Watumishi wa serikali mliwezaje kutoboa, mbona mimi naenda kushindwa

Watumishi wa serikali mliwezaje kutoboa, mbona mimi naenda kushindwa

Huu uzi uwe fundisho kwa vijana wengine

1. Usikimbilie kuwa na mke kabla haujajipanga kuwa na vyanzo vingine vya mapato nje ya mshahara. Mishahara ya watumishi ni dusko dusko tu ili usife njaa.

Ni vigumu sana kwa mtumishi mwenye mshahara dusko kuwekeza akiwa na mke na familia maana kila ukitaka kujibana kwenye matumizi ili uwekeze unagundua mke na watoto nao wanakutegemea.



2. Jitahidi kigezo kimojawapo cha mke awe ni mfanyakazi au mfanyabiashara (ndogo au kubwa).

Huyu kuna muda atajiongeza ni kweli mume ni jukumu lako kuitunza familia lakini mke mwenye kati ya hivyo vigezo 2 atakupunguzia mkazo na mnaweza mkakaa mkayajenga namna ya kutengeneza bajeti ya familia yenu


Mwanamke ambaye hajui kuchakarika kwenye biashara hata uumtafutie mtaji ataufirisi na kukuacha na madeni



3. Ishi kulingana na kipato chako bajeti ni muhimu sana rahisisha maisha yako. ​
Madini mengi
 
Kutoboa m
Habari za jioni.

Nimeshindwa kupata usingizi kutokana na wimbi la mawazo.

Wakuu Take home yangu 613K Mimi ajira mpya mwaka jana ila nimekuwa na wimbi la mawazo na kuona kama sitaweza kutoboa labda nIpate washauri wengine wa maisha labda.

Nnafanya kazi mkoani,ila kadri siku zinavyoenda ninaona maisha magumu ilhali Mimi ni ajira mpya tu wa mwaka jana.

Nina mahitaji ya lazima mengi sana Nina familia ya mke na mtoto mmoja na ndugu wananitegemea.

Kila mwezi lazima.
Nitume nyumbani laki 1.
Nanunua chakula laki 150K.
Nampa mke wangu 150K ya matumizi na bills nyingine.
Kodi nimepanga chumba sebule 100K.
Sijaweka dharura Wala other charges.

Huu ni mwezi wa sita kazini sijanunua shati Wala Chochote juu ya familia yangu. Nimekuwa mtu wa mawazo na ninayeona nakuwa maskini kabisa.

Kazi yangu Ina posho ila ofisini wanatudhulumu tu hivyo hatuna Constant.

Jamani wazoefu naombeni mnishauri kama naona naenda kufeli mapema jamani.

Wengine mmewezaje?
Kutoboa ni process
Sio swala la kulala na kuamka
Tafuta side hustle, yakukuingizia angalau 300k per month

Ila usisubutu kukopa
 
Anza kupunguza hiyo ela unayotuma kwenu,huo uwezo hujafikia
Hata hiyo unayompa wife nayo punguza,badala yake uisave umfungulie hata genge hapo nyumbani
Mana ukiweza kusave 50k kila mwezi kwa miezi hata 6 unapata laki 3 inatosha kabisa kwa genge especially uko mkoani!
Huyu mke wangu mpuuzi sana nimeanza kazi tu mwaka jana akawa ananiforce nimfungulie biashara.

Nikamwambia kwa kuwa ni tunaanza maisha na tuliuza vitu vyote tulipotoka.

Nikamwambia tujibane Kwa miezi 6.
Tununue kitanda,godoro,sofa tv kwwa ajili ya mtoto basi.

Baada ya hapo nikamwambia kama tutajibana kwenye mia 4 per month tutumie laki 2 tutasave tukipata laki 5 nakufungulia biashara.

Ila napoongea hivi mwezi huu wa nne nimefanikiwa godoro na kitanda mwenzangu haiendani na mawazo yangu.

Nanunua kila kitu kuanzia umeme,maji

Lakini ulimpa hata 100K mwambia atoboe mwezi tar 10 imeisha.

