila mwezi?

Muongo
Punguza matumizi yasiyo ya lzm eti ununye vitu vyote ndani Bado umpe 250, Bado 30 ya kusuka acha ujinga huyo mwanamke uwann hakushauri?
Kaka tuwe makini na Hawa wanawake wa kuoa wengine wanaweza kuwa sababu ya umasikini na mikosj ya kutofanikiwa maishani.

Maana mpaka unajiuliza ni lini utatoboa Kwa aina ya mwanamke kama huyu.
 
Yani unatuma laki 1 kwenu then ukweni hutumi kitu halafu unalalamika hiyo laki na nusu unampa mkeo haitoshi hata hujiongezi kuwa mkeo nae anatuma kwako laki 1 kila mwezi. Ngoma droo 😂
Sijaona wapi unampa mkeo hela ya pedi, chupi, kusuka, mafuta nk
Ninampa 30K kila mwezi.

Namnunulia chupi mwenyewe.

Kwa Sasa Sina Hela ila nilikotoka nilikuwa naandaa hata 200K Kwa ajili ya shopping yake kwwa Sasa siko vizuri.

Home kwao natuma maana yuko mama yake ila mpaka nijisokie .

Nanunua vocha.

Kila kitu nafanya kwake na Kwa watoto.
 
Mshahara huo na dharura na laki nanusu mna mifugo kma Kodi unalipa,laki nanusu bills gani mkeo analipia maji na umeme?

Hebu kaeni chini elezeaneni uhalisia wa maisha
Na mkeo nae kama sio mlemavu akatafute Hela ajitume wanawake mjini wanauza maandazi wanauza chakula aende shule za jirani auze ice cream natamni kungekuwa na voice note aisee😀
Huyu sijui mkewe hajui Hali halisi au makusudi
Mke anajielewa lzm atamshauri
Familia ya mtt 1mdogo 😳🤔 nimeshangaa sn, matumizi Gani hayo?

Eti kusuka Kila mwezi 30😀 halafu mnajitafuta?huna mke hapo
 
Huyu sijui mkewe hajui Hali halisi au makusudi
Mke anajielewa lzm atamshauri
Familia ya mtt 1mdogo 😳🤔 nimeshangaa sn, matumizi Gani hayo?

Eti kusuka Kila mwezi 30😀 halafu mnajitafuta?huna mke hapo
Asante hapa Sina mke Wala sikubishii.

Maana nikaa na majamaa zangu unaona kabisa wanawake zao Wana madini ya kutosha.

Huyu mwanamke issue ya bajeti nimeanza kukogambana nae huu mwaka wa tatu.

Yaani ametoka familia masikini Tena sana zaidi yetu ila hana uchungu kabisa wa Hela jamani.

Mimi hata sielewi nifanyaje.

Ulimpa Hela 150K mwezi hauishi anakwambia imeisha.

Ukisema umpe elfu 5 Kwa siku bado anakwambia ndogo na hapo kila kitu Kiko ndani.

Yaani nakasirkka sana jamani
 
N

NIlianza hivyo mwanzoni ila nikaona kama namtesa mke wangu ila ilinisaidia.

Nilipoacha nimejikuta kwenye madeni Hela hazikai.

Mpaka nahisi nimelogwa itabidi nirudi Tena

Kwanza anayekwamisha maendeleo yangu ni huyu mke wangu

Maana kuna kipindi nilimwambka aniambie kiasi chake Cha siku Kwa chakula maana vitu vya muhimu vyote viko ndani akawa ananijibu upuuzi nilitamani nimpige.

Maana Mimi niliwahi kujitolea sehemu nilikuwa nalipwa laki 3 na ilinitosha yeye hana bajeti mwezi hauishi Hela inaisha yaani ana rough bajeti mpaka kuna muda nimeamua nikae na Hela niwe nampa kila asubuhi.
Nimepata jibu
Haiwezekani mke Ambae mnajitafuta asikushauri mbabe matumizi
 
Asante hapa Sina mke Wala sikubishii.