Leo hii ameniachia madeni ameniachia kwenye kupambana yaani nachanganyikiwa Bora ningekuwa singo tu.
 
Kama mnaelewana vizuri na mkeo basis tafuta amani katika maisha yenu.Na amani huja kwa kumtambua Mungu ndiye mleta amani.Toa zaka wapende jirani nk.Fedha hazileti amani kama huna Mungu,hata kama utapewa 2m kama mshahara kwa mwezi.Lakini haya yanataka moyo wake uelewe na kuamua.
Mimi nimeacha kusali waifu ndo anasali maana nimeona miaka inaenda hakuna Cha maana ninachokuwa nacho hata kabla sijaajiriwa Tena nilikuwa na mshahara mkubwa tu.

Leo hii unaniambia niongeze 60K fungu la kumi.

Bado nauli ya kanisani.

Michango kibao wakijua wewe ni mtumishi
 
Mpe mke wako mtaji wa biashara hata kama ni genge asikae home tu. Mkubaliane kabisa kwa mwezi na yeye awe anatoa yani mnaweka vipato vyenu juu ya meza mnafanya bajeti pamoja. Mara nyingi wanawake wasiojua kutafuta pesa wanakuwa na matumizi mbaya ya pesa. Mpe jukumu la yeye kutafuta pesa ndio atajua uchungu wa kupata pesa na ataweka bajeti yake vizuri.
Ananikera sana nilishamfungua biashara mbili na zilifeli zote
 
Huyu mke wangu mpuuzi sana nimeanza kazi tu mwaka jana akawa ananiforce nimfungulie biashara.

Nikamwambia kwa kuwa ni tunaanza maisha na tuliuza vitu vyote tulipotoka.

Nikamwambia tujibane Kwa miezi 6.
Tununue kitanda,godoro,sofa tv kwwa ajili ya mtoto basi.

Baada ya hapo nikamwambia kama tutajibana kwenye mia 4 per month tutumie laki 2 tutasave tukipata laki 5 nakufungulia biashara.

Ila napoongea hivi mwezi huu wa nne nimefanikiwa godoro na kitanda mwenzangu haiendani na mawazo yangu.

Nanunua kila kitu kuanzia umeme,maji

Lakini ulimpa hata 100K mwambia atoboe mwezi tar 10 imeisha.

Leo hii ameniachia madeni ameniachia kwenye kupambana yaani nachanganyikiwa Bora ningekuwa singo tu.
Singo tena aiwezekani we kaa nae chini umueleweshe.
 
Habari za jioni.

Nimeshindwa kupata usingizi kutokana na wimbi la mawazo.

Wakuu Take home yangu 613K Mimi ajira mpya mwaka jana ila nimekuwa na wimbi la mawazo na kuona kama sitaweza kutoboa labda nIpate washauri wengine wa maisha labda.

Nnafanya kazi mkoani,ila kadri siku zinavyoenda ninaona maisha magumu ilhali Mimi ni ajira mpya tu wa mwaka jana.

Nina mahitaji ya lazima mengi sana Nina familia ya mke na mtoto mmoja na ndugu wananitegemea.

Kila mwezi lazima.
Nitume nyumbani laki 1.
Nanunua chakula laki 150K.
Nampa mke wangu 150K ya matumizi na bills nyingine.
Kodi nimepanga chumba sebule 100K.
Sijaweka dharura Wala other charges.

Huu ni mwezi wa sita kazini sijanunua shati Wala Chochote juu ya familia yangu. Nimekuwa mtu wa mawazo na ninayeona nakuwa maskini kabisa.

Kazi yangu Ina posho ila ofisini wanatudhulumu tu hivyo hatuna Constant.

Jamani wazoefu naombeni mnishauri kama naona naenda kufeli mapema jamani.

Wengine mmewezaje?
Kwanza pole sana kwa hii changamoto unayopitia,
Najua umeshapata ushauri wa kutosha sana kutoka kwa wadau namna gan ya kufanya ili mambo yakae vzr
Nataka kusisitiza tu kwenye swala la MIKOPO usije ukathubutu kujihusisha haraka haraka unaona unavyohangaika saiz itakuwa mara mbili yake
Haujagusia hili swala ila kwa dalili hizo unakoelekea ni kwenda kukopa hii itakupa depression kubwa sana.

Pesa ya mkopo hasa kwa watumishi wa umma asilimia kubwa huwa wanafurahia maisha kwenye ile miez miwili ya mwanzo tu after hapo ni huzuni kubwa sana hasa kwa take home yako hiyo changa karata zako vzr mkuu ila usijae kwenye mfumo haraka haraka.
Asante.
 
Weka lengo la kutonunua chakula. Ule cha kujilimia( maharage, mahindi, kunde, njegere nk). Kila mkoa kuna mazao yanastawi.
Lima hata nusu heka ya kula familia yako tu. Lima viazi vitamu hata robo heka.
Panda mboga mboga hapo nyumbani
Panga nyumba yenye space( pembezon mwa mji).
Futa tatizo la kununua nyama kwa kuanza kufuga kuku 5 tu, sungura 3.
Kuku 5 ndani ya miezi 6 utakuwanzo 40, hawa totally kienyeji utawasapoti chanjo tu na dawa za mafua hasa msimu huu wa mvua.
Hili ni zoezi analoweza fanya mkeo kama hana kazi.
Baada ya mwaka 1 utakuwa hununui tena vyakula vya kila siku labda mchele, mafuta ya kula no.
Huwezi hayo anzisha biashara ndogo ndogo hata kuuza nyama choma, au. Chips eu juisi nk. Usiwajali unaofanya nao kazi hawatakupa hela, wafanye kuwa wateja wako.
Learn other skills kama ufundi mdogo mdogo kama simu, tv, computer, kukarabati viatu , ushoni wa nguo nk.
Anzisha genge la kuuza nafaka, mkaa na matunda.
Huwezi jifunze udalali, kuuza mitumba nk.
Hizo ndizo dili za watanzania wengi kipenzi cha Mama Samia.
Hapo ndio kwanza picha linaanza usiombe mzazi/ mke/ mtoto aje apate gonjwa la ajab utajuta.
Nawazaga sana mzazi akiumwa na Sina backup yoyote ile.

Nitaifanyia kazi ushauri wako mkuu.

Niko makao makuu ya mkoa kutoka nje ya mji lazima niingie gharama za usafiri
 
Habari za jioni.

Nimeshindwa kupata usingizi kutokana na wimbi la mawazo.

Wakuu Take home yangu 613K Mimi ajira mpya mwaka jana ila nimekuwa na wimbi la mawazo na kuona kama sitaweza kutoboa labda nIpate washauri wengine wa maisha labda.

Nnafanya kazi mkoani,ila kadri siku zinavyoenda ninaona maisha magumu ilhali Mimi ni ajira mpya tu wa mwaka jana.

Nina mahitaji ya lazima mengi sana Nina familia ya mke na mtoto mmoja na ndugu wananitegemea.

Kila mwezi lazima.
Nitume nyumbani laki 1.
Nanunua chakula laki 150K.
Nampa mke wangu 150K ya matumizi na bills nyingine.
Kodi nimepanga chumba sebule 100K.
Sijaweka dharura Wala other charges.

Huu ni mwezi wa sita kazini sijanunua shati Wala Chochote juu ya familia yangu. Nimekuwa mtu wa mawazo na ninayeona nakuwa maskini kabisa.

Kazi yangu Ina posho ila ofisini wanatudhulumu tu hivyo hatuna Constant.

Jamani wazoefu naombeni mnishauri kama naona naenda kufeli mapema jamani.

Wengine mmewezaje?
Papa Francis na ukubwa wake wote amwfariki na utajiri wa dola 100 pekee.
 
Singo tena aiwezekani we kaa nae chini umueleweshe.
Kaka Haieleweki ugomvi Mimi na yeye Kila siku Tena wote tumetoka kwenye maisha magumu sana lakini nashangaa kwanini mwenzangu sio mzuri Kwa bajeti
Nilikuwa najitolea sehemu X wananilipa laki 2 nikiwa singo na nilitoboa vizuri tu.