Maana nikaa na majamaa zangu unaona kabisa wanawake zao Wana madini ya kutosha.

Huyu mwanamke issue ya bajeti nimeanza kukogambana nae huu mwaka wa tatu.

Yaani ametoka familia masikini Tena sana zaidi yetu ila hana uchungu kabisa wa Hela jamani.

Mimi hata sielewi nifanyaje.

Ulimpa Hela 150K mwezi hauishi anakwambia imeisha.

Ukisema umpe elfu 5 Kwa siku bado anakwambia ndogo na hapo kila kitu Kiko ndani.

Yaani nakasirkka sana jamani
Duh yan hapo ndokurudishana nyuma miaka mitatu haelewi tu.
 
Mimi nimeacha kusali waifu ndo anasali maana nimeona miaka inaenda hakuna Cha maana ninachokuwa nacho hata kabla sijaajiriwa Tena nilikuwa na mshahara mkubwa tu.

Leo hii unaniambia niongeze 60K fungu la kumi.

Bado nauli ya kanisani.

Michango kibao wakijua wewe ni mtumishi
Na hapa ndo tatizo halisi. Nimefatilia kote namna ambavyo umeshusha waraka wa changamoto zinazokupata of which zipo kwa kila mtu. Mshahara ni mdogo kwa watu wengi sana ndugu. Na kuna mahali umeandika kuwa ulishakuwaga vizuri kiuchumi hapo nyuma.

Lakini pamoja na changamoto za mkeo, KAA ukijua yeye pia sio chanzo cha tatizo. Yeye ni mojawapo tu. Ukianza kumuona kama tatizo akati ukute hata hiyo rizki ama neema ya kazi imekuja kwa uwepo wake na m/watoto wako, utaondoa hizo blames kwake.

Neno linasema mjue sana Mungu ili uwe na amani na ndipo MEMA yatakapokujia. Kuacha kusali au kumsogelea Mungu mara nyingi hatumkomoi yeye, tunajikomoa sisi wenyewe, sema ni vile tunajikutaga sana pale ambapo tumepata neema zake kidogo tu.

Yeye Mungu ndie anaeweza kukupa mafunuo mazuri nini ufanye kumanage hiyo hali na kupata kipato extra for He says, "Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea, nitakushauri jicho langu likikutazama" Trust me, yumkini ulikuwa unasali sana kabla ya kupata hii kazi, sema frustrations kidogo tu ukatoka kwenye mstari, rudi! Budda, kunanyesha kila mahali, ni Bwana Mungu tu anayetusimamisha na si kingine, anatupa ile sanity na calmness mwenye hali zote tunazopitia. Kwa haya machache sijui ndo mengi, tafakari......
 
Yani unatuma laki 1 kwenu then ukweni hutumi kitu halafu unalalamika hiyo laki na nusu unampa mkeo haitoshi hata hujiongezi kuwa mkeo nae anatuma kwako laki 1 kila mwezi. Ngoma droo 😂
Sijaona wapi unampa mkeo hela ya pedi, chupi, kusuka, mafuta nk
Utoe mahari tena utume pesa ukweni hivi waafrika tumelogwa
 
Changamoto sisi watumishi wa serikali wanafiki ndo maana mama anatuacha.

Wengi mapambio serikalini kuisifia ccm wakati watu wanakufa njaa
Kusifia kunatokana na mambo matatu:
  • Njaa kali (mtu anaona akisifia labda atapata vifursa vya posho, visemina vya kazini na mambo ya sensa ,uchaguzi)
  • Ujinga tu, mtu hajielewi.
  • Watu wenye vicheo ambao ni wanufaika, au wanatumika kuiba hivho vimishahara vya wafanyakazi, kama vile haya mavyama ya wafanyakazi
 
kaa chini na mkeo mpange pamoja apate chakufanya na yeye mpunguziane majukumu vinginevyo utachoka mkuu na ukichoka utakinai familia wakati ni jambo la kuelewana tu
 
Back
Top Bottom