Leo mwenzangu bajeti ni somo ameshindwa kabisa.
 
Sasa kama ndio unaanza kazi, unapata 613,000 unalia,

Siku ukikopa ukaanza kupata mshahara wa laki na nusu kwa mwezi mbona utajiua kabisa.

Najua wewe ni CO, na hiyo ndio tske home.

Mimi napata salary 260 000.

Nilikuwa na mshahara kama wako.

Nilikopa bank, nikaenda kununua viwanja nikatapeliwa.

Sasa hivi nalipa deni na kiwanja sina. Nimepambana lakimi nchi hii huwezi kupata haki, unadhulumiwa na aliyekudhulumu yupo anadunda na huna cha kumfanya.

Na nina mke na mtoto.

Na sijafa. Nipo tu natuliza moyo maisha mengine yaendelee.

Ushauri wangu.

Kama 613,000 take home haikutoshi, usije kukopa tena mkopo wa muda mrefu, maana bank za sasa zinakopesha mpaka mika 10, utakufa kabisa, maana utaanza kupata 200,000 wakati deni lako la bank halitaisha.

Na kama una passion ya biashara na uko mkoa mzuri au mkeo jichange ufanye kitu. Au kama una passion ya kilimo na mkoa unaruhusu lima.

Mimi niko Kilimanjaro, huku huwezi kulima hata bustani, kufuga wala biashara.

Naishi hivyo hivyo na 260,000 changu kwa kujibana.

Na usije ukawa na matumizi makubwa, sana, kadi yako ya bank itaishia kwa wakopeshaji wahuni wa mtaani, utashindwa kulipa kodi ya nyumba, itaonekana daktari njaa kali kinomaaa.

Na option ya madaktari huwa ni kuanza kupiga dili haramu, kama kutibu wagonjwa nje ya mfumo, kutoa mimba, na kuuza dawa kimchongo maisha yaende.

Utakuha kuanza kypata migogoro na wakuu wa wilaya, waganga wafawidhi, waganga wakuu wa wilaya na TAKUKURU. Utaanza kuhamishwa hamishwa vituo vya kazi kwa adhabu na Utapoteza focus na utaona kazi chungu.

Option kwa kipato kidogo huwa ni 2:
  • Kubana matumizi ya kipato ulicho nacho (njia rahisi) au
  • Kuongeza kipato chako (njia ngumu)

Pambana kujibana katika matumizi yako.
Asante kaka nashukuru kwwa huu ushauri nimeupokea kaka
 
Mzee.

Mungu anisamehe ila naona kama mzzigo.

Mengine siijayaweka wazi.

Ila nshawahi pata kazi mshahara wa million biashara mbili nilimfungulia na zilikufa aisee.

Nimedrop.sana kiuchumi.

Ila
Duh hapo jaribu kumfundisha najua tayar umeshajua wap anadondoka.
 
Mleta uzi unabet.

Watu wawili na mtoto mdogo mnatumia chakula 150K kila mwezi?

Kuna expenses haujazisema. Na ninahisi ni kubet.

Hii ni ajira ya kwanza?
Sibeti kaka.
Mshahara ukitoka.

1.CHAKULA.
Michele 2200×20=44000
Sukari kilo 5 ×3000=15000
Mafuta lita 5 =30K
Unga =15K
Gas 25K
Tambi 8000
Maji 5000
Umeme 1000
Maahrage 15K
Waifu Nampa 30 ya kusuka
Dogo pampas 5K per week

Na hapo ninamwachia waifu 150K Kwa kigezo Cha kununua nyama ,au samaki sabuni Kwa ajiri ya kubadilisha mbona Kwa maana elfu 5 Kwa siku na huyu ananiambia eti haitoshi Sasa ni kweli kabisa issue kama hii.

Kodi ndo nalipa laki 1.



Umeona hiyo bajeti mkuu
 
Back
Top Bottom